LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.

IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

01/04/10

MAONI YA WATEMBELEAJI WA BLOG

 ASANTE KWA KUITEMBELEA BLOG HII, JE, UMEFURAHISHWA NAYO? TOA MAONI YAKO KWENYE KISANDUKU KILICHO KULIA KWAKO SEHEMU ILIYOANDIKWA ADD YOUR COMMENTS HERE, KISHA BONYEZA SEHEMU ILIYOANDIKWA POST, ZUNGUMZA NA JAMAA NA MAFARIKI, IFANYE BLOG HII IWE YAKO.

Clinton aonya udhaifu wa Yemen waweza hatarisha kanda nzima.

Washngton:

Waziri wa Mambo ya Nchi za nje wa Marekani Hilary Clinton ameonya kwamba udhaifu uliopo nchini Yemen, unaweza kutishia udhabiti wa eneo hilo.
Taarifa za uwezekano wa kufanyika kwa mashambulio, iliyotolewa na kikundi kinachojiita Al Qaeda katika rasi ya Arabuni, imeifanya Marekani kufunga ubalozi wake, katika mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa, siku ya Jumapili.
Muda mfupi tu, baadaye Uingereza na Ufaransa nazo zikafanya hivyo.
Seneta wa Marekani Joseph Lieberman amesema nchi yake na Uingereza zimekuwa zikiimarisha juhudi zao za kukabiliana na ugaidi nchini Yemen.

''..Anasema wamechukua hatua katika operesheni zao kuiunga mkono serikali ya Yemen dhidi ya magaidi nchini humo, na kwamba inabidi kufanya hivyo vinginevyo Yemen itakuwa kama Iraq na Afghanistan, na kwamba hawataki hilo litokee.
Wakati huohuo, Mahakama ya rufaa nchini Marekani imethibitisha hukumu ya kifungo cha maisha kwa mshtakiwa Zacarias Moussaoui.
Mshtakiwa huyo raia wa Ufaransa, ndiye pekee aliyetiwa hatiani katika mahakama ya Marekani kwa makosa ya kuhusika katika shambulio lililotokea Septemba 11, mwaka 2001.
Moussaoui jana alishindwa jaribio la kutengua makosa yake ya kula njama katika shambulio hilo, na kuhukumiwa upya.

Marekani yachunguza kwa kina washukiwa wake wa ugaidi.

Washngton:
Marekani inachunguza kwa kina, orodha yake ya washukiwa wa ugaidi, huku ikiwaongeza zaidi washukiwa hao katika orodha ya wale wasiotakiwa kusafiri nchini humo.
Sheria mpya katika viwanja vya ndege vya kimataifa nayo pia imeanza kutumika nchini humo, ambapo abiria wote wanaosafiri na ndege za nchi hiyo sasa wanapaswa kufanyiwa ukaguzi wa kina na mizigo yao pia kukaguliwa, na ikibidi kwa kutumia vifaa maalum vya kubaini miripuko au kumulikwa mwili mzima kabla ya kupanda ndege.
Hatua nyingine zilizoimarishwa za usalama ni kwa wasafiri wote kutoka ama kupitia nchi 14, zinazodaiwa na Marekani kuwa na uhusiano na magaidi, wanalazimika kukaguliwa kwa kutumia mashine ya kumulika mwili mzima.
Sheria hiyo mpya inafuatia jaribio lililofanywa wakati wa Krismas la kulipua ndege ya Marekani, ambalo linadaiwa kufanywa na kijana wa Kinigeria, ambaye Marekani inaamini kuwa amepewa mafunzo na mtandao wa Al Qaeda nchini Yemen.

