LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

03/11/10

UCHUMBA HADI NDOA


Hapana shaka msomaji wa blog hii haujambo na tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuiona tena siku ya leo. Siku za hivi karibuni wasomaji wengi wameomba niwe natoa masomo ya ndoa pamoja na uchumba hadi ndoa. Nafuhi kuwa kwa saada wa Mungu leo naanza kutoa somo hili ambalo watu wengi sana wanalipenda hasa kwa wanafunzi wa shuleni na vyuoni.(Picha hii ni kwa hisani ya blog ya spotstarehe)
Naanza kwa kusema kuwa eneo hili ndilo eneo ngumu kuliko kuliko pengine unavyofikiria. Hatua ya uchumba ndiyo huwa safari ya kuelekea kwenye hatua ya kutengeneza familia yako ama kizazi chako, hivyo unahitajika umakini mkubwa katika kipindi hiki.
Pengine tuanze na kueleza maana ya neno uchumba. Uchumba ni hatua ya kijana/mwanaume kuposa ama msichana/mwanamke kuposwa. Kwa namna moja ama nyingine naweza kusema kuwa, uchumba unaanzia pale msichana anapomtambulisha mchumba wake kwa wazazi au mwanaume anapomvisha msichana pete ya uchumba au vyote kwa pamoja.
Safari ya uchumba huanza mara moja mara baada ya jinsia mbili zikikutana hapa namaanisha wakikutana msichana na mvulana ama mwanaume na mwanamke. Na mara nyingi wahusika huanza kwa kuitana kaka na dada huku ndani ya nafsi zao kukiwa na kitu cha ziada.
Baada ya kupita katika hali hiyo kinachofuata ni suala la matamanio yanaanza hasa kwa mwanaume. Hutamani kukutana na binti huyo ili amweleze juu ya hisia zake, na mara nyingi huanzia mbali ili kukwepa mwanamke asije akashtuka na kumtosa kwa madai ya kuomuona kama hajaokoka ama si mtu mwema.
Mwanaume/mwanamke huanza kufanya mambo ambayo yatamfanya mlengwa kuwa karibu naye kwa kutoa lugha nzuri ambayo siku atakapoingiza hitaji lake iwe rahisi kukubalika tofauti na kuanza kwa kukurupuka.
Kipindi hiki ndiyo huwa ni kigumu na kinaweza kuleta majuto yenye uchungu mzito maishani mwa mlengwa kutokana na kile ambacho hakutarajia kama kingetokea katika siku za usoni.
Ndoa nyingi zimejikuta zikiingia katika majuto yasiyo na kikomo kutokana na kukosea katika suala la uchumba. Baadhi ya wachumba hujikuta wanaingia katika uchumba kutokana na matamanio ya mwili. Mwanamke/mwanaume anaweza kumpenda mwanzake kutokana na uzuri wa sura wakati mwingine tabia nzuri aliyonayo bila kumruhusu Roho Mtakatifu kumwonyesha aliyewake.
Nawengi wameingia katika uchumba usio na makusudi ya Mungu kutokana na msukumo wa kuoa ama kuolewa. Kutokana na hali hiyo, wahusika wamejikuta wakiwa katika ndoa za majuto na leo hii wanatamani kuachika.

Somo hili litaendea…. Toa maoni yako kuhusiana na somo hili.

