LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

01/08/10

ROSE MHANDO AMSUBIRI BWANA AMPE MUME WA KUFANANA NAYE



Mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili Rose Mhando amedai kuwa, kwa sasa anamsubiri Mungu ampe mume wa kufanana naye ili asije akawa kikwako katika huduma yake na kumfanya arudi nyuma kwenye anga za muziki huo na kuwa karibu na Mola wake.
Akiongea na mtandao huu hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Rose alisema kuwa, kutokana na umaarufu alionao kila pembe ya dunia, kila mwanaume anapenda amuoe kwa kuahidi kuendelea kuiheshimu huduma yake, lakini anaamini Mungu bado hajampa wa kufanana naye na siku ikifika ataliweka wazi kila mtu ajue kwani ndoa ni baraka.
Mkali huyo wa muziki wa Injili nchini, alitumia nafasi hiyo kukanusha kwamba, yeye hajihusishi na tabia ya kutoka na vijana wadogo na kufanya nao mapenzi kama baadhi ya watu wanavyodai.
Rose mwenye watoto watatu wenye watoto tofauti, alisema kuwa kwa sasa hana mpango wa kujishughulisha na masuala ya wanaume na amejikita zaidi katika kumtumikia Mungu wake.

JONAS PAPA LUTUMBA

Mwimbaji huyo wa muziki wa Injili anayekwenda kwa jina la Jonas Papa Lutumba kwa sasa anaimba na kuhubiri neno la Mungu katika kanisa linaloongwa na mkewe maeno ya Tabata Mawenzi.

MAKOMA WAMEPOTELEA WAPI?


