Alex Msama: SIMWACHI ROSE
Msama alifikia hatua hiyo ikiwa ni saa chache toka kuingia mtandao kwa habari hii iliyoandika kuwa; ROSE MUHANDO AIPASUA NDOA YA MTU.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa, toka habari hiyo isomeke kwa wadau wengi, amekuwa akipigiwa simu za kumpa pole kwa tukio hilo .(Msama kushoto akifafanua jambo ndani ya ofisi ya TGM)
“Hii habari imenipa wakati mgumu sana , kila mtu pole, pole, mpaka nimekatisha usingizi leo. Mmi sikubali, nataka kujua aliyewaletea nyinyi hizi habari. Unajua hata Meneja wa Rose (Muhando), Nathan naye amenipigia, kaniuliza nani anayeleta habari mtandaoni?” Alisema Msama.
“Mimi na Rose tuko karibu sana , lakini kikazi na siwezi kumwacha, nimetoka naye mbali. Nimefanya naye matamasha mengi mengi, hata hivi karibuni tutafanya jingine la Pasaka,” alisema Msama.
Aliongeza kuwa, kama kuna wanaofikiria vibaya kuhusu ukaribu wake na Rose, “basi wanakosea sana, ni kwa ajili ya kazi tu na kwa hilo mimi siwezi kumwacha Rose kwa sababu hatuna kitu kingine kibaya baina yetu na tunaheshimiana sana,” alisema Msama.
Akipangua zaidi ishu hiyo, Msama alisema kuwa, yeye, mkewe, Rose na meneja wa Rose, Nathan wanamtafuta ‘mchawi’ anayewawangia usiku na mchana na kusababisha pole zisizokuwa na sababu.

