LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

12/27/09

KKKT lakemea mavazi ya kubana



KANISA la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati, limekemea tabia iliyojengeka na  baadhi ya wanawake ya kuvaa mavazi ya kubana mwili ambayo yamekuwa chukizo kwa wanaume.(Pichani ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT nchini Dk Alex Malasusa)

Tamko hilo kali limetolewa na wanawake wapatao 234 wa kanisa hilo kwenye mkutano wao uliofanyika Usharika wa Manyoni, Jimbo la Kusini, mkoani Singida.

“Kanisa limesikitishwa juu ya mavazi yavaliwayo na wanawake kama vile suruali, mavazi ya mipasuo ya aibu na nguo za kubana, mavazi ya harusi yasiyoonyesha heshima na kwamba kwa kufuata msingi mavazi ya aina hiyo hayatakiwi kuvaliwa kanisani na mwanamke au mwanaume,” lilifafanua tamko la wanawake hao.

Kwa mujibu wa tamko hilo, mwanamke ametakiwa asivae mavazi yamfaayo mwanaume wala mwanaume naye asivae mavazi ya mwanamke kwa maana kwamba kila afanyaye hayo humchukiza Mungu.

Katika kilele cha sikukuu hiyo ya wanawake, pia kulifanyika harambee ya kuchangia matengenezo ya gari pamoja na ununuzi wa kompyuta, ambapo jumla ya sh 2,177,810 zilikusanywa na kwamba kati ya hizo sh 1,177,000 ni ahadi na fedha taslimu ni sh 404,810.

Wakati huo huo, usharika wa Tabata Kuu umemuomba mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa kutoa tamko la wazi kupinga uamuzi wa kanisa hilo nchini Marekani na Ulaya kuruhusu ndoa za mashoga.

Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Mchungaji Erasto Ailla wa usharika huo wa KKKT alipohubiri kwenye maadhimisho ya siku kuu ya Krismasi ya kuadhimisha miaka 2009 ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Mchungaji huyo pia aliongoza sala maalum ya kupinga vitendo hivyo.

Mchungaji Ailla, akionyesha kusikitishwa na vitendo hivyo kwa makanisa ya nchi za Magharibi, alisema taarifa za kanisa hilo nchini Marekani na barani Ulaya kubariki ndoa za mashoga na wengine kuongoza ni kumkejeli Mungu ambaye ametamka wazi kwamba waovu wa aina hiyo hawatauona ufalme wa Mungu.

Alimuomba Dk Malasusa tamko la kupinga uamuzi huo kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla na kwamba yeye anaamini kwamba kanisa hilo barani Afrika halitakubali kuruhusu mashoga kuoana kwani ni kinyume na maagizo ya Mungu.

"Kwa kuanzia, nawaomba waumini wote usharika huu tuwe wa kwanza kupinga na sasa tusimame, tufumbe macho na kuomba sala maalum ya kukataa ushoga ndani ya kanisa na kukiri wazi kwamba mashoga... wanamchukiza Mungu kama wale wa Sodoma na Gomola," alisisitiza na kuwaongoza waumini kwa sala maalumu ambayo pamoja na mambo mengine pia ilikuwa inakataa ushoga kwa mbinu zote.

Kanisa la Kilutheri nchini Marekani liliruhusu ndoa za mashoga baada ya uamuzi huo kupitishwa kwenye mkutano wake mkuu, na kuwa kanisa la pili baada ya Anglican ambalo pia ni la Marekani.




NIBEBE WIMBO BORA 2009

Wimbo wa Nibebe wa malikia wa muziki wa Injili nchini Rose Muhando umechaguliwa kuwa wimbo bora mwaka 2009 baada ya kujikusanyia pointi nyingi kutoka kwa mashabiki wa miondoko hiyo hiyo kupitia luninga ya taifa, TBC1. Wimbo huo uliokuwa unashindanishwa na nyimbo nyingine 29 ulionekana bora baada ya kuingia tatu bora pamoja na
Waraka wa Hamani wa Bahati Bukuku na Mfalme wa amani wa Solomoni Mukubwa. Wimbo wa Mfalme wa amani ulishika namba mbili huku Waraka wa Hamani ukishika namba tatu.

Maandamano Tehran

Tehran.
Mpwa wa kiongozi wa upinzani nchini Iran Mir Hossein Mousavi ameuwawa wakati wa maandamano mjini Tehran jana Jumapili. Seyed Ali Mousavi alipigwa risasi kifuani kwa mujibu wa ripoti katika tovuti za upande wa upinzani na maafisa wamekiri kuwa watu kadha wameuwawa. Naibu mkuu wa polisi Ahmad Reza radan amekiambia kituo cha televisheni ya taifa kuwa zaidi ya watu 300 wamekamatwa. Hali ya wasi wasi imeongezeka sana nchini Iran kufuatia kifo wiki moja iliyopita cha kiongozi wa kidini mpinzani ayatollah mkuu Ali Montazeri akiwa na umri wa miaka 87.

