LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

10/16/09

HAKUNA MUWEZA - KABULA J.GEORGE

Ninani mwenye uwezo kama wa Mungu? Pengine wewe ni miongoni mwa watu wanaopitia majaribu magumu kiasi kwamba unatamani kujiua kutokana na kuona huna tena msaada baada ya kuhangaika huku na kule. Yawezekana umeenda kwa waganga wa kienyeji, umetafuta msaada kila kona hajafanikiwa, lakini leo nakuambia kuwa, matatizo unayopitia ukimkabizi Jehova sasa hivi hutakuwa kama ulivyoamka asubuhi. Nijambo gani lililogumu kisia kwamba Mungu ashindwe kukusaidia? Hakuna. Sasa ungana na Mtumishi wa Mungu Kabula katika wimbo wake wa HAKUNA MUWEZA. Urudie mara nne kwa makini kisha liangalie  tatizo lako kama litaendelea kukusumbua ukisha fahamu uweza wa Mungu.

DHIHIRISHA - KABULA J.GEORGE

 Yawezekana una muda mrefu ndani ya ndoa yako ukiwa huna mtoto, pengine jirani, rafiki ama ndugu zako wanakubeza kutokana na maisha magumu unayopitia. Nakuomba usikilize wimbo huu kwa makini ikiwezekana urudie mara sita huku ukiwa umeuachia moyo wako upokee ujumbe uliomo ndani ya wimbo huu. Watu wengi Jehova amewafungua vifungo vyao baada ya kuusikiliza kwa utulivu. Ukisha sikiliza mwambie na mwenzako, nakushauri ununue DVD ama VCD ili usikilize kwa utulivu nyumbani kwao ama ndani ya gari lako.

TUNAISHI KWA NEEMA- KABULA J.GEORGE

 Mtumishi wa Mungu Kabula amekuwa miongoni mwa waimbaji wachache wa muziki wa Injili ambao nyimbo zao zikiimbwa huambatana na nguvu ya Mungu. Usikilize kwa makini wimbo huu naamini hutatoka kama ulivyoanza kuuangalia.

ROSEMARY: NITAMTUMIKIA MUNGU MPAKA SIKU YA MWISHO

WAIMBAJI wengi wa muziki wa Injili wamekuwa wakijiingiza katika huduma hiyo kwa kusaka masilahi zaidi kuliko kulihubiri neno la Mungu kwa njia hiyo.
Kutokana na hali hiyo ndiyo maana baadhi yao wamekuwa wakitunga nyimbo kwa kulenga biashara na kufanya usanii wa hali ya juu wakati wa kurekodi vibao vyao na ukivisikiliza kwa haraka utajua kama ni uimbaji ndiyo huo.
Nasema hivyo nikiwa na ushahidi wa kutosha juu ya waimbaji wa muziki wa injili ambao wameamua kuivamia huduma hiyo baada ya kuona kuwa inakubalika katika jamii ukilinganisha na muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva).
Na ukitaka kujua nyimbo za waimbaji wa muziki huo wa kumtukuza Mungu kama wanafanya kama biashara, utasikia nyimbo zinazoenda na nyakati ama matukio yanayoizunguka jamii na pindi hali hiyo ikiisha nyimbo hizo hupotea kutokana na majira yake kupotea.
Pamoja na kuwa na kundi kubwa la waimbaji ambao kila kukicha wamekuwa wakiwaza kutunga nyimbo ambazo zitawatoa kimaisha, baadhi yao wamekuwa wakimwomba Mungu awape vibao ambavyo vitafanyika msaada mkubwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali wakiwemo waliokata tamaa ya kuishi kutokana na kuzongwa na majaribu ya kila iitwapo leo.
Miongoni mwa waimbaji ambao wanafanya huduma ya kumuimbia Mungu kwa kutumia gharama zao ili kuhubiri neno la Mungu kwa njia hiyo ni, Rosemary Nyato mpakwa mafuta wa Bwana ambaye amekubali kujitoa kuieneza injili kupitia uimbaji.
Muimbaji huyu anaweza kuwa mgeni masikioni mwa wengi, lakini ni miongoni mwa waimbaji wachache ambao wamekuwa wakisikiliza sauti ya Roho Mtakatifu juu ya nini anatakiwa afanye katika kumtumikia Mola wake kwa njia hiyo.
Mpakwa mafuta huyo wa Mungu tayari amefanikiwa kurekodi albamu yake yenye vibao vinane aliyoipa jina la ‘Mbinguni si lelemama’ ikiwa katika mfumo wa audio na video ambayo ina nyimbo zilizojaa utukufu wa Mungu na hazichoshi kuzisikiliza na pia kuziangalia.
Albamu hiyo anatarajia kuizindua Oktoba 24 katika ukumbi wa chini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Azania Front jijini Dar es Salaam, na shughuli hiyo itasindikizwa na wakali wa muziki wa injili nchini kama Christina Shusho, David Robert, Trenet Band, The Voice na Upendo Safari.
Alizitaja nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo kuwa ni Toa sadaka, Dunia imeharibika, Ibilisi mjanja, Mbinguni si lelemama, Bariki, Kizazi cha ukaidi, Maisha ya mwanadamu na Ndoa.
Rose alimaliza kwa kusema kuwa atamtumikia Mungu wake mpaka mwisho wa maisha yake kwa maana anatambua kuwa amepewa kipawa cha kutunga na kuimba nyimbo za injili ili zifanyike msaada kwa watu wengi wanaoshi maisha yasiyompendeza Mola pamoja na wanaoishi maisha ya shida.

Wasiliana naye kwa +255 713 864539/ +255 755 333332























Newer Posts Older Posts