PICHA HII NI KWA HISANI YA MTANDAO WA anniemakoma.skyrock.com

Witness Mallya: Tusiimbe kwa kushindana



Ni siku nyingine imempendeza Mungu tukutane katika safu hii ya tukiwa katika Mwaka Mpya wa 2010. Tuna kila sababu za kumrudishia heshima na utukufu Muumba wetu kwa kutuvusha salama mwaka 2009 ambao ulikuwa na majaribu ya hapa na pale, kwani kuna baadhi ya watu walifanikiwa kutimiza malengo waliyojiwekea na wengine kutokana ba sababu tofauti walishindwa kuyatimiza. Hilo lisikutie shaka, pengine mwaka huo haukuwa wako na wewe umepangiwa kufanikiwa mwaka huu.
Kikubwa nasema kuwa, shukuru kwa kila jambo na Mungu atakisikia kilio chako. Ikiwa leo ni siku ya kwanza ya mwezi huu wa kwanza tunaianza safu hii kwa muimbaji Witness Joseph Mallya mzaliwa wa Kilimanjaro lakini sasa masikani yake yapo jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kukutana na mtumishi huyu wa Mungu, swali langu la kwanza nilitaka kujua, ni kwanini leo hii baadhi ya waimbaji wa muziki wa Injili wamekuwa wakiimba kwa mashindano kama wafanyavyo watu wa mataifa? Licha ya uchanga wake katika huduma hii ya kuimbaji wa nyimbo za Injili, Witness alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa, kufanya hivyo ni kumkosea Mungu ambaye hapendi neno lake lishindanishwe.
“Tusiimbe kwa kushindana kama wanamuziki wa mataifa, kwani Neno la Mungu huwa halishindanishwi na wala Mola hapendi tufanye hivyo. Nimezunguka kwenye matamasha mengi ya muziki wa Injili hasa kwenye uzinduzi ambapo waimbaji wengi wa muziki huo hualikwa kwa ajili ya kuimba kabla ama baada ya muhusika kupanda jukwaani.
“Kufika kwangu kwenye matamasha hayo nimejifunza mambo mengi sana likiwemo hili la waimbaji kutegeana kupanda jukwaani na baadhi yao huwaambia hata wasema chochote (MC) kuwapanga wa mwisho baada kuimba wengine ili watakapopanda waimbe kwa kujituma na kuwashawishi watu kuwashangilia ili waonekane wameimba vizuri kuliko wengine,” anafafanua muimbaji huyo.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo ameeleza kwamba jambo hili limekuwa likijitokeza katika baadhi ya makanisa na kuifanya kazi hiyo kuwa ya ushindani tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo watu walikuwa wakiimba kwa ajili ya huduma.
 “Jambo hili lipo pia makanisani hasa kwenye kanisa lenye kwaya zaidi ya moja. Utakuta waimbaji wanapopewa nafasi ya kuimba hucheza stepu kwa kujituma ili waonekane wao ni zaidi ya wenzao, na baada ya ibada hukaa na kuanza kusema wamewafunika wenzao na wao ni wazuri zaidi.
“Hali hiyo mesababisha kuibuka kwa matabaka ya waimbaji makanisani na nje ya makanisa. Bila woga utasikia  muimbaji anasema ooh! wale hawatuwezi, sisi ni zaidi yao, unaona tulivyowafunika, siku nyingine hawatakubali kupanda jukwaa moja na sisi. Hii siyo sawa na huchangia  waimbaji kuogopana jambo ambalo ni kinyume na malengo  ya Injili,” anasema Witness.
Hata hivyo, Witness anafafanua kwamba kitendo cha waimbaji wa Injili kuimba kwa kushindana kumesababisha kutunga nyimbo zisizo na upako wa Mungu ambazo huwa na utamu kama pipi ambayo hupoteza utamu wake kwa muda mfupi.
“Kutokana na hali hiyo,waimbaji wengi wamejikuta wakiimba bila utukufu wa Mungu, bali wao kama wao ndiyo maana nyimbo zao huwa zinaburudisha tu watu ila hazina uponyaji ndani yake,” anasema Witness.
Kadhalika aliongeza kuwa endapo waimbaji hao wangekuwa wanaimba katika Roho na kweli na kumtanguliza Mungu wao kabla ya uimbaji, lisingekuwa jambo la kushangaza kuona watu wanapokea uponyaji pindi wanapokuwa kwenye matamasha ya uzinduzi wa albamu za nyimbo za Injili, ama kwenye makongamano.
Akizungumzia huduma yake, Witness alisema kuwa, kwa sasa yupo studio anamalizia albamu yake yenye nyimbo nane na tayari nyimbo tatu zipo mtaani  kupitia vituo vya redio kote nchini. Albamu hiyo inakwenda kwa jina la Niite Bwana.
Amezitaja baadhi ya nyimbo zilizopo mtaani hivi sasa kuwa ni pamoja na Niite Bwana, Sifa zako zivume na Tunamtazamia nani? Huku akitarajia kutoka na nyimbo nyingine tano siku chache zijazo.
Nyimbo zinazounda albamu hiyo ni pamoja na Mbona unachelewa sana, Niite Bwana, Sifa zako zivume, Usinitenge, Tunamtazamia nani?, Anatupenda, Nitoe Hivi nilivyo na Nakuulize Mungu.
Witness alimaliza kwa kuwataka waimbaji wenzake kuachana na tabia ya kuimba kwa mashindano badala yake waimbe nyimbo zao katika Roho na kweli ili kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali kwa maana wao ni watumishi kamili wa Mungu, na nyimbo zao zinanafasi kubwa ya kuwaponya watu ama kuibadili jamii kuondokana na tabia chafu kuliko kuimba nyimbo za kusisimua mwili pekee.