ROSE MUHANDO APASUA NDOA YA MTU



Msanii nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando ‘anabeba’ mzigo wa lawama kufuatia kuwepo kwa mpasuko ndani ya ndoa ya Promota maarufu wa muziki huo nchini, Alex Msama na mtangazaji wa Kituo cha Redio cha WAPO FM, Laura Bonaventure.
Chanzo cha habari hii kimepasha kuwa, ndoa hiyo ina ‘masiku kibao’ sasa ‘inapumulia mashine’ huku Rose akitajwa tajwa kuhusika na mgogoro wake.
Chanzo hicho kikaendelea kuweka ‘nje’ siri kuwa, chanzo cha kuwepo kwa ufa katika ndoa hiyo ni kufuatia mke wa Msama, Laura kuchezwa na machale kuhusu ukaribu kati ya mumewe na Rose Muhando kiasi cha kukosa amani kama siyo furaha.
Habari zinazidi kumwagika kwamba, hali hiyo ikashamiri, ikanawiri, ikafika mahali hisia za mwanamke huyo zikawa wazi na hivyo kuanza ‘kumsomea’ mashitaka  mumewe akitaka maelezo kuhusu ukaribu huo.
Habari zaidi zinapasha kuwa, licha ya kujitetea bila ‘mwanasheria’, bado mke huyo akaweka ngumu kuelewa hali iliyosababisha kila mtu kuanza kuishi kivyake ndani ya nyumba.
“Hii hali ilifika mahali kila mmoja akawa kivyake ndani, Msama akashika hamsini zake, mkewe naye anakumbatia zilizobaki,” kilisema chanzo.
Kikaongeza: “Kubwa kuliko zote, kuna wakati Msama akipiga wimbo wowote wa Rose (Muhando), mkewe anazima redio au anapunguza sauti, moyo unamtuma kuwa, hisia zake zina ukweli.”
Habari zaidi zinasambaa kuwa, hata pale Msama anapokwenda Dodoma kwa shughuli za kikazi, mkewe hudhani ‘mista’ wake yupo ‘andapromisi’ na Rose hali ambayo imekuwa ikizidi kuvuruga ndoa hiyo.
Mambo yalipozidi kuwa mabaya, nyeti zinapasha, mke aliamua kuondoka nyumbani hapo na kwenda ‘kujichimbia’ sehemu  moja jijini Dar es Salaam (Risasi linahifadhi jina kwa sasa).

UTETEZI WA WADAIWA
Kufuatia madai haya, blgo hii ilipiga ‘jaramba’ mpaka ofisini kwa Msama, Msama Promotion, Block 41, Kinondoni jijini Dar na na kufanikiwa kuongea naye kwa kumpa ‘a e i o u’ ya ishu yake ambapo alipagawa kwa kuanza kutaka kujua ‘sosi’ wetu.
Alipokataliwa kutunza maadili, alisema mambo ya kifamilia yaachwe kwa wanafamilia, kwani ni jukumu lao kuweka sawa kwenye ‘korogesheni’ endapo mambo yataharibika.
“Mambo ya kifamilia yabaki kuwa hivyo, kama kuna tatizo linalomshirikisha Rose Muhando si kihivyo, hata wewe mkeo anaweza kukuuliza kuhusu mwanamke flani ukamwelewesha, akaelewa na mkaendelea na safari yenu ya maisha,” alisema Msama.
TGM: Kwa hiyo ni kweli?
Msama: Nimeshakupa jibu kaka, mimi kwangu ni amani tu, hakuna wasiwasi wowote ule.
Aidha, TGM ilikachanganya miguu kumsaka Laura, mke wa Msama lakini baadaye akapatika kwa njia ya simu ya kiganjani.
Kwa upande wake baada ya kupigwa ‘mashuti’ na TGM alisema nyumbani kwake hakuna tatizo na wala hana kinyongo na Rose kisha papo hapo akaiomba TGM imtwangie simu baada ya dakika tano, (eti) ana mgeni.
 TGM ilizifuata sekunde kwa macho angavu hadi zilipotimu dakika tano, alipopigiwa tena, cha ajabu, akawa anakata simu.
TGM halikuchoka, likamgeukia bingwa wa muziki wa Kwaito, Rose Muhando ambaye kwa ‘binafsi’ yake alisema tuhuma dhidi yake na Alex Msama ni maneno ya ‘wachovu’ wa kiimani, lakini akakiri kuwa karibu sana na Promota huyo kwa sababu za kikazi.
Alipobanwa sana kwamba kuna madai ya malalamiko ya Laura, Rose alisema anaapa kwa Mungu wake kwamba, hakuna ‘malavidavi’ kati yake na Msama na Laura kwake ni wifi yake kwa kuwa Msama kwake ni kama kaka yake ingawa si wa damu moja.

KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mwaka 2007, gazeti moja nchini liliwahi kuripoti kuwepo kwa uhusiano usiofaa kati ya Msama na Rose, wakati huo Promota huyo alikuwa kwenye vikao vya maandilizi ya harusi yake na Laura, lakini wenyewe waliruka ‘kimanga’.
   

Anna Clara Masala: Muziki wa Injili ni kazi ya Mungu, si umaarufu



Leo katika TGM nakuletea muimbaji wa muziki wa  Injili, Anna Masala ambaye ni miongoni mwa waimbaji wa muziki huo nchini Tanzania ambaye ameamua kuimba nyimbo za kumsifu Mungu tangu mwaka 1997 mara baada ya kupata nafasi ya kumpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake.
“Pamoja na ukweli huo lakini nikwambie jambo moja ambalo mimi ninaliona kuwa si sahihi nalo ni ushirikiano mdogo  na kukosekana upendo wa dhati miongoni mwetu sisi waimbaji wa muziki wa Injili,” anasema Anna.
Akizungumzia juu ya  mwanzo wa huduma yake, Anna  anasema kwamba  kazi ya uimbaji alianza kuifanya akiwa muimbaji wa kwaya ya kanisani alipokuwa anaabudu, (Tanzania Assemblies of God -TAG-Kinondoni) ambapo kupitia muziki huo, Mungu ameweza kumsimamia kwenye masuala mengi ya kimaendeleo.
Miongoni mwa mambo ambayo anaamini kuwa yametokana na matunda ya kufanya kazi ya kuhubiri Injili kwa njia ya nyimbo,  ni pamoja na kupata kazi za kucheza filamu tatu ambazo ni Hero of Church, Kiapo na Danger Zone jambo analoamini kuwa ni kutokana na rehema za Mungu tu.
 “Haya kwangu nayaona kuwa ni mafanikio makubwa, lakini haikuwa ni safari nyepesi kwa sababu nilikutana na vikwazo vingi katika maisha yangu, hii si mimi pekee bali waimbaji wengi hukabiliana na mambo haya.
“Pamoja na  hayo, pia muziki huu umekuwa ukitumika kwa ajili ya kubadilisha tabia na miondoko ya wanajamii na kumtangaza Mungu, lakini cha kushangaza wapo baadhi ya waimbaji hawapendani, jambo ambalo ni baya kwa mustakabali wa huduma hii,” anaongeza muimbaji huyo ambaye bado hajapata jina kubwa ikilingansihwa na waimbaji wengine waliopo juu hivi sasa kama Rose Mhando, Bahati Bukuku na Upendo Nkone.
Akielezea ushirikiano uliokuwepo baina ya  waimbaji chipukizi, anasema kuwa  kila wakati wamekuwa wakipeana moyo na kuamini kuwa kufanya muziki wa Injili si kwa ajili ya kutafuta fedha, au umaarufu bali ni kazi ya wito ili kuwaokoa watu wa Mungu na matatizo ya kidunia.
“Japokuwa ni kazi ya Mungu lakini kuna tatizo lingine kubwa nalo ni usumbufu kwenye studio wakati tukijiandaa kurekodi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba studio hizihizi ndizo zinazotumika kurekodi nyimbo za kidunia,” anaongeza mwanadada huyo aliyejikita vilivyo kwenye imani ya kilolole.
Aneleza kuwa studio nyingi za kidunia zinakuwa na matatizo ya kuiba kazi za waimbaji na kuziuza kinyemela huku akikiri kuwa hata yeye alitokewa na jambo hilo.
 “Nimalizie kwa kusema kuwa huduma ya uimbaji wa nyimbo za Injili inagusa zaidi kumtumikia Mungu na siyo kujulikana kama baadhi ya watu wanavyodhani, na wakati huo huo  niwape moyo watumishi wa Mungu kutokana na kujituma kwao kwenye huduma hii,” anamaliza Anna.





Newer Posts Older Posts