LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

01/03/10

MAONI YA WATEMBELEAJI WA BLOG

JE, UMEFURAHISHWA NA KITUGANI NDANI YA BLOG HII BAADA YA KUITEMBELEA? TOA MAONI YAKO KWENYE KISANDUKU KILICHO KULIA KWAKO SEHEMU ILIYOANDIKWA ADD YOUR COMMENTS HERE, KISHA BONYEZA SEHEMU ILIYOANDIKWA POST, NAMI NITAYAFANYIA KAZI ASANTE KWA KUITEMBELE BLO HII

Eritrea yailaumu Ethiopia kwa kuishambulia


ADDIS ABABA
Eritrea jana imeituhumu Ethiopia iliyo adui wake mkuu kuwa imefanya mashambulio kwenye mpaka wenye mgogoro. Lakini Eritrea imesema majeshi yake yalijibu shambulio hilo na wanajeshi 10 wa Ethiopia waliuawa na wawili walikamatwa.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wizara ya mambo ya nje ya Eritrea imesema wanajeshi wa chama tawala cha Ethiopia cha Tigrai People's Liberation Front-TPLF walishambulia eneo la Zalambesa siku ya Ijumaa. Ripoti hiyo pia imesema kuwa maafisa wa Ethiopia hawakupatikana kutoa maelezo yao kuhusu suala hilo.
Chama cha Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi cha TPLF ni mwanachama mkuu katika serikali ya muungano na kilikuwa mshirika wa karibu wa serikali ya Eritrea kabla ya nchi hizo mbili hazijaanza kugombania eneo la mpakani.


Watu 50 wauawa katika mapigano Somalia.


Mogadishu:
Nchini Somalia, takriban watu 50 wameuawa na wengine 100 wamejeruhiwa katika mapigano makali kati ya wanamgambo wanaoiunga mkono serikali na wapiganaji wa kiislamu, waliokuwa wakijaribu kuuteka nyara mji wa Dhusamareb ulioko katikati ya Somalia.
Ripoti zinasema kwamba Kundi la Ahlu Sunna Jammaa, ambalo ni washirika wa serikali ya nchi hiyo walifanya mashambulio ya kujikinga dhidi ya wanamgambo wa Al Shabaab ambao wanauhusiano na mtandao wa Al Qaeda na kuwaondoa katika mji huo.
Wakati huohuo Waziri Mkuu wa Somalia Omar Abdirashid Ali Sharmarke ameliambia Shirika la habari la Uingereza kwamba majeshi ya serikali yapo tayari kuanza mashambulizi makali dhidi ya wapiganaji na kutarajia kuwaondoa waasi hao nje ya mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu ifikapo mwishoni mwa mwezi

Theluji nyingi yasababisha safari za ndege kuahirishwa Ujerumani.



Frankfurt:
Hali ya hewa ya baridi inayoambatana na theluji nyingi imeikumba tena Ujerumani, ambapo katika uwanja wa ndege wa Frankfurt kuanguka kwa theluji nyingi kumesababisha ndege nyingi kuahirisha safari zake.
Katika Uwanja wa Ndege wa Dortmund ndege ya Shirika la ndege la ''Air Berlin'' iliyokuwa ikianza kuruka ikiwa na abiria 165 ndani yake iliteleza na kuacha njia yake hali iliyosababisha uwanja wa ndege kufungwa kwa muda.
Kuanguka kwa theluji nyingi katika msimu huu wa majira ya baridi pia kumesababisha hali ya hatari ya msongamano wa magari.
Wakati huohuo zaidi ya asilimia 90 ya ndege katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing, zimeahirisha safari zake ama kuchelewa kutokana na theluji nyingi, na kuacha maelfu ya abiria wakiwa wamekwama, huku baadhi ya viwanja vya ndege katika miji ya jirani vikiwa vimefungwa.

Marekani na Uingereza zafunga balozi zao Yemen.


Sana'a:
Marekani na Uingereza zimefunga balozi zake zilizoko katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a.
Balozi hizo zimefungwa kutokana na vitisho vinavyotolewa na tawi la Mtandao wa Kigaidi wa Al Qaeda katika rasi ya Arabuni, kushambulia maslahi ya Marekani nchini Yemen.
Baada ya kushindwa kwa jaribio la kulipua ndege ya abiria ya Marekani siku ya Krismas, Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown alisema Uingereza na Marekani zinaimarisha juhudi zake za kukabiliana na ugaidi nchini Yemen, nchi ambayo imekuwa kituo cha magaidi wenye msimamo mkali.
Oton Brown
''..Anasema Yemen imetambulika kama Somalia, kuwa eneo moja wapo ambalo sio tu wanapaswa kulitizama, lakini wanapaswa kulichukulia hatua zaidi.
Aidha amefahamisha kuwa ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi unaimarishwa zaidi...''
Hatua mbalimbali tayari zimechukuliwa kupambana na ugaidi nchini humo, ikiwemo kulisaidia jeshi la nchi hiyo na kutoa msaada wa kifedha kwa kikosi cha nchi hiyo cha kupambana na ugaidi.
Kamanda wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, Jenerali David Petraeus amekutana na Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh kuzungumzia hatua za kuchukua kukabiliana na wapiganaji nchini humo.

Ujerumani kuanza kutumia mashine za ''Scanners'' katika viwanja vyake vya ndege.



Berlin:
Serikali ya Ujerumani katika kipindi cha mwaka huu, inatarajia kuanza kutumia mashine za kumulika mwili katika viwanja vyake vya ndege, ukiwemo Uwanja wa Ndege wa Frankfurt, ambao ni wa pili barani Ulaya wenye kutumika sana.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Wolfgang Bosbach, amesema majaribio yataanza kufanyika ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.
Tangu kutokea kwa jaribio la kulipua ndege wakati wa Krismas lililofanywa dhidi ya ndege ya Marekani, hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kuimarisha ulinzi, hali ambayo pia imezua mabishano kuhusiana na mashine za kumulika miili zilizoanza kutumiwa na badhi ya nchi kwamba zinafikiriwa kukiuka faragha ya wasafiri.
Katika hatua nyingine, Uingereza nayo pia imetangaza kwamba itaweka mashine hizo katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow, baada ya serikali kuridhia.
Uwanja wa Ndege wa Schipol wa Amsterdam ulitangaza wiki iliyopita kwamba mwisho wa mwezi, utaanza kutumia mashine hizo.

Marekani yatangaza utaratibu mpya kwa wasafiri waingia nchini humo.


Washngton:
Idara inayohusika na Usalama wa Usafari nchini Marekani imetangaza ukaguzi zaidi kwa wasafiri wa ndege kutoka Nigeria, Yemen, Pakistan, Afghanistan, Saudi Arabia na nchi nyingine tisa.
Utaratibu huo mpya wa Usalama, ambao unaanza kutumika leo, utawataka wasafiri kabla ya kupanda katika ndege kukaguliwa mwili mzima, kukagua mizigo, ikiwemo pia kuchunguza vifaa vya milipuko.
Sheria hiyo mpya imekuja kufuatia jaribio la kulipua ndege ya Marekani ilipokuwa ikijiandaa kutua katika Uwanja wa ndege wa Detroit siku ya Krismas, jaribio ambalo lilifanywa na raia wa Nigeria, ambaye Marekani inaamini kuwa amepewa mafunzo na mtandao wa Al Qaeda ulioko Yemen.

Newer Posts Older Posts