LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

01/14/10

Marekani na Ufaransa waitisha mkutano kuhusu Haiti





Mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince unavyoonekana sasa ukiwa umeharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea siku ya Jumanne.
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince unavyoonekana sasa ukiwa umeharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea siku ya Jumanne.
Mbali na kuitishwa kwa mkutano huo wa kimataifa, Marekani imetoa kiasi dola milioni 100 kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Haiti.
Rais Barack Obama wa Marekani na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa wameitisha mkutano wa kimataifa kuhusu Haiti kufuatia nchi hiyo kukumbwa na tetemeko la ardhi siku ya Jumanne.
Rais Sarkozy pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa Brazil, Lula Inacio da Silva na Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper. Rais huyo wa Ufaransa amesema nchi yake itashirikiana kwa karibu na washirika wake wa Umoja wa Ulaya na pia atafanya ziara Haiti kwa ajili ya kukutana na rais wa nchi hiyo, Rene Preval.
Wakati huo huo, Rais Obama ametangaza kuwa Marekani itatoa msaada wa awali wa dola milioni 100 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Haiti na kwamba juhudi za uokozi za Marekani zinaendelea kupangwa haraka iwezekanavyo.
Kiasi watu 50,000 wanahofiwa kufa kutokana na tetemeko hilo la ardhi na watu wengine wanaokadiriwa kufikia milioni tatu wanahitaji msaada wa dharura.
Wakati huo huo, wananchi wa Haiti wameanza kushikwa na hasira kutokana na kuona kuwa misaada inachelewa kuwafikia. Katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince, waandamanaji walizuia barabara kwa kuweka maiti kati kati huku wakitaka kupatiwa haraka misaada ya dharura.
Ukiwa ni usiku wa tatu tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi nchini humo, chakula na maji bado havipatikani kwa urahisi. Watu wengi bado wamefunikwa na vifusi vya majengo yaliyodondoka. Wafanyakazi wa mashirika ya misaada wameonya kuwa idadi ya vifo inaweza ikaongezeka haraka kama watu waliojeruhiwa hawatapatiwa msaada wa haraka katika siku chache zijazo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema kuwa maafisa 3,000 wa umoja huo wanafanya doria katika mitaa mbalimbali kwa hofu kuwa hasira hiyo inaweza ikasababisha ghasia, kama misaada ya kimataifa haitafika haraka.