MWAMPULULE: Mtandao wa biashara umeharibu huduma ya uimbaji




Leo ni siku ya nane ya mwezi huu wa kwanza na kwenye safu hii tunaye  muimbaji wa muziki wa Injili nchini anayekwenda kwa jina la Emmanuel Mwampulule mzaliwa wa Mbeya lakini sasa masikani yake yapo jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukutana na muimbaji huyo mwenye nyimbo zenye mguso wa ajabu, alionekana kuwa na uchungu juu ya waimbaji wa muziki huyo ambao wameugeuza muziki huo kuwa biashara ya kuwaingizia kipato cha kila siku na kusahau wito walioitiwa na Mungu wao.
Mwampulule anasema kuwa, kitendo cha baadhi ya waimbaji kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kwenda kuhudumia katika mikutano ya dini, semina, makongamano na makanisani kumeonesha wazi kwamba, watumishi hao wa Mungu wamekuwa wafanya biashara  licha ya kupinga mara kwa mara kauli hiyo ambayo imekuwa ikitolewa na wadau wa muziki huo hapa nchini.
Muimbaji huyo anayeabudu katika kanisa la Mito ya Baraka jijini Dar es Salaam alisema kuwa, waimbaji hasa wenye majina makubwa, baada ya kuinuliwa ili wamtumikie vema Mungu wao kwa njia ya uimbaji na kuwarejesha kundini kondoo waliopotea, wamekuwa wakijiona wao ni bora kuliko wengine na ndiyo maana wamekuwa wakiomba dau kubwa pindi wanapoitwa kwenda kuimba sehemu walikoalikwa.
“Sikatai kwamba, mtumishi anastahili kula kutoka madhabahuni kwake, lakini isiwe kama hawa wenzetu wanavyofanya pindi wakialikwa kwenda kutoa huduma ya uimbaji sehemu, ambapo  hudai pesa nyingi bila kuangalia kwamba kuinuliwa kwake na Mungu ni njia mojawapo ya kuwarejesha kundini kondoo waliopotea kwa njia ya uimbaji.”
Aliendelea kusema kuwa, muimbaji aliyeinuliwa na Mungu na jina lake kuvuma kila pembe ya nchi na hata duniani kwa ujumla, pindi anapoenda sehemu kuimba, watu wengi hukusanyika kwa ajili ya  kumuangalia jinsi anavyoimba na baadhi yao kuamua kuachana na matendo maovu na kuokoka.  Lakini kama ukishindwa kwenda sehemu alikoalikwa, ni dhahiri kwamba watu hao watabaki kama walivyo.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Mwampulule alisema kuwa, kitendo cha soko la muziki wa Injili kuonekana kuwa juu kuliko miziki mingine kwa sasa, kumepelekea waimbaji kuinua mabega na kuona kuwa, muda huu ndiyo wa wao kufaidika na upepo huo ambao haujulikani unaweza kuchukua kipindi gani.
Mwampulule aliendelea kudokeza kuwa, waimbaji wote ambao Mungu amewainua na majina yao kufahamika kwa kila rika, watambue kwamba, yeye aliyewainua ana uwezo wa kuwashusha pia akainua wengine ambao watatumika katika roho na kweli bila kuangalia maslahi.
Mtumishi huyo wa Mungu tayari ana albamu yake mkononi aliyoipa jina la Maisha Bila Yesu Utaishije? yenye vibao tisa ambavyo ni Amani utaipata wapi, Amen Haleluya, Kiburi cha uzima, Nani kama Yesu, Akabhalilo (wa kilugha) wenye maana ya Nyakati, Neema na Baraka, Mito ya baraka na Maisha Bila Yesu Utaishije? ambao umebeba albamu hiyo.
Huduma ya uimbaji aliianza mwaka 1998 akiwa kama mwalimu wa  kwaya ya Yerusalemu ya mkoani Mbeya, iliyokuwa chini ya kanisa la Pentekoste. Mwaka 2000 alianza rasmi zoezi la kurekodi albamu yake binafsi na ilikamilika mwaka 2004 na kuiita Maisha Bila Yesu Utaishije?
Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo katika mchakato ya kufyatua albamu  ya pili, alimaliza kwa kuwataka waimbaji wa muziki wa Injili kuachana na tabia ya kuendekeza suala la pesa pindi wanapoalikwa kwenda kutoa huduma kwenye makanisa na mikutano ya dini ama kazi zinazohusiana na mambo ya kiroho. Bali watu watakaowaalika nao watakuwa wanatambua kuwa ni kiasi gani ambacho wangependa kuwalipa watumishi hao ili kuendelea na shughuli zao za kihuduma.
Nakukumbusha pia kuwa albamu ya muziki wa Injili  inayokwenda kwa jina la Ushindi ya Kabula J.George sasa ipo madukani nchi nzima. Albamu hiyo imefanyika baraka kubwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali na waliofungwa na nguvu za giza, na sasa wako huru wakimtukuza Mungu. Kwa wanunuaji wa jumla na rejareja wasiliana na msambazaji kwa simu namba 0713328290.



Newer Posts Older Posts