LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013
JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA
ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.
IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404
REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI
12/28/09
Nabii Joedavie
Gospel Music Center 0
Westerwelle asema Ujerumani itasusia mkutano wa Afghanistan.
Gospel Music Center 0
Berlin.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle, amesema kuwa atasusia mkutano wa kimataifa kuhusu Afghanistan, iwapo mkutano huo hautaangalia juhudi za ujenzi wa kiraia. Westerwelle ameliambia gazeti la kila wiki nchini Ujerumani la Stern kuwa iwapo mkutano huo utakaofanyika mwezi Januari mjini London utakuwa tu kuhusu kuchangia majeshi zaidi kwa ajili ya Afghanistan, Ujerumani haitashiriki. Hata hivyo, Westerwelle amerudia maelezo rasmi ya serikali kuwa itaangalia juu ya kuchangia waalimu zaidi kwa ajili ya jeshi la polisi . Kuongeza idadi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan litakuwa si jambo linaloungwa mkono nchini humo.
EU yaitaka Israel kuangalia upya mradi wa nyumba.
Gospel Music Center 0
Brussels.
Umoja wa Ulaya na Marekani zimepinga mipango ya Israel ya kujenga nyumba 700 katika eneo la Jerusalem ya mashariki. Katika taarifa, umoja wa Ulaya umeutaja ujenzi wa nyumba hizo kuwa ni kinyume na sheria chini ya sheria za kimataifa, wakati msemaji wa ikulu ya Marekani Robert Gibbs ameieleza mipango hiyo kuwa ni kitisho kwa amani ya eneo hilo. Wapalestina wanataka kulifanya eneo la Jerusalem ya mashariki kuwa mji wao mkuu wa taifa wanaloahidiwa na wanaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa pamoja na umoja wa Ulaya. Israel wakati huo huo imesema mji wote wa Jerusalem ni mali ya taifa la Kiyahudi na imekataa miito ya kusitisha ujenzi wa makaazi katika eneo la mashariki inalolikalia.
Afghanistan kuchunguza shambulio la NATO.
Gospel Music Center 0
Kabul.
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameshutumu vikali shambulio la anga lililofanywa na majeshi ya NATO mashariki mwa nchi hiyo, ambalo linaripotiwa kuwa limesababisha vifo vya watu 10. Kwa mujibu wa maafisa katika ofisi ya rais, wanane kati ya wahanga walikuwa ni watoto wa shule. Msemaji wa bunge amesema kuwa tume itachunguza shambulio hilo. NATO inaripotiwa kuwa imekubali kushiriki katika uchunguzi huo.
30 wauwawa na bomu la kujitoa muhanga.
Gospel Music Center 0
Karachi.
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameshambulia mlolongo wa Waislamu wa madhehebu ya Kishia katika mji mkubwa nchini Pakistan wa Karachi na kuuwa watu 30. Kiasi watu 60 pia wamejeruhiwa. Watu walioshuhudia wamesema kuwa watu wawili ama watatu waliingia katika kundi la watu wapatao 50,000 waliokuwa wakishiriki katika maandamano ya Ashura na kulipua bomu lililokuwa limefungiwa mwilini. Mlipuko huo baadaye ulizusha ghasia mjini Karachi, mji wa kibiashara, ambapo watu wenye hasira walifanya ghasia. Lilikuwa ni shambulio la tatu dhidi ya sherehe hizo za Ashura nchini Pakistan mwaka huu. Siku ya Jumapili mshambuliaji wa kujitoa muhanga alishambulia msikiti wa Washia katika eneo linalomilikiwa na Pakistan la Kashmir na kuuwa watu saba. Bomu liliwajeruhi watu 17 mjini Karachi siku hiyo hiyo. Washia ni kiasi cha asilimia 20 ya jumla ya watu nchini Pakistan ambapo Wasunni ni wengi zaidi miongoni mwa watu milioni 167 nchini humo.
Muingereza kunyongwa China
Gospel Music Center 0
Beijing.
Muda unakaribia kufikia mwisho kwa mtu mmoja raia wa Uingereza anayekabiliwa na hukumu ya kunyongwa nchini China. Akmal Shaikh mwenye umri wa miaka 53 alikamatwa Septemba 2007 mjini Urumqi magharibi mwa China akiwa na kilo nne za madawa ya kulevywa katika mzigo wake. Alihukumiwa kifo mwaka jana , Shaikh ameshindwa katika rufaa yake ya mwisho katika mahakama kuu mwezi huu. Waungaji wake mkono wanadai kuwa baba huyo mwenye watoto watatu ni mgonjwa wa akili, utetezi ambao hauna uzito wa kutosha kwa mujibu wa sheria za China. Hukumu ya kifo inatolewa kwa makosa kadha nchini humo na hutekelezwa mara zote. Mwaka jana kiasi cha zaidi ya watu 1,700 wamenyongwa.
