LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

01/31/09

PAPA JONAS LUTUMBA KUIPUA DVD,VCD & VHS

Kila kukicha ukifungua vituo vya radio za dini hapa nchini, utasikia matangazo ya matamasha yakitangazwa kwa lengo la uzinduzi wa albamu za waimbaji wa muziki wa injili.
Ukichunguza kwa undani zaidi juu ya matamasha hayo, utabaini kwamba, waandaaji hulenga kujipatia fedha za chapuchapu ili wajinasue na dimbwi la umasikini.
Nasema hivyo nikiwa na ushahidi kwamba baadhi ya waimbaji wa muziki wa injili miaka hii wamekuwa wakitunga nyimbo zao kwa kuangalia ni kwa jinsi gani watachomoza katika anga la muziki huo.
Safu hii, ilifanikiwa kuzungumza na mwimbaji wa muziki huo Papa Jonas Lutumba, ambaye naye bila kuficha alisema kuwa watu hao miaka ya hivi karibuni, wameibuka
kama uyoga na kuwafanya waimbaji wa muziki huo waangushiwe shutuma yakuwa wamekuwa wakipenda fedha zaidi kuliko kuangalia huduma.
Papa alisema kuwa, kitendo cha waimbaji hao wanaoibukia katika fani hiyo kuanza tabia ya kutanguliza fedha badala ya kuangalia huduma ya Mungu, kunaidhalilisha uimbaji na kuonekana haina heshima katika jamii.
Mwimbaji huyo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC
Congo), anayeishi hapa nchini alisema kuwa, waimbaji hao, wamekuwa waiipaka matopete huduma ya muziki wa injili na kuonekana si kitu, na ndio maana mifano mingi mibaya, watu wengi wamekuwa wakiwatolea watumishi hao wa Mungu.
Akizungumzia historia yake ya wokovu, Papa alisema, huduma ya kumuimbia Mungu wake alianza mwaka 1996 baada ya kuokoka. Hata hivyo si kwamba uimbaji ulianza mwaka huo, la hasaha, bali kabla ya wokovu alikuwa akiimba katika bendi ya Mosha Star ya DRC
Congo mwaka 1990.
Papa Lutumba tayari amefanikiwa kurekodi albamu tatu ambazo tayari ziko sokoni. Albamu hizo ni Mungu wangu aliyoitoa mwaka 2004, Wakati wa Neema aliyoirekodi mwaka 2006 na Nikumbuke aliyoifyatua mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na safu ya Gospel Fleva Papa alisema albamu yake ya tatu inayokwenda kwa jina la Unikumbuke, mwanzoni mwa mwezi Fabruari inatarajiwa kuingia mtaani ikiwa katika DVD, VCD na VHS na maandalizi yote yamekamilika.
Akielezea juu kuhusu mauzo ya kazi za muziki wa injili, Papa alisema kwa Tanzania soko si kubwa sana ukilinganisha na nchi kama Kenya na Kongo, kutokana na ukosefu wa ushindani wa wasambazaji wa kazi hizo.
Hata hivyo Papa alisema kwamba Waimbaji wa muziki wa
Tanzania wao wanafaida kubwa ya kuwa na studio nyingi za kurekodia muziki tofauti na Kongo ambapo studio ni chache hali ambayo husababisha kazi ya kurekodi kuwa ngumu.

MCHUNGAJI JAMES MWAIPYANA


KUTOTII SAUTI YA MUNGU KUMEWAPONZA WAKRISTO WENGI.

Imeelezwa kuwa kitendo cha kutotii sauti ya Mungu kumewaponza wakristo wengi kuishi maisha ya dhiki kwa kuonewa na Ibilisi, nakujikuta wanalalamika kwamba Mungu hawasikii kila wanapomuita hali ambayo wengine hujikuta wanaachana na wokovu na kujitumbukiza katika imani za kishirikina.(Mchungaji James Mwaipyana Kulia akihubiri Neno la Mungu katika kanisa la Glory Temple Tabata)
Mchungaji James Mwaipyana wa kanisa la Glory Temple Tabata aliyasema hayo hivi karibubuni wakati wa mahubiri yaliyofanyika kanisani hapo na kuongeza kuwa kitendo cha wakristo kushindwa kuisikiliza sauti ya Mungu kunatokana na wahusika kushindwa kutofautisha kati ya sauti ya Mungu na sauti ya Ibilisi kutokana na kutopata elimu ya kutosha juu ya kuitambua sauti ya Mungu.
“ Wakristo wengi leo hii wamekuwa wakilia na matatizo wanayoyapata maishani mwao na wengine wamelazimika kuacha wokovu baada ya kuona wamefanya maombi kwa muda mrefu bila majibu na kudhani kwamba Mungu hawasikii, huku wakishindwa kutambua kuwa Mungu husema nao juu ya kilio chao bila wao kujitambua,” alisema Mwaipyana.
Mchungaji Mwaipyana alisema mbali na kutotii sauti ya Mungu, wakristo wengi wamekuwa na imani zenye mashaka ambazo kwa asilimia kubwa zimekuwa zikichelewesha miujiza yao na kuendelea kuishi maisha ya dhiki huku wakiwashuhudia wale wenye imani kali wakifanikiwa kwa kila wakiombacho kwa Mungu wao. (Mchungajia Mwaipyana kushoto akiwa na Mzee Kiongozi wa kanisa hilo Mzee Kapama wakiwa nje ya jengo la kanisa hilo)
Alisema hali hiyo ndio imewafanya wakristo wengi kuwa masikini kutokana na kitendo hicho cha kuwa na imani haba kwa kile wanachokiomba ikiwa ni pamoja na kushindwa kuisikiliza vema sauti ya Mungu ambayo hutoa maelekezo ya nini cha kufanya ili kujinasua na hali wanayopitia.
Aidha Mwaipyana alisema wakati mwingine Mungu hawaamusha watu usiku ili kuombea jambo ambalo liko mbele yao, lakini hujikuta wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kuzidiwa na usingizi mzito, na jaribu kubwa linapowakuta hujikuta wanamnung’unikia kuwa kwanini anaruhusu hali kama hiyo.
“ Inasikitisha kuona kwamba Mungu hulazima kuwaamusha watu nyakati za usiku pindi anapoona kuna jambo la kuombea kabla halijatokea, lakini mhusika huamuka na kujikuta analala na kupatwa na usingizi mzito na jaribu linapompata anaanza kunung’unika kwamba kwanini Mungu ameruhusu hali hiyo,” alisema Mwaipyana.
Mchungaji huyo alisema kila itwapo leo Mungu huwa ana mbinu mpya kwa ajili ya watu wake ili kuhakikisha wanaishi maisha ya raha, lakini wahusika wamekuwa wakishindwa kufuata kila Mungu anachowaelekeza.

Newer Posts Older Posts