LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013
WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.
JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA
KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.
ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.
IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404
REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI
09/25/09
WOSIA WA BABA IKO TAYARI
Gospel Music Center 0
Muimbaji wa muziki wa Injili nchini ambaye pia na Mchungaji Efraim Mwansasu wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (E.A.G.T) River Side Ubungo, Jijini Dar-es-salaam tayari amekamilisha albamu yake mpya inayoenda kwa jina la Wosia wa Baba ikiwa na vibao vinane. Kwa habari zaidi juu ya upatikanaji wa albamu hiyo, endelea kutembele blog hii.
Rosemary Nyato alia na Studio
Gospel Music Center 0
Lakini maono ya watu hao yamekuwa yakikwamishwa na wajanja wachache ambao wamekuwa wakiendesha maisha yao kwa kupitia mgongo wa wasanii hao.
Katika hali ya kusikitisha kumbe wasanii hawa, wanapati matatizo kwa wasambazaji peke yao, eneo lingine ambalo watu hawa wamekuwa wakitabika ni studio. Eneo hili kwa kiasi fulani nalo limeonekana kuwa ni kero kubwa kutokana na ratiba za kurekodi kutokuwa katika mpangilio uliokamilika.
Hivi karibuni, muimbaji huyu wa muziki wa Injili nchini Rosemary Nyato ambaye kwa uchungu mkubwa alielezea jinsi waimbaji wanavyotabika kipindi cha kurekodi nyimbo zao, alisema kuwa, hali hiyo imekuwa kero kubwa kwa wasanii kutokana na kuwavurugia mtiririko mzima wa kuifanya kwa ufasaha kazi hiyo.
Mwanamama huyo alisema kuwa, asilimia kubwa baadhi ya studio zimekuwa zikididimiza maono ya waimbaji hasa wa muziki wa injili kutokana na kauli za nenda rudi na wakati mwingine muimbaji hujikuta anaimba akiwa amekwazika na kupelekea albamu yake itoke ikiwa katika kiwango cha chini tofauti na matarajio yake.
“Unajua mbali na tatizo la wasambazaji kutuibia kazi zetu, lakini kero nyingine ambayo imeonekana kutukatisha tamaa wasanii hapa nchini, kwa sababu wakati mwingine muimbaji huchukua mwaka mmoja akiwa studio anahangaikia suala la kurekodi pasipo mafanikio,” alisema Rose.Muimbaji huyo aliwataka wahusika katika studio kurekebisha tabia hiyo chafu ambayo kwa namna moja ama nyingine imeonekana kuondoa utayari wa msanii kutoa kitu kilicho bora na badala yake anakuwa na bora albamu na kujikuta anapata wakati mgumu katika kuiingiza sokoni.
Rose alisema kuwa, pamoja na kwamba majira haya kuna studio nyingi ambazo zimekuwa katika hali ya kushindana kutokana na kujitangaza kupitia vyombo vya habari, lakini imekuwa ni vigumu kubaini ni studio ipi ambayo inausumbufu pindi msanii anapoenda kurekodi kazi yake.
Akizungumzia suala la waimbaji wenye majina makubwa kuwabeza wale wachanga, Rose alisema kuwa, kitendo kimekuwa kero kubwa katika huduma ya kulieneza jina la Bwana, kwa sababu Neno la Mungu limeagiza wote kuwa wamoja, lakini mambo yamekuwa yakionekana yako kinyume na maagizo hayo.
Rose alisema kuwa, waimbaji ambao Mungu amefanikiwa kuwainua kwa asilimia kubwa wamejikuta wakijikweza, hali inayopelekea hata katika matamasha hualikana wao kwa wao na kuwaacha wasanii wachanga wakihangaika licha ya kuwa na nyimbo zenye jumbe nzuri.
Aliwataka waimbaji hao waliofanikiwa kukubalika katika jamii kuwasaidia waliochini yao ili, wote kwa pamoja waweze kulihubiri vema Neno la Mungu kupitia huduma ya uimbaji.
Kana kwamba hilo hali toshi, msanii huyo alionekana wazi kukerwa na tabia ya waimbaji hao kutamka pesa kubwa pindi wanapoalikwa kwenye shughuli hasa za kiroho.
