LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

01/11/10

Mtikila arudishwa rumande


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana (Jumatatu) ilimfutia dhamana Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na kumrudisha rumande baada ya mwanasiasa huyo kukiuka masharti ya dhamana yake.
Mtikila anayekabiliwa na tuhuma za kumwita Rais Jakaya Kikwete gaidi, alitiwa nguvuni na polisi baada ya Hakimu Mkazi Elirehema Lema kudai mchungaji huyo kushindwa kufika mahakamani hapo kwa muda muafaka.
Kwa mujibu wa hakimu huyo,ni mara ya pili sasa Mtikila kuchelewa mahakamani hapo bila kutoa taarifa zozote kwa wadhamini wake kama masharti ya dhamana yanavyoelekeza.
Hata hivyo, Mtikila alidai mahakamani kuwa, alikuwa anaumwa na kuongeza kwamba, taarifa za kuumwa kwake alimpatia Wakili wake ambaye naye alidai mwanawe anaumwa na hivyo mahakama kushindwa kupata taarifa zake.
“Ni mara ya pili sasa umekuwa ukirudia kosa hili bila kutoa taarifa zozote kwa wadhamini wako hivyo ninakufutia dhamana utarudi rumande hadi Januari 25, mwaka huu kesi yako itakapoletwa kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya awali,” alihitimisha Hakimu Lema.
Januari 4, mwaka jana, mtuhumiwa hakufika mahakamani hapo ambapo upande wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kutoa kibali cha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kutokana na kutofika kusikiliza kesi inayomkabili bila kutoa taarifa yoyote wala maombi ya kumfanya ashindwe kufika mahakamani.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Victoria Nongwa hakutoa kibali cha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo licha ya kuombwa na upande wa mashitaka.
Januari 6, mwaka jana, Mtikila aliwasilisha barua ya kuiomba msamaha mahakama hiyo, akieleza kuwa alikuwa akimhangaikia ndugu yake ambaye amepooza na kudai kuwa aliwatuma wadhamini wake kutoa taarifa hiyo lakini hawakufanya hivyo.
Inadaiwa kuwa,Oktoba 21, 2007, maeneo ya Ilala katika Shirika la Nyumba (NHC) la Taifa, Mtikila alitoa maneno ya dharau na kujenga chuki dhidi ya Serikali ya Rais Kikwete.
Katika shitaka la pili, Mtikila anadaiwa kutoa lugha ya uchochezi akidai: “Ahadi zote za Rais Jakaya Kikwete siku zote zinaongozwa na imani yake ya dini tena kutekeleza malengo yake ya kusilimisha nchi”
Mtikila alikana mashitaka hayo na alikuwa nje kwa dhamana.

SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 46 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUFANYIKA LEO NZANZIBAR


Leo ni sherehe ya  kutimiza miaka 46 ya  Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika tarehe 12 January 1964. Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Amani Abeid Karume atakagua gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya maadhimisho hayo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo


Israel kujenga uzio katika mpaka wake na Ulaya.



Israel imeidhinisha mipango yake ya kujenga vizuizi katika mpaka wake na Misri.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu (pichani), amesema uzio huo unakusudia kuwakinga na wapiganaji pamoja na wahamiaji haramu. Hata hivyo, amesema Israel inaendelea kuwapokea wakipimbizi kutoka maeneo yanayokabiliwa na vita.
Polisi nchini Israel inakadiria kuwa wafanyakazi wahamiaji wapatao 200, wakimbizi na wahalifu wanavuka mpaka kinyume na sheria na kuingia nchini humo kila wiki kupitia mpaka wake na Misri.
Israel pia inajenga uzio ambao umesababisha utata katika eneo la Ukingo wa magharibi, kwa madai ya kuwazuia watu wanaotumia mabomu ya kujitolea mhanga kuingia katika miji yao. Wapalestina wamelalamikia kujengwa kwa uzio huo kwa kusema kwamba unachukua sehemu ya ardhi yao.

Israel kujenga uzio katika mpaka wake na Ulaya.


Tel Aviv: 


Israel imeidhinisha mipango yake ya kujenga vizuizi katika mpaka wake na Misri.

Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu (pichani), amesema uzio huo unakusudia kuwakinga na wapiganaji pamoja na wahamiaji haramu. Hata hivyo, amesema Israel inaendelea kuwapokea wakipimbizi kutoka maeneo yanayokabiliwa na vita.
Polisi nchini Israel inakadiria kuwa wafanyakazi wahamiaji wapatao 200, wakimbizi na wahalifu wanavuka mpaka kinyume na sheria na kuingia nchini humo kila wiki kupitia mpaka wake na Misri.
Israel pia inajenga uzio ambao umesababisha utata katika eneo la Ukingo wa magharibi, kwa madai ya kuwazuia watu wanaotumia mabomu ya kujitolea mhanga kuingia katika miji yao. Wapalestina wamelalamikia kujengwa kwa uzio huo kwa kusema kwamba unachukua sehemu ya ardhi yao.


RATIBA YA HUDUMA KANISANI


Kanisa la Pentecostal Holiness Mission (PHM) Lighthouse Christian Center Ubungo, linakukaribisha katika ibaada zake ambazo hufanyika hapo kama ifuatavyo:


Jumapili saa 1-3 Ibaada ya Kiingereza
3- 6:30 Ibaada Kuu, Mafundisho na maombi.
Jumatatu saa 10:00 – 12:00, Ijue kweli ya neon
Ijumaa sa 10 :00 – 12:00, Maombi na maombezi
Jumanne na Alhamis saa 10 asubuhi hadi 10:00 jioni, Ushauri kwa kila mtu.
Kanisa lipo chini ya askofu Rejoice Ndalima, jinsi ya kufika, fuata kibao mkabala na njia panda ya Chuo kikuu, utaona kibao kimeandikwa Pentecostal Holiness Mission (PHM) Lighthouse Christian Center.

Newer Posts Older Posts