LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.

IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

12/29/09

Tamasha la Injili kufanyika CCM Kirumba

TAMASHA la muziki wa Injili lililofanyika sikukuu ya Krismasi ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam limehamishiwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na litafanyika siku ya Mwaka mpya.

Waimbaji wote walioshiriki tamasha la Dar ndiyo watamkanyaga shetani siku hiyo wakiongozwa na mshindi wa wimbo bora wa Injili mwaka 2009 kupitia televisheni ya Taifa, TBC1, Rose Muhando.

Wengine ni Solomoni Mukubwa, Bahati Bukuku, Jennifer Mgendi, Geraldine Oduor, Upendo Nkone, Enock Jonas, Flora Mbasha na Kundi la Muziki wa Injili la Upendo la Kijitonyama, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa baada ya kumaliza tamasha hilo Mwanza wataelekea Shinyanga.

"Tamasha lilikuwa la mafanikio makubwa, na nashukuru tumevuka malengo ya kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia walemavu kununua baiskeli, sasa tunataka kufanya hivyo kwa jiji la Mwanza na vitongoji vyake," alisema.

Misiri kuruhusu waandamanaji 100 kuingia Gaza.

Cairo.
Viongozi   wa  wanaharakati   ambao  wamekwama  mjini Cairo  wamekubali  pendekezo  la  Misiri  jana  Jumanne kuwaruhusu  wanaharakati  100  tu   miongoni  mwa wanaharakati  1,300  kuingia  katika  eneo  la  Gaza lililozingirwa  na   majeshi  ya  Israel  baada  ya wanaharakati  hao   kufanya  maandamano  pamoja  na mgomo  mkubwa  wa  kula.
Uamuzi  huo  umewagawa  wanaharakati  hao  kutoka karibu  nchi  40  ambao  wamekwenda  mjini  Cairo wakipanga   kuingia  katika  eneo  hilo  la  Wapalestina, ambalo  linapakana  na  Misiri  katika   eneo  la  mpakani  la Rafah.
Baadhi  ya  watayarishaji  wamesema   kuwa   pendekezo la  Misiri  ni  ushindi  baada   ya  hapo  kabla   kukataa kuwaruhusu  wanaharakati  hao  kuingia  ukanda  wa  Gaza kwa  ajili  ya  maandamano  yanayoitwa  ya  uhuru  , ambayo  yanapangwa  kufanyika  kesho  Alhamis.

Maharamia wa Kisomali wakamata meli mbili zaidi.

London.
Maharamia  wa  Kisomali  wameteka  nyara   meli  mbili zaidi  za  mizigo  katika  ghuba  ya  Aden  katika  bahari  ya Hindi   siku  ya  Jumatatu. Kukamatwa  huko   kwa  meli ya  Uingereza  ya  St. James  Park  , na  meli  ya  mizigo ya  Panama , Navios Apollon , kuna  maana  wahalifu  hao wa  Kisomali  hivi  sasa  wanashikilia  kiasi  ya  meli  11  na karibu  mabaharia  250. Miongoni  mwa  wale wanaoshikiliwa   ni  pamoja  na  raia  wawili  wa  Uingereza mke  na  mume  waliokamatwa  mwezi  wa  Oktoba  wakati wakisafiri  na  meli  yao  kwenda  Tanzania. Maharamia wamepata  mamilioni  ya  dola  kutokana  na  kuteka  nyara meli  na  kulipwa  fedha  nyingi  katika  ghuba  ya  Aden, ambayo  inaunganisha  bara  la  Ulaya  na  Asia. Majeshi ya majini  ya  nchi  za  kigeni   pamoja  na   yale  ya  umoja wa  Ulaya   yameweka  meli  zao  za  kivita  katika  eneo hilo   ili   kulinda  meli  za  kibiashara  lakini  eneo  hilo kubwa   ambalo  linahitaji  kufanyiwa  doria  linaendelea kuwa  hatari  kwa  meli  nyingi.

Serikali ya Ujerumani yaishutumu Iran .

