MUZIKI WA INJILI HAUWEZI KUPOROMOKA KAMA BONGO FLEVA
Muimbaji wa muziki wa injili nchini John Shabani amesema kuwa, muziki huo hauwezi kuporomoka kama ilivyo kwa bongo fleva. Alisema tofauti na miziki mingine muziki wa injili unagusa sana hisia za watu wengi na unabadili maisha yao. Katika hatua nyingine mwimbaji huyo alisema kuwa,baadhi ya waimbaji wa muziki wa injili hubweteka pindi wanapopata mafanikio makubwa baada ya albamu zao kufanya vizuri.
