LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

01/29/09

MWANSASU AJA NA WOSIA WA BABA


Hakuna asiyeelewa kwamba mkoa wa Mbeya ni mkoa ambao umekuwa ukitoa waimbaji mahiri wa muziki wa injili wenye tungo ambazo msikilizaji wa nyimbo hizo huwa hachoki kila anapozisikiliza.(Ephraim Mwasasu kulia akiimba kwa hisia kali)
Na kama wewe ni mpezi wa muziki huo naamini utaungana nami katika hili kwa sababu kila ukisikiliza nyimbo zenye mauzui mazito yanayowarejesha kwa Mungu watu waliopotea katika dimbwi la dhambi, ukiuliza ni nani kaimba wimbo huo, utasikia majina yanayoanza na Mwa…
Lakini wengi wameibuka miaka ya 2000 na kuliteka anga la muziki wa injili ndani na nje ya nchi. Miongoni mwa waimbaji hao ni Ambwene Mwasongwe, Bony Mwaitege, Ency Mwalukasa, Bahati Bukuku na wengine wengi.
Pamoja na majina hayo kuonekana kutesa katika anga hilo, lakini jina la Ephraim Mwasansu ni miongoni mwa majina ya waimbaji wa muziki wa injili nchini ambao hawachuji kila itwapo leo, na hiyo ni kutokana na umahiri wake wa kutunga nyimbo zenye mvuto na ujumbe mzito wa neno la Mungu na zisizochuja haraka.
Mwimbaji huyo ambaye huduma yake ya uimbaji ilianza tangu akiwa mtoto, alifanikiwa kurekodi albamu yake ya kwanza mwaka 1998 iliyojulikana kwa jina la Tutatesa milele ambayo ilionekana kuwashika watu wengi hali iliyomshawishi aingie tena studio mwaka 2001 na kufyatua albamu iliyojulikana kwa jina la Umepoteza namba.
Albamu hiyo nayo ilitikisa anga la muziki wa injili na kumpa moyo tena wa kuingia studio na kurekod albamu ya tatu aliyoipa jina la Msigombane ambayo bado inatesa katika anga la muziki ndani na nje ya nchi.
Hata hiyo Mwansasu ameamua kuifumua albamu yake ya pili inayojulikana kwa jina la Umepoteza namba baada ya kuonekana haina ubora wa kutosha na ametunga nyimbo nyingine tano ambazo zitakuwemo katika albamu ambayo ameipa jina la Wosia wa Baba.
Mwansasu ambaye sasa ni Mchungaji wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania lililopo Riverside jijini Dar es Salaam, alisema katika albamu hiyo atabakiza nyimbo tatu, ambazo ni Watoto wachanga, Umepoteza namba na Yumwema, ambapo nyimbo mpya ni pamoja na Wosia wa Baba unaobeba jina la albamu, Sitasahamu, Dunia ya sasa, Nakushukuru Mungu na Haleluya ulioimbwa kwa lugha ya kinyakwisa.
Safu hii ilitaka kujua ni kwa nini ameamua kuita Wosia wa Baba, Mwansasu alisema, kuna wosia ambao Mungu amempa kwa ajili ya kuwafikishia wanadamu ujumbe huo, ina inatarajia kukamilika mwezi April 2009.
Akielezea juu ya nyimbo zake kuendelea kuonekana kuwa ni mpya kila itwapo leo, Mwansasu alisema, siri kubwa ni kukaa katika unyenyekevu wa Mungu na kutobeza huduma za watu wengine.
Akielezea juu ya waimbaji wanaomkuna katika fani hiyo ya muziki wa injili, Mwansasu alisema anafurahishwa sana na huduma ya David Masaga Nyanda, David Robert na Fenuel Sedekia kutoka na miziki yao isiyoyumbishwa na kizazi cha sasa.
Mwansasu alisema kuwa si kwamba waimbaji wengine hawapendi isipokuwa hao aliowataja wanamvutia zaidi katika utunzi wa tungo zao nzuri na pamoja na staili yao ya uimbaji kuikubali wao wenyewe na nyimbo zao zikitoka huwa zinakubalika katika jamii.

KING'S MASSANGER


Maelezo ya kwaya hii nitakuletea muda si mrefu

DISCIPLES TEAM

Hakuna asiyeelewa Kwamba miaka ya hivi karibuni muziki wa injili umekuwa ukipanda chati kila kukicha, kutokana na kupata idadi kubwa ya wapenzi wa muziki huo ambao wamekuwa wakizifuatilia nyimbo za injili kwa makini pengine kuliko ile ya kidunia.
Nadhubutu kusema hivyo nikiwa na vigezo vya kutosha juu ya
hilo na moja ya vigezo hivyo ni kufanya vizuri katika soko la muziki hapa nchini pamoja na nje ya nchi.
Leo hii ukipita katika maduka ya kuuza kanda, nyimbo ambazo utasikia zikipingwa ni zile za injili, hiyo ikiwa ni pamoja na wanunuaji wa kanda za jumla mara nyingi wamekuwa wanunua za muziki wa injili kuliko wa kidunia.
Lakini pamoja na mafanikio hayo ambayo kwa namna moja ama nyingine yameonekana kuwapatia a
jira baadhi ya waimbaji wa muziki huo, bado kundi la Disciples linasema sanaa ya maigizo inalipa zaidi kuliko nyimbo za injili.
Kundi
hilo linasema limekuwa katika sanaa ya maigizo kwa muda mrefu na limepata mafanikio kwa kiasi fulani, na siku za hivi karibuni limejiingiza katika harakati za kulihubiri neno la Mungu kwa njia ya uimbaji.
Akizungumza na safu hii kwa niaba ya wenzake, kiongozi wa kundi hilo Lazaro Philemon (Kibiwi), alisema pamoja na kwamba wapo katika sanaa ya maigizo, shauku yao ni kuhakikisha wanauona ufalme wa Mungu siku ya mwisho.
Alisema maigizo wanayoigiza yamelenga kulitanga jina la Mungu kwa njia hiyo na ndio maana wameamua kujitumbukiza tena katika fani ya muziki wa injili ili kupanua wigo wa mahubiri kwa njia ya sana
a.(DISCIPLES TEAM wakiwa katika picha ya pamoja)
Kiongozi huyo wa kundi la Disciples alisema sanaa ya maigizo waliianza mwaka 2003 kipindi hicho wakiwa shuleni, na tangu kipindi hicho wamekuwa wakitembea kila pembe ya nchi na nje ya nchi kwa lengo la kulihubiri neno la Mungu.
Mwaka 2008 mwanzoni kundi
hilo limefanikiwa kurekodi albamu moja iliyopewa jina la Sadaka ikiwa na nyimbo nane.
Nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni, Kuna swali, Mbele yake, Aliteseka, Kilio, Vitani, Simama mwenyewe, Heri kuwa na Yesu na Sadaka ambao umebeba jina la albamu.
Wasanii wanaounda kundi hilo ni Philip Dilunga, Godfrey Lwiza, Mshana Chakupewa, Lazaro Philemon, Godfrey Sekumbo, Dions Bundara na Naomi.
Wasanii hao kwa pamoja waliiambia safu hii kwamba tangu waingie katika fani ya muziki wa injili, hawajapata faida kubwa ya kipato
kama wanachokipata katika sanaa ya maigizo hali ambayo wanaona sanaa ya maigizo ni bora zaidi ya muziki wa injili.

Newer Posts Older Posts