Tukio jingine katika ndege iendayo Detroit.

Detroit, Marekani.
Kumekuwa na tukio jingine la kutisha katika ndege ya shirika la ndege la Northwest iliyokuwa inakwenda mjini Detroit, kiasi siku moja baada ya abiria kujaribu kulipua mlipuko katika ndege inayokwenda katika njia hiyo. Wafanyakazi wa ndege walihitaji msaada wa dharura baada ya abiria mmoja , ambaye alitumia zaidi ya saa nzima katika choo cha ndege hiyo, baada ya kuanza kutoa matusi wakati akihojiwa. Baada ya kutua, ndege ilipelekwa katika sehemu ya kando ya uwanja wa ndege wa Detroit, ambapo polisi waliondoa mizogo na kuichunguza iwapo ilikuwa na vitu vinavyotia shaka. Maafisa baadaye walimwachia mtu huyo. Kutokana na matukio hayo, mkuu wa usalama wa ndani Janet Napolitano aliwahakikishia wasafiri kuhusu hali kuwa tulivu.
Maafisa duniani wameongeza hatua za usalama katika viwanja mbali mbali vya ndege kutokana na tukio hilo la hivi karibuni.

Maporomoko ya barafu yaua 7

Roma.
Watu saba wameuwawa na maporomoko ya barafu kaskazini mwa Italia mwishoni mwa juma hili. Watalii wawili raia wa Italia siku ya Jumamosi walizikwa na maporomoko hayo ya barafu katika milima ya Alps nchini Italia, kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo na watu wanne wafanyakazi wa kikosi cha uokozi wameuwawa katika maporomoko hayo wakati wakiwatafuta wahanga. Watalii hao wawili walipotea siku ya Jumamosi mchana wakati wakipanda milima katika jimbo la Trentino Alto Adige. Katika tukio jingine tofauti, maafisa wa kikosi cha uokozi pamoja na polisi wamesema jana Jumapili kuwa kijana mmoja wa kiume kutoka Ujerumani aliuwawa papo hapo baada ya kufunikwa na barafu wakati akifanya mchezo wa kuteleza katika barafu pamoja na kaka yake na rafiki katika milima ya Alps nchini Italia.

Bomu katika jengo la bima Ugiriki.

Athens.
Polisi wa mjini Athens wamethibitisha kuwa bomu lililipuka jana jioni katika ofisi za moja kati ya kampuni kubwa kabisa za bima nchini Ugiriki, inayomilikiwa n a benki ya taifa ya Ugiriki Ethniki Asfalistiki. Watu walioshuhudia wamesema kuwa bomu liliharibu jengo na magari lakini hakuna mtu aliyejeruhiwa. Maafisa wamelaumu makundi yanayofuata nadharia za mrengo wa shoto kwa shambulio hilo dhidi ya polisi katika miezi ya hivi karibuni kuwa wanahusika na mlipuko huo. Polisi wamesema kuwa walipata simu iliyotoa tahadhari kutoka gazeti moja dakika 15 kabla ya mlipuko huo lakini hakuna kundi ambalo limedai kuhusika.

Wauzbekistan wapiga kura.

Tashkent. Wapiga  kura  katika  taifa  la  Asia  ya  kati  la  Uzbekistan wamemiminika   katika  vituo  vya  kupigia  kura  jana Jumapili  kwa  ajili  ya  uchaguzi  wa  bunge. Kiasi  cha zaidi  ya  wapiga  kura  milioni  17  wamejiandikisha  kupiga kura  kulichagua  bunge  litakalokuwa  na  viti  150  la baraza  la  wawakilishi. Tangu  kupigwa  marufuku  kwa vyama  vya  upinzani   kushiriki  katika  siasa, wapiga  kura walikuwa  wana  nafasi  tu  ya   kumchagua  mgombea kutoka  vyama  vinne  vinavyomuunga  mkono  rais  Islam Karimov  ambaye  ameitawala  nchi  hiyo  kwa  muda  wa miongo miwili  iliyopita. Wachunguzi  wa  uchaguzi  huo kutoka   shirika  la  usalama  na  ushirikiano  katika  bara  la Ulaya   wamesema   kuwa  uchaguzi  huo  katika  jimbo hilo  la  zamani  la  iliyokuwa  Urusi  ya  zamani haukufanyika   kwa  uhuru  na  haki. Licha   ya  hali  hiyo, uchaguzi  huo  haukukumbana  na  ukosoaji  mkubwa kutoka  mataifa  ya  magharibi  kutokana  na  jukumu  la Uzbekistan  katika  juhudi  za   kuwadhibiti  Wataliban katika  nchi  jirani  ya  Afghanistan.

Newer Posts Older Posts