Al Qaeda yadai kuhusika na jaribio lililoshindwa.
Gospel Music Center 0
Washington.
Tawi la kimkoa la kundi la kigaidi la al-Qaeda, limetoa taarifa katika tovuti yake likidai kuhusika katika jaribio lililoshinda dhidi ya ndege ya abiria ya Marekani Desemba 25. Al Qaeda katika ghuba ya Arabia ama kama linavyojulikana kama AQAP, limesema kuwa mtuhumiwa, Umar Farouk Abdulmutallab alijaribu kuilipua ndege ya shirika la ndege la Northwest iliyokuwa imebeba watu 278 kulipiza kisasi kwa mashambulio ya majeshi ya Marekani dhidi ya kundi hilo nchini Yemen. Taarifa hiyo iliyotolewa katika tovuti kadha za Kiislamu imesema kuwa kundi hilo lilimpatia mtuhumiwa huyo wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 23 kifaa kilichotengenezwa kwa ufundi wa hali ya juu, lakini kilishindwa kulipuka kutokana na matatizo ya kiufundi na kuwaonya Wamarekani kuwa watashambuliwa zaidi.
Westerwelle asema Ujerumani itasusia mkutano wa Afghanistan.
Gospel Music Center 0
Berlin.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle, amesema kuwa atasusia mkutano wa kimataifa kuhusu Afghanistan, iwapo mkutano huo hautaangalia juhudi za ujenzi wa kiraia. Westerwelle ameliambia gazeti la kila wiki nchini Ujerumani la Stern kuwa iwapo mkutano huo utakaofanyika mwezi Januari mjini London utakuwa tu kuhusu kuchangia majeshi zaidi kwa ajili ya Afghanistan, Ujerumani haitashiriki. Hata hivyo, Westerwelle amerudia maelezo rasmi ya serikali kuwa itaangalia juu ya kuchangia waalimu zaidi kwa ajili ya jeshi la polisi . Kuongeza idadi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan litakuwa si jambo linaloungwa mkono nchini humo.
WALIOTEMBELEA BLOG HII
TUMA HABARI NA MATUKIO
KAMA UNA HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI POPOTE DUNIANI TUMA KWA EMAIL HII. productiongmk@gmail.com. NAMI NITAZIWEKA KWENYE BLOG HII BILA GHARAMA YOYOTE. NAKARIBISHA HABARI ZA MATAMASHA YA INJILI, MIKUTANO, RATIBA ZA MAKANISA, SEMINA, HARUSI NA MAMBO MBALIMBALI KWA AJILI YA KUWAJULISHA WANAULIMWENGU. WASILIANA NAMI KWA NAMBA ZIFUATAZO.
+255 712 001 880,
+255 755 240 136.
HABARI MUHIMU
-
Wapendwa katika Yesu Kristo leo nimefanikiwa tena kukutana na muimbaji wa muziki wa Injili nchini anayekwenda kwa jina la Upendo Nkone ambay...
-
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Efatha Ministries anayetikisa jijini la Dar es salaam na amejikusanyi waumini wengi kiasi kwamba huduma...
-
Aliyekuwa muimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini Fanuel Sedekia alizikwa Januari 10 mkoani Arusha baada ya kufariki dunia usikua wa kua...
-
Nivigumu kuamini lakini ukweli ni huo kwamba, mtoto mmoja wa miaka 10, Anna Msingwa aliyezaliwa akiwa kipofu ameanza kuona huku Iringa, kwa...
-
Hakuna asiyeelewa kwamba mkoa wa Mbeya ni mkoa ambao umekuwa ukitoa waimbaji mahiri wa muziki wa injili wenye tungo ambazo msikilizaji wa ny...
-
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Kenya , Solomon Mukubwa leo (Jumamosi) anafunga pingu za maisha na Bi. Betyy katika kanisa moja la Kir...
-
Ndoa ni nini? Ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke unaokubalika kiutamaduni na kidini ambao unatarajiwa kudumu, kuwapa haki sawa za kiji...
-
Kwa wapenzi wa muziki wa injili nchini, jina la Shusho si jina geni masikioni mwao kutokana na umahiri wa kutumia kipawa cha uimbaji cha mwa...
-
Baraka akiwa na mwanaye Deliver akiwa nyumbani kwake mkoani Mbeya Deliver Baraka akiwa katika pozi safi Deliver Baraka ...
-
Baada ya kukaa kimpya kwa muda mrefu bila kutoa albam mpya na kupelekea baadhi ya wadau wa muziki wa Injili kuhoji uwepo wa Bony Mwaitege ka...
Categories
- George Kayala (23)
- George Kayala. (6)
- Kabula John George (1)