Berlin.
Serikali ya Ujerumani imesema kuwa ina wasi wasi mkubwa kuhusu matukio ya hivi karibuni nchini Iran, na imeshutumu vikali vitendo vya majeshi ya usalama ya Iran . Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Werner Hoyer pia ameitolea wito Iran kuzuwia kuongezeka zaidi kwa hali ya wasi wasi. Katika muda wa siku za hivi karibuni kumekuwa na maandamano makubwa dhidi ya utawala wa Iran, wakati watu karibu wanane wameuwawa katika maandamano siku ya Jumapili. Miongoni mwa wale waliouwawa ni pamoja na mpwa wa kiongozi wa upinzani Mir Hossein Muossavi. Siku ya Jumanne rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad amelaumu kile alichosema ni Marekani na Wayahudi kwa hali hiyo ya kukosa utulivu.

Viwanja vya ndege vyaongeza ulinzi.

Washington.
Katika  mkutano  na  waandishi  habari   uliofanyika  Hawaii, rais  wa  Marekani  Barack  Obama  amekiri  kuwa  usalama wa  ndani  nchini  humo   pamoja  na  ulinzi  kupitia  taarifa za  siri  umepata  pigo  kabla   ya  kutokea  jaribio lililoshindwa  la  kigaidi  wakati  wa  sikukuu  ya  Chrismass.
Wakati  huo  huo , viwanja  vya  ndege  nchini  Ujerumani vimeongeza   usalama, na  kuanzisha  upekuzi  mkali  wa wasafiri  na  mizigo  kufuatia  hatua  kama  hizo zilizochukuliwa  na   maafisa  wa  viwanja  vya  ndege barani  Ulaya  na  Marekani. Maafisa  wamewaomba wasafiri  kuwa  na  uvumilivu   kutokana  na  hatua  hizo mpya. Kundi  la  kimkoa  la  kigaidi   la  al Qaeda  limedai kuhusika  na  shambulio  hilo  lililoshindwa  la  kigaidi, likisema  limempatia  kijana  huyo  mwenye  umri  wa miaka  23  raia  wa  Nigeria  kifaa  hicho  cha  mlipuko. Matatizo  ya  kiufundi  yalizuwia   kifaa  hicho  kulipuka ndani  ya  ndege  ya  shirika  la  ndege  la  Northwest, ambayo  ilikuwa  imewachukua  abiria  278  na  hakuna mtu  mwingine  mbali  ya  kijana  huyo  aliyejeruhiwa.

Watu 33 wameuawa katika mapambano nchini Nigeria

Abuja:
Kumetokea mapigano makali kati ya vikosi vya usalama vya Nigeria na waumini wa dini ya kiislamu wenye imani kali ambayo yamesababisha vifo vya watu 38 katika jimbo la Bauchi.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini humo, Atiku Kafur, ameliambia gazeti moja la nchini humo kwamba, mapigano hayo yalianza baada ya kiongozi wa dhehebu la Kalo Kato, Malam Badamasi, kukasirishwa na tetesi kwamba mmoja wa wafuasi wake alikuwa akifanya vitendo vya kishirikina dhidi yake.
Katika kujibu tetesi hizo, kiongozi huyo alianzisha mahubiri ya hadhara ambayo yaliwaudhi baadhi ya watu na hivyo kuzusha machafuko.
Wakati huo huo, polisi ya nchi hiyo inatarajia kuwa na mkutano na vyombo vya habari juu ya uchunguzi wa kesi ya Umar Farouk Abdul Muttallib, ambaye alifanya jaribio la kuiripua ndege ya abiria iliyokuwa inaelekea Detroit, Marekani, wakati wa sikukuu ya Krismas.

