LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

12/31/09

Zaidi ya watu milioni moja wakaribisha mwaka mpya Berlin

BERLIN:

Katika mji mkuu wa Ujerumani Berlin, zaidi ya watu milioni moja wameukaribisha mwaka mpya 2010. Tangu jana mchana, watu walianza kumiminika katika eneo maalum lililotengwa kwa sherehe za mwaka mpya kwenye barabara ya urefu wa kilomita mbili, kuelekea Lango la Brandenburg
Hapo awali, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Benedikt wa 16, alitoa mwito kwa waumini waliokusanyika uwanja wa St. Peters mjini Vatikan na kote ulimwenguni, kusaidia familia zilizoathirika kwa msukosuko wa uchumi na ukosefu wa ajira.
Sherehe za kukaribisha mwaka mpya kama kawaida zilianzia Australia kwenye bandari ya Sydney kwa maonyesho makubwa ya fashifashi. Katika jiji la New York kumechukuliwa hatua za kuimarisha usalama.


Mwaka 2009 ulikuwa mgumu sana kwa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan

BERLIN:
Mwaka 2009 ulikuwa mgumu na hatari sana kwa ujumbe wa wanajeshi wa Ujerumani "Bundeswehr" nchini Afghanistan. Wizara ya Ulinzi ya Ujerumani imethibitisha taarifa ya gazeti la "Bild" kuwa wanajeshi watano wa Kijerumani waliuawa mwaka 2009, ikiwa ni wawili zaidi kuliko katika mwaka 2008.
Kwa mujibu wa makao ya vikosi vya Ujerumani mjini Potsdam, wanajeshi wanne waliuawa katika mapambano na mmoja alifariki katika ajali ya barabarani. Vile vile katika mwaka 2009 mashambulio 77 yaliwalenga wanajeshi wa Kijerumani - 71 yalitokea Kunduz pekee, kaskazini ya Afghanistan. Katika mwaka 2008 vikosi vya Ujerumani huko Afghanistan vilishambuliwa mara 43.

RATIBA YA MAZISHI YA SIMBA WA VITA


 Mwili wa Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa ‘Simba wa Vita’ utatolewa leo Ijumaa katika hospoiali ya Jeshi Lugalo saa 7:00 mchana na utapelekwa katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya wananchi kutoa heshima za mwisho. Mazishi ya yanatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi nyumbani kwa marehemu Madale jijini Dar es Salaam.
Hii ni ratiba fupi iliyotolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. William Lukuvi.
Mh Lukuvi amewataka pia wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kuanzia majira ya saa saba mchana kumuaga aliyekuwa mpendwa wetu Simba wa Vita.

ROSE MHANDO NA SOLOMONI MKUBWA KULIFUNIKA TAMASHA LA ZABURI GOSPEL SEARCH LEO?

Wakazi wa mkoa wa Mwanza leo watausherehekea vema mwaka 2010 kutokana na matamasha makubwa mawili yatakayokuwa yakimtukuza Mungu kwa njia ya uimbaji kwenye viwanha viwili tofauti.

Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kutakuwa na tamasha la mwaka mpya lililochini ya Alex Msama na Katika Uwanja wa Nyamagana kutakuwa na Shindano la kumpata mshindi wa Zaburi Gospel Search 2009 huku kiingilio kikifanana, cha 5000 kwa viti maalum na 2000 kwa viti vya kawaida.
Mbali na Rose na Solomoni waimbaji wengine watakao imba leo katika tamasha la Mwaka mpya ni Bahati Bukuku, Jennifer Mgendi, Geraldine Oduor, Upendo Nkone, Enock Jonas, Flora Mbasha na Kundi la Muziki wa Injili la Upendo la Kijitonyama, Dar es Salaam.

