LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

12/25/09

Kilaini awaanga wakazi wa Dar


Aliyekuwa askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, ambaye amehamishiwa Jimbo la Bukoba, amewaaga rasmi waumini wa Jimbo hilo na kudai kuwa atawakumbuka kwa upendo wao waliokuwa nao juu yake(Picha kwa hisani ya Habari Leo).

Akiwaaga waumini hao kupitia ibada ya Misa ya sikukuu ya Krismasi iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Kilaini alisema kuwa, mbali na kuwakumbuka, pia amewataka Watanzania wote kuliombea taifa lao ili uchaguzi mkuu wa mwakani uwe wa amani na utulivu.

Kilaini alisema kuwa, Watanzania wana wajibu wa kuwaombea viongozi wa vyama vya siasa ili washiriki katika uchaguzi huo bila kuvunja amani.

“Kama tunavyojua, mwaka kesho tuna uchaguzi, katika nchi yoyote uchaguzi ni kitu cha muhimu, tumwombe Mwenyezi Mungu uchaguzi uwe wa amani , tuwaombee wenyeviti wa vyama vya siasa ili watupitishe mwaka ujao salama na tupate viongozi watakaotufikisha miaka mitano ijayo salama,” alisema Kilaini.

Katika hatua nyingine Kilaini alitumia nafasi hiyo kuwasamehe watu wote mabaya waliyomfanyia wakati akiwa Askofu Msaidizi wa jimbo kwani ni hali ya kibinadamu na hivyo hana budi kuyasahau na pia waumini wa kanisa hilo walitumia misa hiyo kumuaga rasmi.

Mashambulizi yatokea nchini Iraq.

BAGHDAD
Watu 18 wameuawa, nchini Iraq, katika mashambulizi mapya licha ya usalama kuimarishwa katika sikukuu ya Krismamasi, pamoja na sherehe za Ashura zinazofanyika katika jamii ya Washia nchini humo. Watu sita waliuawa, kufuatia mripuko wa bomu lililokuwa limetegwa barabarani, lilipolipuka wakati msafara wa Washia walipokuwa wanapita huko Sadr, Baghdad. Watatu kati ya waliouawa wanasemekana ni waalimu waliokuwa wakikusanya data, za taasisi ya kuhesabu watu nchini Iraq. Zaidi ya polisi elfu 46 na wanajeshi wamepelekwa katika miji ya Karbala na Najaf, kushika doria, leo katika sherehe za siku ya Ashura

Kumbukumbu ya Tsunami miaka 5

ACEH, INDEONESIA
Raia wa jimbo la Aceh nchini Indonesia wametenga leo kuwa siku ya maombi, kuwakumbuka wahanga wa janga la Tsunami lililokumba bara Asia miaka mitano iliyopita. Kiasi cha watu elfu 200 waliuawa, na mabilioni ya mali kuteketezwa. Eneo la Aceh, huko Indonesia ndilo lililoathirika zaidi, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha Tsunami Desemba tarehe 26 mwaka wa 2004. India, Sri Lanka na Thailand ambazo pia ziliathirika, zimetenga leo kuwa siku ya maombi kama kumbukumbu ya janga hilo. Hapa nchini Ujerumani, maombi yatafanyika katika kanisa moja mjini Dusseldorf.

Shambulizi katika ndege ya kuelekea Marekani.

WASHINGTON
Rais Barack Obama ameagiza kuchukuliwa hatua za ziada za kiusalama katika usafiri wa ndege, baada ya mtu mmoja kujaribu kulipua ndege moja ya shirika la Marekani iliyokuwa inaelekea Detroit kutoka mjini Amsterdam. Mtu huyo ambaye anasemekana ni raia wa Nigeria, alikuwa abiria ndani ya ndege hiyo, yenye chapa AIRBUS 330 iliyokuwa imewabeba abiria 278, alizidiwa nguvu na wenzake alipojaribu kuwasha fataki wakati ndege hiyo ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege huko Detroit. Vyombo vya habari vya Marekani, vinaripoti kuwa mtu huyo amewaambia maafisa wa usalama kuwa alitoa fataki hizo na maagizo ya kuilipua ndege hiyo kutoka nchini Yemen. Rais Obama ambaye yuko likizoni huko Haiwaii anasemekana anafuatilia matukio, lakini hajabadili ratiba yake. Taarifa kutoka shirika la ndege la Northwest zinasema raia huyo wa Nigeria amekamatwa na abiria wengine walihojiwa kufuatia tukio hilo.

Maaskofu wa Ireland wajiuzulu kutokana na kashfa ya ulawiti.