Ujerumani yaimarisha usalama katika viwanja vya ndege

Berlin:
Ujerumani imeimarisha zaidi usalama katika viwanja vya ndege, ambapo maafisa wameongeza ukaguzi wa abiria na mizigo yao.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani amesema maafisa wa usalama wana dhamana kubwa kufuatia taarifa ya kundi la kigaidi la Al Qaeda kuhusika katika njama zilizoshindwa za kuripua ndege ya abiria nchini Marekani wakati wa sikukuu ya Krismasi.
Katika taarifa hiyo iliyochapishwa katika tovuti za kiislamu, kundi hilo limesema kuwa lilimpa kijana wa Kinigeria, Umar Farouk Abdul muttallib, mwenye miaka 23, kifaa cha uripuaji chenye teknolojia ya hali ya juu, ili kuiripua ndege hiyo iliyokuwa na abiria 278 ndani yake.

Pakistan yatoa wito wa utulivu baada ya machafuko ya usiku

Karachi:
Maafisa nchini Pakistan wametoa wito wa utulivu kwa wananchi wake baada ya machafuko ya jana usiku katika jiji la Karachi.
Maandamano yaliyosambaa sehemu kubwa yalizuka baada ya bomu la kujitoa mhanga kuua watu 40 katika maandamano ya Waislam wa madhehebu ya Shia hapo jana.
Waombolezaji wenye hasira kali walichoma moto soko na mamia ya maduka katikati ya jiji hilo.
Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na bomu hilo la kujitolea mhanga, ambalo limekuja wakati wa hatua kali za kiusalama zinazochukuliwa dhidi ya wanamgambo wa Taliban.

Netanyahu akutana na Rais Hosni Mubarak wa Misri

Cairo:
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu, amekutana na Rais Hosni Mubarak wa Misri mjini Cairo hii leo juu ya juhudi za Marekani za kutaka kuendelea kwa mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati yaliyokwama karibu mwaka mmoja sasa.
Hata hivyo, hakuna kiongozi yoyote kati yao aliyezungumza na vyombo vya habari baada mkutano huo, lakini ofisi ya Netanyahu imesema mazungumzo yalikuwa mazito na ya kirafiki.
Ofisi hiyo ilisema viongozi hao walijadiliana namna ya kuanzisha mchakato wa amani na Wapalestina, na juhudi za kumrudisha Gilad Shalit, mwanajeshi wa Israel aliyetekwa na wanamgambo wa Gaza miaka mitatu na nusu iliyopita.
Marekani imekuwa ikiandika barua kwa Israel na Wapelestina ikishadidia kwamba itakuwa mdhamini na kuchukua jukumu la kuanzishwa mazungumzo ambayo mwisho wake yatapelekea kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.

Iran yakataa kuziachia maiti za watu watano waliouawa

Tehran:
Iran imekataa kuiachia miili ya watu watano kati ya kiasi ya waandamanaji wanane waliouawa na vikosi vya usalama, wakati wa maandamano ya kuipinga serikali mjini Tehran Jumapili iliyopita.
Inaaminika kuwa miongoni mwa miili hiyo ni pamoja na waziri wa zamani wa mambo ya nje na mpwa wa kiongozi wa upinzani, Mir Houssen Moussavi.
Serikali imesema inataka kuzifanyia uchunguzi maiti hizo, lakini upinzani unaaamini kwamba hilo ni jaribio la kuwazuia wanaharakati kutumia mazishi ya watu hao kama msingi wa maandamano zaidi.
Wakati huo huo Iran imemuita balozi wa Uingereza mjini Tehran hii leo, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Manouchehr Mottaki, akitishia kuichapa kibao cha mdomo Uingereza kama haitaacha kuingilia mambo ya Iran.

Urusi kujenga mfumo wa mashambulizi ya makombora

Moscow:
Urusi imesema imedhamiria kujenga mpango wa mfumo wa mashambulizi ya makombora ili kukabiliana na mpango wa Marekani wa kinga dhidi ya makombora.
Waziri Mkuu wa Urusi, Vladmir Putin, alitoa tangazo hilo wakati wa ziara yake katika mji wa Vladivostok uliopo Mashariki ya Mbali ya nchi hiyo.
Mnamo mwezi Septemba, Rais Barack Obama wa Marekani aliufuta mpango wa Marekani ulioanzishwa na mtangulizi wake, George W. Bush, wa kujenga mfumo wa kujikinga dhidi ya makombora kutoka Iran katika nchi za Poland na Jamhuri ya Czech.
Putin alisema mpango wa Marekani wa ujenzi wa mfumo wa kujikinga na makombora ulikuwa ni kikwazo kikubwa katika mpango wa nchi hizo wa kupunguza silaha za nyuklia.