Iran yaanza kujadiliwa

Washngton:
Marekani na nchi rafiki zake kidiplomasia, zimeanza kujadili vikwazo vipya dhidi ya Iran.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hilary Clinton, amesema madhumuni ya hatua hiyo ni kuishinikiza serikali ya Iran, bila ya kuweka ugumu wa maisha kwa wananchi wa kawaida wa Iran.
Wakati huohuo, ziara iliyokuwa imepangwa na ujumbe wa wabunge wa Umoja wa Ulaya kuitembelea Iran, imezuiwa na serikali ya nchi hiyo, bila ya kutarajiwa.
Shirika la Habari la Iran, limesema ziara hiyo imeahirishwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya nchi hiyo ili kupisha muda zaidi, wa kujiandaa na ziara hiyo.
Lakini hata hivyo, kiongozi wa ujumbe huo Barbara Lochbihler, amesema ziara hiyo iliahirishwa baada ya hatua ya Iran kuzuia mkutano uliopangwa kufanyika kati ya Wabunge wa Umoja wa Ulaya na viongozi wa upinzani wa nchi hiyo.

Hispania yaikoromea Cuba

Madrid:
Hispania ambayo sasa inashikilia kiti cha Urais wa Umoja wa Ulaya, imeitaka Cuba kutoa maelezo kwa nini imemkatalia mjumbe wa Bunge la Umoja wa Ulaya, kuingia nchini humo, siku ya Jumapili.
Serikali ya Cuba ilimkatalia kuingia nchini humo Luis Yanez, baada ya mwanachama huyo wa Kisosholisti wa Bunge la Umoja wa Ulaya, kuwasili na mke wake Carmen Hermosin (pichani), ambao walikuwa wakienda kwa mapumziko.
Hata hivyo, duru za serikali zililiarifu Shirika la Habari la Uingereza kwamba serikali ya Cuba haikutoa maelezo kwanini ilimkatalia mbunge huyo, kuingia nchini humo, ambaye awali alisema kuwa hakuwa na ajenda za kisiasa.

Rompuy atangaza uchumi kuwa mada kuu ya mkutano ujao wa Umoja wa Ulaya.

Brussels:
Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy ametangaza kuwa, Uchumi utakuwa mada kuu katika mkutano ujao wa baraza la umoja huo, utakaofanyika Februari 11.
Herman Van Rompuy ambaye ni Rais wa kwanza wa kudumu wa Umoja huo, ameyasema hayo katika siku yake ya kwanza ofisini.
Amesema umoja huo unahitaji kuhakikisha ukuaji wa uchumi barani Ulaya.
Hispania, nchi ambayo tangu januari mosi inashika nafasi ya Urais wa Umoja wa Ulaya, kwa kipindi cha miezi sita, imeeleza pia kuupa kipaumbe uchumi katika kipindi cha uongozi wake kwenye umoja huo unaojumuisha nchi 27 za Ulaya.

Urusi yaanza kupeleka mafuta Belarus.

Moscow:
Naibu Waziri Mkuu wa Urusi Igor Sechin ametangaza kwamba nchi yake imeanza kupeleka tena mafuta kwenda Belarus, baada ya kusitisha Januari mosi.
Amesema mafuta yalianza kutiririka siku ya Jumapili na kwamba usambazaji katika nchi za Ulaya magharibi haukuathirika.
Urusi na Belarus zimekuwa zikibishana juu ya bei ya mafuta na pia gharama za upitishaji kwa mwaka 2010.
Mabishano hayo yalisababisha kupanda kwa bei ya mafuta kwa zaidi ya dola 80 kwa pipa siku ya Jumatatu.

Karzai ataka baraza la mawaziri kuidhinishwa haraka.

Kabul
Rais Hamid Karzai ameahirisha mapumziko ya bunge la nchi hiyo katika kipindi hiki cha majira ya baridi, mpaka pale wabunge watakapowasilisha majina ya mawaziri wapya kuchukua nafasi ya yale yaliyokataliwa siku ya Jumamosi.
Rais Karzai amesema bunge la taifa la nchi hiyo linaweza kuchukua likizo, mara tu baada ya baraza hilo la mawaziri kuidhinishwa.
Ni majina saba tu ya mawaziri, kati ya 24, yaliyowasilishwa na Rais Karzai ndio yaliyokubaliwa.
Majina hayo mapya ya mawaziri 17 yanatarajiwa kuwasilishwa katika siku chache zijazo.

Newer Posts Older Posts