DUBLIN
Maaskofu wengine wawili wa kanisa Katoliki nchini Ireland wamesema kwamba watajiuzulu kufuatia kufichuka kwa kashfa kwamba dayosisi kuu ya Dublin imekuwa ikificha vitendo vya kulawiti vilivyokuwa vinafanywa na makasisi dhidi ya watoto. Maaskofu wasaidizi, Eamonn Walsh na Ray Field, wamesema wanatumai hatua yao ya kujiuzulu inaweza kusaidia kuleta amani na maridhiano ya Yesu Kristo kwa wahanga na watoto walionusirika na vitendo hivyo vya ulawiti. Ripoti iliyotayarishwa na serikali ya Ireland, imefichukua kuwa kanisa Katoliki limekuwa likificha vitendo hivyo vya kuwalawiti watoto wadogo kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 2004 pamoja na kuwalinda makasisi 170 waliokuwa wakiendesha vitendo hivyo wasichukuliwe hatua za kisheria.Tangu kutolewa kwa ripoti hiyo takriban mwezi mmoja uliopita, maaskofu wengine wawili, tayari wamejiuzulu.

Hotuba ya Krismasi ya Papa

VATICAN
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Benedikti wa 16, ametoa wito kwa ulimwengu kuachana na vurugu na machafuko katika hotuba yake ya sikukuu ya Krismasi. Papa Benedict alitoa hotuba hiyo saa chache baada ya kuangushwa chini na mwanamke aliyeruka vizuizi vya usalama  katika misa ya mkesha wa Krismasi. Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Susana Maiolo, ametajwa kuwa na historia ya matatizo ya akili  na aliwahi pia kujaribu kumkaribia kiongozi huyo wa kidini mwaka uliopita lakini akazuiwa. Kiongozi huyo wa kidini, hata hivyo, alinyanyuka mara moja baada ya tukio hilo la kuanguka na kuonekana kuwa katika hali nzuri ya kiafya wakati akihutubia umati wa wafuasi waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa kanisa la St Peters.
 

Wimbo bora wa injili mwaka 2009

Nyimbo za injili zipatazo 30, zimeingizwa katika kinyang’anyiro za kutafuta wimbo bora wa mwaka 2009. Shindano hilo linaendeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1). Watazamaji wa TBC1 wanatakiwa kuchagua wimbo mmoja kati ya hizo, kisha kupiga kura kwa kuandika jina la wimbo na namba ya mhusika kwenda 15788. Kipindi cha shindano hilo kinarushwa majira ya saa 3:15 usiku kuanzia Desemba 25 mpaka 27. Mshindi wa atapatikana Desemba 27 mwaka huu.
Waimbaji waliokatika shindano hilo na namba zao za ushiriki kwenye mabano ni;
Neema Mwaipopo – Usijinyime raha (101)
Jenn Joel Makila -  Mungu hana upendeleo (102)
Jennifer Mgendi – Jaribu langu (103)
AIC Chang’ombe – Mpinga Kristo (104)
Medrick Sanga  -  Mapambano  (105)
Mwanga town Choir – Mwambie Yesu (106)
Ency Mwalukasa – Usilie (107)
AIC Mwadui – Haki (108)
Apostle Kyande – Selemala (109)
AIC Makongo – Kekundu (110)
Rose Mahenge – Mbinguni ndiko nyumbani (111)
Jenn Miso – Omoyo (112)
Solomon Mukubwa – Mfalme (113)
Upendo group – Jina lako li hai (114)
Rose Mhando – Jipange sawasawa (115)
Upendo group – Yesu yeye yule (116)
Flora Mbasha – Furaha yako (117)
Rose Mhando – Si salama (118)
Joseph Nyuki – Tegemeo langu (119)
Mt. Cecilia Arusha – Nimevunja mkataba na shetani (120)
Upendo group – Mungu wetu ni mwema (121)
Geraldine Odwaa – Upendo wa ajabu (122)
Upendo group – Amen haleluya (123)
Abiud Misholi – Tenda miujiza (124)
Christina Shusho – Unikumbuke (125)
Ado November – Amenitoa mbali (126)
Upendo Nkone – Haleluya usifiwe (127)
Mhubiri kwaya – Nani kama wewe (128)
Rose Mhando – Nibebe (129)
Bahati Bukuku – Waraka (130)
Piga kura sasa kwa wimbo unaopenda uwe Bora mwaka 2009  kwa kuandika namba ya mwenye wimbo na kisha tuma kwenda 15788.








Newer Posts Older Posts