Maharamia wa Somalia wateka meli mbili

Mogadishu:
Maharamia wa Somalia wameziteka meli hapo jana na kuashiria hatari kubwa inayoendelea juu ya kutumia usafiri wa meli katika eneo hilo la maji lenye shughuli nyingi za ushafirishaji wa kibiashara.
Somalia imekuwa kwenye machafuko huku ikiwa haina serikali imara tangu mwaka 1991, na makundi yanayoendesha shughuli za kiuharamia katika pwani ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika, wamefaidika kwa miaka kadhaa iliyopita.
Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Abdul Rahman Jangeli, amesema uharamia huo ni wa kupangwa.
Makundi hayo yamejikusanyia mamilioni ya dola kutokana na kuteka meli katika Ghuba ya Aden.

Uhohe hahe wa wasanii umewatajirisha Wadosi

Ni siku nyingine tena tuna ambayo imempendeza Mungu tukutane katika blog hii ambayo imekuwa mbele kukuletea habari za mtumishi wa Mungu Kabula J. George ambaye nyimbo zake zimefanyika msaada mkubwa katika jamii. Leo hii mpakwa mafuta huyo mwa Mungu ameamua kuzungumzia tena suala la usambazaji wa kazi za waimbaji wa muziki wa injili pamoja na ya kimataifa.

Ni ukweli usiofichika kwamba waimbaji wetu wa muziki wa injili pamoja na wa mataifa wengi wamekuwa wakiishi maisha duni kutokana na kushindwa kufaidika na kazi zao pindi zinapoingia sokoni. Waimbaji hao wamekuwa wakitumia gharama kubwa katika kuiandaa albamu kwa malengo kuwa, siku moja pesa yake hiyo itarudi kutokana na mauzo ya kanda, CD, ama DVD, VCD na VHS.

Kabula naye ni miongoni mwa waimbaji wa muziki wa Injili wanaolia na tatizo la dhuruma kutoka kwa wasambazji wa kazi za wasanii mbalimbali hapa nchini. Mwimbaji huyo ambaye tayari amekamilisha albamu yake ya pili inayokwenda kwa jina la Ushindi alisema kuwa, tatizo la uhohe hahe wa wasanii wetu ndiyo kimekuwa kigezo kwa wasambazaji wenye asili ya Kihindi ‘Wadosi’ kujitajirisha kupitia kazi za waimbaji hao.

Kabula alisema kuwa, wadosi hao wamebaini udhaifu wa waimbaji wa fani mbali mbali na kuona ni wakati mwafaka wa kujipatia kipato cha kuendeleza maisha yao bila kutoa jasho lolote na kuwaacha wahusika wakiishi maisha ya dhiki.

Muimbaji huyo alisema kuwa, wasambazaji hao wamekuwa wakiwaibia watumishi wa Mungu na wasanii kwa kutoa kopi nyingi wakati wa kudurufu  ikiwa ni pamoja na kuwapa pesa ndogo mara baada ya kuingia nao mikataba.

“ Inasikitisha sana kuona jasho letu linaliwa na watu wachache ambao wamebeba jukumu la kusambaza kazi zetu, na hii inatokana na uhohe hahe walionao  waimbaji wengi. Muimbaji hutumia gharama ya kurekodi, kwa sababu mpaka kukamilika kwa kazi hiyo, kunaweza kugharimu kiasi cha shilingi laki nane, hivyo pesa nyingi inatumika katika shughuli hiyo tu, na pindi kazi inapokamilika utakuta muimbaji hana fedha hata kidogo,” alisema Kabula.