MAGOKE: Ufisadi umeingia kwa watangazaji wa radio,Tv za dini


Leo nimefanikiwa kukutana na ndugu yangu Magoke Junio, wakazi wa mkoa wa Shinyanga kumuita Alpha Magoke kutokana na jina hilo kulitumia wakati akiwa shuleni hasa shule ya mzisingi.
Muimbaji huyu kwa namna moja ama nyingine ameoneka kukerwa na kile alichokiita ufisadi kwa baadhi ya watangazaji wa radio na Tv za dini, kutokana na kucheza nyimbo za watu wenye majina makubwa kwa lengo la kujipatia kipato kutoka kwa wahusika.
Magoke ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Shinyanga alisema kuwa, leo hii ukifika studio za vyambo hivyo vya habari utakuta CD nyingi za waimbaji zimewekwa kabatini pasipo kuchezwa huku ukisiliza nyimbo za waimbaji waliotofa fedha zikichezwa kila kukicha tena zikipambwa kwa sifa ambazo wakati mwingine mhusika anakuwa hana.
“Ninakila sababu za kusema kuwa, ufisadi umeingia kwa watangazaji wa radio,Tv za dini kw sababu leo hii ukipeleka kazi yako studio unatakiwa ulipie kwanza shilingi laki 3 ama zaidi ili kazi yako ipigwe mara kwa mara, na usipofanya hivyo, Cd yako inazikwa”.
“Ninaushahidi wa kutosha juu ya jambo hili, si kwamba waimbaji wenye majina tulionao sasa ni hao tu, bali kunawengine nyimbo zao ni kali kuliko hizo zinazosikika zenye ujumbe mzito lakini kwa kuwa wao hawana pesa ya kuwapa watangazaji hao, ndiyo maana hawasikiki”.
Magoke aliendelea kusema kuwa, wakati mwingine baadhi ya waimbaji walioinuliwa huwa wanakampeni ya kuwachombeza watangazaji hao kutopiga nyimbo za waimbaji hasa ambao huonekana kuwa tishio pindi wanaposimama nao jukwaani kutokana na jumbe zao kuwa nzuri na zenye upako wa ajabu.
Alitoa mfano mmoja kuwa, katikati ya mwaka jana, kuna tamasha la uimbaji liliandaliwa mkoani Mwanza ambalo liliwashirikisha baadhi ya wakali wa muziki wa Injili kutoka jijini Dar es Salaam, wakati wa kuimba walitangulia wakongwe ndipo akapanda jukwaani mwanadada naye kutoka Dar ambaye jina lake siku kubwa sana, alionekana kuvuta hisia za watu waliohudhuria tamasha hilo.
“Kuna tamasha la waimbaji lilifanyika mkoani Mwanza katikati ya mwaka jana, waimbaji wakonge walipewa nafasi za kwanza kuimba na watu waliwashangili kutokana na kuwafahamu majina yao, lakini alisimama mwanadada mmoja na kuimba wimbo uliovuta hisia kali kwa mashabiki wa muziki huo, na alijikuta anatunza fedha nyingi kuliko wakongwe,” alisema Magoke.
Kitendo hicho kinadhihirisha kwamba ni kweli kuna waimbaji ambao wanagandamizwa na watangazaji wa vituo hivyo, lakini wakipewa nafasi wanaweza kufanya maajabu na kuponya mioyo ya watu ambao inahitaji kuhubiriwa kwa njia ya uimbaji.
Magoke amewataka watangazaji wanaojishughulisha na vitendo hivyo kuacha mara moja, kitendo cha kukaa kwenye studio hizo ni sawa na kuwa madhabahuni, hivyo suala la kukubali kupokea hongo kama kichocheo cha kupiga nyimbo linahitaji kuachwa ili kuponya roho zao.
“Nawasihi kuachana na tabia hiyo, kwani uwepo wao katika studio hizo ni sawa na kwamba wapo madhabahuni, hivyo kuchanga masuala ya kuchukua rushwa ili wacheze nyimbo za waimbaji wachanga waache ili kuokoa roho zao, suala la muimbaji kuwapa asante ya kucheza kazi yao linaweza kutolewa na wahusika bila kujenga mazingira ya rushwa,” alisema Magoke.
Jitihada za kuwapata baadi ya watangazaji wa radio na Tv za dini zinaendela, endalea kuwa nami katika safu hii.
Mtumishi huyo wa Mungu tayari anayo albamu yake moja yenye vibao tisa ambavyo ni Mwamba uliobeba jina la albamu, Rudi, Mungu nakushukuru, Hubiri, Niko kwako, Tafuteni, Faster faster, Kanisa na Mama.
Nyimbo za Makonge zipo katika miondoko mchanganyiko, kama vile miondoko ya muziki wa kizazi kipya kwa lengo la kuwapata vijana wengi, zuku na mingine mengi.

Israel yaomba radhii Uturuki.

Istanbul.
Uturuki imesema kuwa imekubali kuombwa radhi na Isreal baada ya nchi hiyo kutishia kumrejesha balozi wake kutokana na mzozo wa kidiplomasia mapema wiki hii. Naibu waziri wa mambo ya kigeni, Danny Ayalon amemkaripia balozi wa Uturuki nchini Israel, Oguz Celikkol, na kukataa kushikana nae mkono mbele ya kamera za televisheni, akilalamika kuhusiana na kipindi cha televisheni nchini Uturuki ambacho kimewaonyesha wakala wa idara ya ujasusi nchini Israel, Mossad, kama wanaoteka nyara watoto. Ayalon ameandika barua ya kuomba radhi pamoja na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Netanyahu pia amewataka maafisa wa nchi hiyo kutafuta njia za kuzuwia tukio kama hilo kutotokea tena hapo siku zijazo.

