LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

12/30/09

SOLOMONI MUKUBWA KUITEKA MWANZA

MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Solomon Mukubwa anatarajiwa kuliteka jiji la Mwanza katika  Tamasha la Mwaka mpya litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba mkoani humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, aliiambia Mwananchi jana kuwa Mukubwa amethibitisha na ataingia na albam yake iitwayo Mungu Mwenye Nguvu.

Msama alisema Mukubwa atafuatana na wasanii mbalimbali maarufu wanaolijenga kundi lake pamoja wacheza shoo wa nyimbo za injili.


Baadhi ya wasanii wa Tanzania katika tamasha holo ni pamoja na Rose Mhando, Bahati Bukuku pamoja na Kundi la Upendo la Kijitonyama, dar es Salaam ambalo mbali na kushiriki, wataadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa pamoja na kutambulisha albam yao, Jina Lako Li Hai.

Misr yaruhusu wanaharakati 85 kuingia Gaza.


Cairo.
Serikali ya Misr jana Jumatano imewaruhusu wanaharakati 85 wa kimataifa kuingia katika ukanda wa Gaza baada ya kuomba kwa muda mrefu kuruhusiwa kuingia katika eneo hilo kupitia katika kivuko cha mpakani nchini Misr cha Rafah kwa ajili ya ujumbe wa kiutu. Hata hivyo haijafahamika iwapo wanaharakati hao, ambao wanasemekana kufikia kiasi cha 1,300 wanakubali kuruhusiwa kwa baadhi yao kuingia katika ukanda wa Gaza. Wengi wao wamekuwa wakifanya maandamano mjini Cairo kuhusiana na uamuzi wa Misr wa kuwazuwia kuingia katika ukanda wa Gaza.
Watayarishaji wa maandamano ya uhuru wa Gaza wamesema kuwa wanaharakati hao kutoka nchi 42 duniani wameingia nchini Misr kujaribu kuingia katika ukanda wa Gaza kutoa msaada na kushiriki katika maandamano ya amani wakipinga kufungwa kwa mipaka ya ukanda wa Gaza.

Viongozi wa upinzani wakimbia Iran.


Tehran.
Shirika  la  habari  la  taifa  nchini  Iran  IRNA, limeripoti kuwa  viongozi  wawili  maarufu  wa  upinzani  nchini  humo wamekimbia  kutoka  mji  mkuu  Tehran   kwa  hofu  na wamekimbilia  katika  jimbo  la  kaskazini  mwa  nchi  hiyo. Ripoti  hizo  zinamaana  kuwa  viongozi  hao  wawili  ni viongozi  wakuu  wa  upinzani  nchini  humo , Mir  Hossein Mousavi  na  Mehdi  Karroubi. Hata   hivyo , mmoja  wa watoto  wa  Karoubi , ameliambia  shirika  la  habari  la Parleman  ambalo  huchukua  msimamo  wa  kati  kuwa baba  yake  na  Mousavi  wote  bado  wako  mjini  Tehran. Mamia   kwa  maelfu  ya  watu  walishiriki  katika maandamano  kadha  ya  kuiunga  mkono   serikali, yaliyotayarishwa  na  viongozi  wa  kidini  na  kisiasa kutokana  na  wimbi  la  maandamano  ya  wapinzani ambayo  yamekuwa  yakifanyika  nchini  kote. Ujerumani na   umoja  wa  mataifa   zimewataka  maafisa  wa  Iran kuwa  watulivu  wakati  wakiwashughulikia    waandamanaji wa   wanaopinga  serikali.

Newer Posts Older Posts