Alisema, ni ukweli usiopingika kuwa, waimbaji hasa wa muziki wa Injili endapo wangekuwa na mitaji ya kutosha ya kuwawezesha kusambaza wenyewe kazi zao, leo hii hakuna msanii ambaye angekuwa analia na kunyonywa na wadosi, kwa sababu wao ndiyo wangekuwa wamiliki wa shughuli zote.

Kabula alitoa mfano kwa nchi kama Kenya ambapo baadhi ya watumishi wa Mungu na wasanii kazi zao wanasambaza wenyewe, hali ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kujikwamua kiuchumi kutokana na kipato wanachokipata baada ya kuuza kazi zao. Alisema kuwa, leo hii wadosi hao wanapanga pesa ya kumpa muimbaji husika. Mpaka leo hii kuna waimbaji wanapewa shilingi mia 100 kwa kopi moja na wengine 200 na 300.

Kabula aliongeza kuwa, tangu miaka ya 90 kipindi ambapo kanda moja ilikuwa inauzwa shilingi 700, msanii alikuwa analipwa 100 au 200 kwa kopi moja, na leo hii kanda moja inauzwa 1500 lakini muimbaji bado analipwa kiwango hicho cha pesa kwa kopi moja.

Akizungumzia suala la wezi wa kazi za waimbaji wa muziki wa dini na wa mataifa, Kabula alisema, huko nako kunatatizo kubwa sana na hiyo inamfanya  muimbaji wa asiwe na namna yoyote ya kula vema matunda ya jasho lake.
Alisema kuwa, licha ya kuwepo kwa chama cha Kutetea Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ambacho kina jukumu la kusimamia na kulinda kazi za wasanii hapa nchini, kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge mwaka 1999, bado tatizo la kuibiwa kazi zao lipo na linaendelea kwa kasi kubwa.
Wizi huo umeshamili vilivyo katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na mikoa mingine iliyompakani mwa  nchi za Kenya na Uganda. Mikoa hiyo imekuwa ikiongoza katika kudulufu CD, DVD na  VCD kisha kuzitawanya kwa wamachinga ambao nao wamekuwa wakizunguka nazo mitaani bila ya kuwa na baraka kutoka kwa husika.
Alisema kuwa hali hiyo inatokana na kutokuwa na  sheria za kulinda na kutetea vema kazi za wasanii hapa nchini. Kwa mfano  miaka ya hivi karibuni, COSOTA ilifanikiwa kukikamata kiwanda  cha kuzalisha nyimbo za wasanii mbalimbali eneo la Buguruni Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, lakini cha kushangaza mtuhumiwa huyo alilipa faini ya 200,000 tu ambayo hailingani na gharama ambazo wamiliki wa kazi hizo waligharamia katika kuzitengeneza.
Aidha, hivi karibuni, Chama cha Haki Miliki na Shiriki Tanzania, COSOTA, ambacho kinasimamia kazi za wasanii, kiliwanasa watu wawili waliokuwa wanajihusisha na shughuli ya kudurufu kazi za wasanii zenye thamani ya sh.161milioni .

Watu hao ni Loveness Masonda, wa Tabata na Ayaj Chavda, wa Kariakoo, ambao kila mmoja kwa wakati wake walitengeneza na kuuza kazi hizo bila vibali vya wamiliki wa kazi hizo.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani, lakini mpaka sasa haijulikani nini kinaendelea juu yao. Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, wa chama hicho Yustus Mkinga alisema kuwa, Loveness alikuwa anamiliki mtambo wa kudurufu wenye uwezo wa kufyatua kaseti 16 kwa dakika tatu, nyumbani kwake na alikuwa na karatasi maalum pamoja na vyombo vya kudurufia 'scanner' anavyotumia kuiba kazi za wasanii na kubandika nembo ambayo si rahisi kwa mteja kugundua kuwa ni feki.

Ilielezwa kuwa, Shavda alikuwa akitengeneza kwa kununua nakala moja ya picha za kihindi na kubadili lugha ya picha hiyo kuwa kwa kiswahili na yeye kutengeneza kopi zaidi ya laki tatu na kuziuza mitaani huku zikitoka kwa nembo yake kama mmiliki halali wa kazi hizo.