FAINALI YA MSHINDI WA ZABURI GOSPEL SEARCH NI LEO


Fainali ya kumpata mshindi wa shindano la Zaburi Gospel Search 2009, anatarajiwa kupatikana leo kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza na ataondoka na gari aina ya Toyota Vistar yenye thamani ya milioni nane.
Mshindi wa pili katika shindano hilo  ataondoka na seti ya vyombo vya muziki vyenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kutoka kampuni ya Samila Mobile Sound, mshindi wa tatu atajinyakulia kitita cha shilingi laki mbili, pia mshindi wa kwanza mpaka wa tano watarekodiwa albamu moja moja na studio za Habari Maalum.
Kiingilio katika shindano hilo litakaloanza majira ya saa saba mchana ni 5000 kwa viti maalum na 2000 kwa viti vya kawaida na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini wiliam Ngereja.
Lengo la shindano hilo linaloendeshwa na Kampuni ya Flora Promotions ya jijini Mwanza ni kukuza na kuwezesha vipaji vya waimbaji wa muziki wa Injili kumtumikia Mungu ipasavyo.






HERI YA MWAKA MPYA 2010


Wapendwa wasomaji wangu wa blog hii, kutoka kila pembe ya dunia hasa Marekani, Uingereza, Kenya  na nyumbani Tanzania nawatakia kila la heri ya mwaka mpya wa 2010. Nawashukuru kwa kuungana nami tangu nilipoifungua blog hii mwaka jana. Naomba mnitumie maoni ya kunieleza nini nikifanye ili kuhakikisha ninaiboresha blog hii hasa mwaka 2010. Mnapenda niongeze vitu gani ama nipunguze vipi kwa ajili ya kukufurahisha mpwanda wangu. Sina mengi ya kusema ila tumuombe Mungu atuvushe mwaka huu salama japo zimebaki saa chache.

Naitwa George Kayala,
Nipo Tabata, Dar es Salaam, Tanzania,
Simu 0755 240 136,
E-mail, georgeekayala@yahoo.com

Albamu ya Ushindi yawa tiba kwa watu wenye matatizo sugu



Nivigumu kuamini lakini ni kweli juu ya mambo yanayojitokeza kwa watu wanaoisikiliza albamu ya Ushindi ya mpakwa mafuta wa Mungu Kabula J.George ambayo imegeuka kuwa tiba kwa watu wenye matatizo sugu ambayo yameshindikana kutibiwa kwa madaktari bingwa na waganga wa kienyeji.
Albamu hiyo iliyo katika mfumo wa Audio, CD, VCD na DVD imewafungua watu wengi waliokuwa wamefungwa na nguvu za giza kwa kubambikiwa magonjwa sugu kama Malaria, Kisukari, Presha, Kukosa nguvu za kiume, Kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa, Moyo mpana, Uvimbe tumboni, Utasa, (Ugumba), Miguu kuwaka moto, Kutofanya kazi kwa figo, Maumivu ya mgongo, aleji na mengine yanayofanana na hayo.

Wakizungumza kwa njia ya simu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, watu waliokumbana na miujiza hiyo walisema kuwa, albamu hiyo imesheheni nyimbo zilizojaa utukufu wa Mungu hasa wimbo wa Dhihirisha na Hakuna muweza, zimeonekana kuwa msada kwa waliokuwa wasumbuliwa na matatizo hayo ambayo yaliwatesa kwa miaka mingi.

Wakiongea kwa nyakati tofauti, Josephat Magesa, Epa Hamza (Mwanza), Sophia Peter (Kahama), Lukas Mayunga (Kilosa) na Lyimo Lyatonga (Kilimanjaro) walisema baada ya kuipata albamu hiyo, walisikiliza kwa kumanisha nyimbo za Dhihirisha na Hakuna mumeza na kujikuta wanapokea uponyaji bila kuombewa na watumishi wa Mungu kama ilivyozoeleka.
  ===========================

WIMBO WA DHIHIRISHA
==========================
WIMBO WA HAKUNA MUWEZA

KAMANDA KOVA AHIDI KUWADHIBITI WATU WAKOROFI JIJINI DAR



Kamishina Mkuu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ameahidi kuwepo ulinzi mkali katika shamrashamra ya kuukaribisha mwaka mpya 2010. Kova amesema kuwa jeshi lake limejipanga vema kuhakikisha linadhibiti baadhi ya watu wakorofi hasa watakaokaidi agizo la kutochoma mataili sehemu za barabarani na hata mitaani. Kova pia amewazuia watu kurusha fataki kama ishara ya kuukaribisha mwaka mpya.