Misaada yaanza kuwasili Haiti



Misaada hiyo ni kwa ajili ya kuwasaidia kaisi watu milioni tatu wanaohitaji msaada wa dharura.

Serikali kadhaa duniani pamoja na mashirika ya misaada yameendelea kupeleka misaada ya kibinaadam nchini Haiti baada ya nchi hiyo kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi siku ya Jumanne linalohofiwa kusababisha vifo vya mamia ya maelfu ya watu. Marekani kwa upande wake jana imeanzisha operesheni ya misaada ya kijeshi na kiraia kwa ajili ya Haiti, wakati wasaidizi wawili wa ngazi ya juu wa Rais Barack Obama wakiwa wameahirisha safari zao nje ya nchi kwa ajili ya kulizingatia zaidi janga hilo. Rais Obama alisema amewaamuru wasaidizi wake kulishughulikia haraka suala hili kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wa Haiti.
''Watu wa Haiti watapata msaada wote wa Marekani katika jitihada za dharura za kuwaokoa watu waliokwama chini ya vifusi na kupeleka msaada wa kibinaadam, ikiwemo vyakula, maji na madawa, ambavyo watu wa Haiti watahitaji katika siku zijazo, alisema Rais Obama.'' Kikosi cha jeshi la Marekani kitakachokuwa na kazi ya kuokoa watu waliosalimika na kujaribu kutathmini hasara iliyopatikana kutokana na tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa kipimo cha saba katika kipimo cha Richter, kimewasili nchini Haiti. Kamisheni ya Umoja wa Ulaya imesema itatoa Euro milioni tatu kwa ajili ya misaada ya dharura. Mataifa mengine pia ya Umoja wa Ulaya, yakiwemo Uingereza, Italia, Ufaransa na Uhispania, yametuma vifaa vya uokoaji pamoja na misaada.
Wito kwa jumuiya ya kimataifa
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, ambaye kwa sasa ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, ameitaka jumuiya ya kimataifa kutoa misaada ya fedha. Bwana Clinton amesema maji, chakula, malazi na madawa vinahitajika haraka kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Haiti, hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Port-au-Prince. Rais huyo wa zamani anataka kuokoa maisha ya watu wengi iwezekanavyo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema hali ni ya kutisha na kutoa wito wa kutolewa misaada zaidi. Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa umetoa dola milioni 10 kwa jili ya kugharamia kulishughulikia janga hilo. Maafisa wa Umoja wa Mataifa mjini New York wamethibitisha kuwa wanajeshi 16 wa kikosi cha kulinda usalama cha umoja huo wamekufa kutokana na tetemeko hilo la ardhi. Aidha, inadaiwa kuwa mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, Hedi Annabi, hajulikani alipo.
Japan nayo kutoa msaada
Wakati huo huo, serikali ya Japan leo imeahidi kutoa msaada wa dharura wa dola milioni tano kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa Haiti. Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Japan imesema kuwa nchi hiyo imepanga kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa, likiwemo lile la kuwahudumia watoto-UNICEF- na la Mpango wa Chakula Duniani-WFP- katika kugawa misaada hiyo. Mbali na mashirika ya misaada na serikali kutoa misaada, watu maarufu duniani, wakiwemo wanamuziki, wameanzisha kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Haiti. Mwanamuziki wa hip-hop wa Marekani, Wyclef Jean, ambaye ni mzaliwa wa Haiti, anaongoza kampeni hiyo. Mcheza sinema, Angelina Jolie, na mpenzi wake, Brad Pitt, wamechangia dola milioni moja kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Haiti. Tetemeko hilo la Jumanne lililowaacha watu milioni tatu wakiwa wanahitaji msaada wa haraka ni baya na kubwa kabisa kuwahi kuikumba Haiti, moja ya nchi masikini sana duniani katika muda wa karne mbili.
  • Habari hii imeandikwa na mwandishi: Grace Patricia Kabogo (AFPE,DPAE) na kuhaririwa na Miraji Othman wa radio Deutsche Welle ya Ujerumani.

Newer Posts Older Posts