SIFA FM, redio ya Kikristo nchini Kenya.

Mmoja wa watangazaji wa redio hiyo iliyopo Voi  km 350 kusini mashariki mwa Nairobi ina 600w yenye uwezo wa kusikika sehemu ya jirani umbali wa eneo la duara km 250.

Kwa kuwa sehemu ndani ya pwani ni jimbo la Kenya Sifa FM imechukua sehemu kubwa yenye mkusanyiko wa waislamu ndani ya Kenya, pamoja na miji mikubwa katika pwani. Makadirio ya wasikilizaji ni kama millioni 3, pamoja na vikundi vya watu ambao wengi wao 100% ni waislamu. Scripture Mission tuna saa tatu (3) kila siku iliyo tafsiriwa kwa dakika 36/20, vipindi 6 vya uinjilisti na ufuasi kwa wiki, ni vipindi maalumu kwa waislamu.

Uchaguzi 2010: Maaskofu watoa ujumbe mzito

MALASUSA ADAI VIONGOZI WANG’ANG’ANIZI WATABAINIKA

HOMA ya uchaguzi mkuu mwakani imeanza kupanda miongoni mwa viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali ambao wametumia mahubiri yao katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi kuwaonya wanasiasa na kutahadharisha wananchi kuwa waangalifu wakati taifa linajiandaa na uchaguzi huo.
Akitoa mahubiri katika Kanisa la Azania Front jijini Dar es Salaam jana, Akofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa alisema dhana ya kung’ang’ania madaraka itajidhihirisha mwakani wakati wa uchaguzi mkuu.
Alisema katika kipindi hicho wabunge hujitokeza na kuonyesha kwamba wao ndiyo wamiliki wa majimbo.
“Ving’ang’anizi tutawaona mwakani katika uchaguzi mkuu, mara watajitokeza wabunge watakaosema hili ni jimbo langu…hivi ndivyo Herode alivyokuwa baada ya kusikia Yesu amezaliwa na atakuwa mfalme,” alisema.
Dk. Malasusa alibainisha kwamba si wabunge pekee wenye hulka hiyo bali hata maofisini tabia hiyo bado ipo.
Kwa upande mwingine, alieleza dunia ya sasa imejaa ukandamizaji na pia haimjali mtu masikini na kuwataka waumini hao kupendana.
Aliwasifu wazee kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhudhuria ibada na kuwataka kuwahamasisha vijana nao kufanya hivyo kwani kwa sasa hali yao kiimani inazidi kuwa mbaya.
Kwa upande wake, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki, Dar es Salaam, Methodius Kilaini, aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na Watanzania kuwa waangalifu wakati taifa linajiandaa na uchaguzi mkuu, ili kuepuka vurumai kama mataifa mengine.
“Leo tunaposherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo, napenda kuwakumbusha kuwa mwaka 2010 ni mwaka wa uchaguzi mkuu… hiki ni kitu muhimu mno, tunaomba ufanyike kwa amani na kwa mafanikio makubwa, ili kuepuka matatizo.
“Nawaomba viongozi wa vyama vya siasa, wapitishe zoezi hili kwa usalama, upendo ili mwishowe tufike mwisho wa siku tukiwa salama,” alisema.
Askofu Kilani ambaye sasa amehamishiwa katika Jimbo Kuu la Bukoba, alisema kutokana na mapenzi aliyonayo Mungu kwa taifa hili, Watanzania wanapaswa kuendeleza upendo, mshikamano na uelewano uliopo.
“Tuombe msamaha pale tulipokosea, Mungu awape nguvu, umoja na uelewano miongoni mwenu ili kudhihirisha kweli leo tunaadhimisha mtoto, mkombozi Yesu Kristo amezaliwa ili kutukomboa,” alisema.
Aliwasihi waumini kote nchini kuendelea kuliombea taifa kwa yote yaliyotendeka ingawa hakufafanua ni mambo gani.
Katika hatua nyingine, Askofu Kilaini alitumia nafasi hiyo kuwaaga rasmi waumini wa dhehebu lake mkoani Dar es Salaam, huku akisisitiza kuwa atawakumbuka kwa ukarimu wao ambao amekuwa nao katika utumishi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
“Narudishwa kwenye jimbo ambalo nimetoka miaka 37 iliyopita, napenda kuwahakikishia kwamba nitaendelea na uzi uleule wa kutetea kile ninachokiamini,” alisema Askofu Kilaini.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana, Valentino Mokiwa aliwataka viongozi wa serikali kuzaliwa upya ili kuepuka matatizo yanayowapata.
Aliyasema hayo juzi usiku wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Krismasi kwenye Kanisa la St. Albano, Dar es Salaam ambapo alisema kutokana na matukio yanayowapata viongozi wanastahili kuzaliwa upya ili kuepuka aibu kwa taifa.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Kardinal Polycarp Pengo aliwatoa hofu waamini wa dhehebu juu ya uchaguzi mkuu ujao kuwa utakuwa wa haki na amani.