HISTORIA YA RASHIDI MFAUME KAWAWA



Kawawa alizaliwa Mei 27 , 1926 huko Songea kijiji cha Matepwende mkoani Ruvuma. Alianza elimu ya msingi huko Liwale Lindi. Aliendelea na elimu ya kati (middle school) hapo Dar-es-Salaam school ambapo mmojawapo wa wanafunzi wengine ni marehemu mzee Kanyama Chiume mpigania uhuru toka Malawi aliyeishi uhamishoni nchini Tanzania kwa muda mrefu. Wengine katika shule hiyo wakati huo ni pamoja na kina Abdul Sykes, Ali Sykes, Hamza Aziz na Faraji Kilumanga. Aliendelea na masomo yake huko Tabora Boys kati ya 1951-1956. Alikuwa ni Waziri Mkuu wa Tanganyika mwaka 1962 wakati Mwalimu Nyerere alipoamua kwenda mikoani kujenga chama na kufanya shughuli za kisiasa. Baadaye aliteuliwa tena kuwa Waziri Mkuu mwaka 1972-1977 na akawa miongoni mwa wahamasishaji wakubwa wakati wa vita ya kumng'oa nduli Idi Amin ambapo alitembelea wapiganaji wetu waliokuwa mstari wa mbele kule Uganda. Hii ilimpatia jina la "Simba wa Vita" jina ambalo lilimkaa vyema kwa muda mrefu. Kabla ya kuingia katika harakati za kupigania Uhuru Mzee Kawawa alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa Shirikisho la Wafanyakazi mwaka 1955 ambapo alichaguliwa kuwa Katibu wake Mkuu wa kwanza. Ni katika nafasi hii ndiyo aliweza kuanza kushiriki kwa nguvu zaidi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika akihamasisha wafanyakazi. Kabla ya hapo alikuwa ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi wa Serikali. Februari 1956 Mzee Kawawa aliacha kazi yake ya Shirikisho la Wafanyakazi kutokana na kuwa mwajiriwa wa serikali kitu ambacho kilimkataza kuhusisha na siasa na kuamua kuingia katika harakati za kudai uhuru kupitia TANU. Alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU mwaka 1957, Makamu mwenyekiti wa TANU mwaka 1960. Mwaka 1964 baada ya Muungano Mzee Kawawa alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais akiwa ni msaidizi wa Rais wa Muungano kwa upande wa mambo ya Bara. Katika siasa amewahi kushika nafasi mbalimbali ikiwemo ile ya Ukatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM na amekuwa mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CCM. Mzee Kawawa alikuwa ni mtoto wa kwanza kati ya watoto nane na mojawapo ya kazi zake za awali ilikuwa ni uchezaji wa filamu za uhamasishaji na akawa ndiye mcheza filamu wa kwanza kiongozi mweusi.

KIFO CHA MZEE KAWAWA, TAIFA KUOMBOLEZA SIKU SABA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ametangaza siku saba za maombolezo kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mzee Rashid Mfaume Kawawa, aliyefariki duania leo saa 3:20 asubuhi baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu.

Rais alisema kuwa taratibu zote mazishi zitasimamiwa na serikali na atapewa heshima kwa muasisi wa kupigania uhuru wa Tanzania
Rais Kikwete na mkewe Mama Salima Kikwete wakimuangalia Hayati Mzee Kawawa jana alipokuwa amelazwa kwenye chumba cha watu mahututi kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili.


MZEE RASHID KAWAWA AFARIKI DUNIA


Habari za kusikitisha za asubuhi ya leo zinasema kuwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Awamu ya Kwanza wa Serikali chini ya hayati Baba wa Taifa, JK. Nyerere, Mzee Rashid Mfaume Kawawa, ambaye alizushiwa kifo jana, amefariki dunia leo asubuhi hii.  Mzee Rashid Kawawa, amefariki ikiwa ni saa chache kumalizika kwa  mwaka 2009 na amekufa akiwa na umri wa miaka 83. Enzi za uhai wake, Mzee kawawa alijulikana kwa jina la Simba wa Vita. MUNGU AILAZE ROHO YAKE PEPONI - AMIN!

Newer Posts Older Posts