Alisema kuwa, imekuwa ni kawaida kwa waimbaji hao kutaja kiwango kikubwa cha fedha pindi wanapohitajika sehemu, ambapo nako huwa wanaimba wimbo mmoja tu na kushindwa kukidhi kiu ya watu waliomualika kwenda katika shughuli hiyo.
Katika hatua nyingi, muimbaji huyo ambaye yupo mbioni kukamilisha albamu yake aliwataka wasanii wa muziki wa injili kutunga nyimbo zenye ujumbe mzito ambao unaweza kuponya na kuwapa faraja watu waliovunjika moyo badala ya kuwa na nyimbo za kuchangamsha peke yake.
Alisema kuwa, waimbaji wengi siku hizi wamekuwa wakiangalia soko zaidi na kutunga nyimbo za kuwasisimua watu bila kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuwa hubiri watu kwa njia hiyo ya uimbaji.
Msanii huyo alimaliza kwa kusema kuwa, waimbaji kuacha kukurupuka kwenda studio kurekodi nyimbo za ujumbe wa Mungu kwa lengo la kufanya biashara, kwa sababu hata kama muimbaji akiwa na nyimbo za taratifu watu wanaweza kuzipenda bila kuangalia ni kwa jinsi gani wanasisimka pindi wanapokuwa wanazisikiliza.
Rose alitoa mfano kwa waimbaji kama Christina Shusho, marehemu Fanuel Sedekia, Abiudi Misho na Jackson Benty ambao nyimbo zao ni za taratibu lakini zinakubalika sokoni.
WALIOTEMBELEA BLOG HII
TUMA HABARI NA MATUKIO
KAMA UNA HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI POPOTE DUNIANI TUMA KWA EMAIL HII. productiongmk@gmail.com. NAMI NITAZIWEKA KWENYE BLOG HII BILA GHARAMA YOYOTE. NAKARIBISHA HABARI ZA MATAMASHA YA INJILI, MIKUTANO, RATIBA ZA MAKANISA, SEMINA, HARUSI NA MAMBO MBALIMBALI KWA AJILI YA KUWAJULISHA WANAULIMWENGU. WASILIANA NAMI KWA NAMBA ZIFUATAZO.
+255 712 001 880,
+255 755 240 136.
HABARI MUHIMU
-
Wapendwa katika Yesu Kristo leo nimefanikiwa tena kukutana na muimbaji wa muziki wa Injili nchini anayekwenda kwa jina la Upendo Nkone ambay...
-
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Efatha Ministries anayetikisa jijini la Dar es salaam na amejikusanyi waumini wengi kiasi kwamba huduma...
-
Aliyekuwa muimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini Fanuel Sedekia alizikwa Januari 10 mkoani Arusha baada ya kufariki dunia usikua wa kua...
-
Nivigumu kuamini lakini ukweli ni huo kwamba, mtoto mmoja wa miaka 10, Anna Msingwa aliyezaliwa akiwa kipofu ameanza kuona huku Iringa, kwa...
-
Hakuna asiyeelewa kwamba mkoa wa Mbeya ni mkoa ambao umekuwa ukitoa waimbaji mahiri wa muziki wa injili wenye tungo ambazo msikilizaji wa ny...
-
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Kenya , Solomon Mukubwa leo (Jumamosi) anafunga pingu za maisha na Bi. Betyy katika kanisa moja la Kir...
-
Ndoa ni nini? Ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke unaokubalika kiutamaduni na kidini ambao unatarajiwa kudumu, kuwapa haki sawa za kiji...
-
Kwa wapenzi wa muziki wa injili nchini, jina la Shusho si jina geni masikioni mwao kutokana na umahiri wa kutumia kipawa cha uimbaji cha mwa...
-
Baraka akiwa na mwanaye Deliver akiwa nyumbani kwake mkoani Mbeya Deliver Baraka akiwa katika pozi safi Deliver Baraka ...
-
Baada ya kukaa kimpya kwa muda mrefu bila kutoa albam mpya na kupelekea baadhi ya wadau wa muziki wa Injili kuhoji uwepo wa Bony Mwaitege ka...
Categories
- George Kayala (23)
- George Kayala. (6)
- Kabula John George (1)