Askofu Augostine Ndeliakyama Shao wa Kanisa la Minara Miwili, Mji Mkongwe, Zanzibar, alisema viongozi wa siasa nchini wanakwepa kuwapa wananchi elimu ya uraia, kwa kuhofia watawakataa katika uchaguzi baada ya kuelewa haki zao za msingi.
Akizungumza wakati wa ibada ya mkesha wa Krismasi, alisema: “Elimu ya uraia inapingwa na baadhi ya wanasiasa, kwani wanajua elimu ni nguvu ya mnyonge, hivyo hawatapata fursa ya kudanganya wapiga kura.”
Askofu huyo ambaye amekuwa mstari wa mbele kutetea misingi ya haki za binadamu na utawala bora nchini, alisema hivi sasa taifa linakabiliwa na tatizo la kukithiri kwa ufisadi na kuathiri wananchi wanyonge na kunufaisha wawekezaji kutoka nchi za kigeni.
Alisema kilio cha Watanzania wengi hivi sasa ni kukithiri kwa ufisadi na kwamba njia pekee ya kuondokana na hali hiyo ni kufanyika mabadiliko ya kiuongozi.
“Umasikini uliokithiri katika jamii ni wimbo usiofurahisha kwa rushwa na ufisadi, wizi wa mali ya umma na kutowajibika kwa viongozi wa jamii, haya yote ni madhaifu yanayoashiria tupo gizani na kuna ulazimika wa mabadiliko,” alisema.
Alisema Tanzania hivi sasa ni nchi ya 102 katika orodha ya nchi 180 zinazotajwa kukithiri kwa rushwa, na itaendelea kukamata nafasi hiyo mbaya, iwapo suala hilo halitapigwa vita katika uchaguzi wa mwakani.
Aidha, alisema kitendo cha wafanyabiashara Zanzibar kuachiwa kupandisha bei ya mafuta ya dizeli wapendavyo, ni kielelezo kwamba wahusika wa kulinda sheria za nchi hawawajibiki na hivyo kusababisha athari kubwa kwa wananchi.
Alieleza viongozi wote wana wajibu wa kusimamia haki na maslahi ya raia na hivyo haikuwa haki kuachiwa kupandisha bei za mafuta watakavyo.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Dk. Owdernbug Mdegella, aliwataka Watanzania kuepuka kuendelea kulalamika dhidi ya mawaziri na wabunge mafisadi, kwani hawakujiweka madarakani bali wamewekwa na wananchi na kwamba dawa ya kuwaondoa mwakani ipo mikononi mwao na si mahakama.
“Watanzania hatujui kuchagua viongozi bora na ndiyo maana tumekuwa watu wa kuwalalamikia viongozi mafisadi wakati chungu cha kupika mafisadi ni kura zetu,” alisema.
Alisema wabunge na mawaziri wanaolalamikiwa kwa ufisadi na uwajibikaji mbovu katika nafasi zao wamefika bungeni na kuteuliwa mawaziri baada ya wananchi kuwapigia kura na kusema kwamba kama wanaamini walifanya makosa katika uchaguzi huo wasirudie tena makosa hayo kwenye uchaguzi mkuu mwakani.
Akitoa salamu baada ya kumaliza shughuli za ibada ya tatu katika Usharika wa Iringa Mjini, alisema kwa upande wake ameamua kwa mwakani kuzungumzia mambo makuu manne likiwemo la wakazi wa Iringa kutoogopa kufa hata kuamua kujinyonga, suala la kilimo ambalo wananchi wanauelewa mkubwa ila wanakwamishwa na viogozi wabovu, ushuhuda wa kikristo kwa kuepuka kufanya maovu wakati wa sikukuu na kupata viongozi bora.
Hivyo hivyo, alisema ili kumpata kiongozi bora ni lazima kila Mtanzania mwenye sifa kujiandikisha kupiga kura na kushiriki kupiga kura wakati wa uchaguzi.
Aidha, alisema Watanzania wamekuwa ni watu wa kulalamika kuhusu viongozi mafisadi huku wao wakikwepa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Hivyo alishauri kuwepo kwa mkakati kamili kutoka kwa wananchi wote ili kuhakikisha wale wenye sifa wanajitokeza kugombea nafasi mbalimbali bila kujali chama cha siasa kama njia ya kuwaondoa viongozi mafisadi.
“Nimewaambia Iringa haiendelei kwa sasa, tunashindwa kuchagua viongozi bora… sasa ili kupata viongozi bora lazima wote tushiriki kuchagua viongozi pamoja na kujitokeza kugombea kwa wale wenye sifa… wengine wanasema tatizo viongozi waliochaguliwa ni mafisadi tu… sasa wewe usiye fisadi mbona hujagombea?” alihoji.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, aliitaka jamii kuiombea nchi katika uchaguzi mkuu ujao kwani mazingira yaliyopo yanaonyesha kukosekana kwa haki na amani na kuongeza kuwa kanisa hilo litaandaa semina mbalimbali za kuelimisha wanajamii kuhusu haki zao kama kupiga kura.
Habari hii imeandaliwa na Kulwa Karedia na Sauli Giliard (Dar), Makame Amer (Zanzibar), Francis Godwin (Iringa) na Beatrice Maina kutoka Moshi.
Chanzo:tzdaima

Mr.Nice kweli ameokoka?

Kumekuwa na maswali mengi juu ya wokovu wa aliyekuwa mkali wa sataili ya Takeu  Mr.Lucas Mkenda (Mr.Nice ) kukaa kimya baada ya kudaiwa kuokoka na kutaka kufyatua albamu yake ya kwanza ya nyimbo za injili. Hivi karibuni, Mr.Nice alipanda jukwaani na kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu katika huduma ya Ngurumo za Upako iliyopo Arusha. Wemgi wanauliza, kama kweli kaokoka mbona yupo kimya tofauti na walivyookoka akina Cosmas Chidumule, Mzee Makas ambao nao  kwa sasa ni waimbaji wa Nyimbo za injili.(Picha kwa hisani ya Ngurumo ya Upako)

Mr.Nice kweli ameokoka?

Kumekuwa na maswali mengi juu ya wokovu wa aliyekuwa mkali wa sataili ya Takeu  Mr.Lucas Mkenda (Mr.Nice ) kukaa kimya baada ya kudaiwa kuokoka na kutaka kufyatua albamu yake ya kwanza ya nyimbo za injili. Hivi karibuni, Mr.Nice alipanda jukwaani na kuimba nyimbo za kumtukuza Mungu katika huduma ya Ngurumo za Upako iliyopo Arusha. Wemgi wanauliza, kama kweli kaokoka mbona yupo kimya tofauti na walivyookoka akina Cosmas Chidumule, Mzee Makas ambao nao  kwa sasa ni waimbaji wa Nyimbo za injili.

Newer Posts Older Posts