LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

04/08/10

Pastor Wambura - Sijaukana ulokole

Mwanamuziki wa muziki wa Injili nchini Steven Wambura, ambae ilidaiwa alikuwa akitaka kuingia katika muziki wa kidunia ameibuka upya na kukanusha vikali madai hayo.
Akiongea na safu hii Wambura alisema kuwa wakati yuko Moani Arusha ambako ndio makazi yake alisikia wapinzani wake wakisema maneno hayo na kudai ameishiwa kabisa na amejiunga na bendi ya Tanzanite iliyoko huko hivyo kumuasi bwana.

“Siwezi katu kuimba muziki huo na kama nitashindwa kabisa basi nitabaki kumuimbia bwana kanisani kwani ninaimani ujumbe utafika na sio kuingia katika bendi za kidunia,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa anashangazwa na maneno hayo ya waimba injili chipukizi ambao anahisi walikuwa wanataka kumchafulia ili aonekane ni kondoo aliyepotea kitu ambacho si kwani hivi sasa amesha kamilisha Album yake mpya iitwayo Roho wa Bwana na inaendelea kufanya vizuri katika television na redio mbalimbali nchini.

Wambura, ambaye sasa anatamba na kibao chake cha 'Roho wa Bwana' amesema baadhi ya wanamuziki wa Injili wanashangaza kwa tabia hizo lakini yeye anaamini hiyo ni dalili ya kufika kwa siku za mwisho.

Katika hatua nyingine Wambura amedai kuchukizwa na waimbaji wa muziki huo ambao wamekuwa wakipata kiburi kila kunapokucha kutokana na kupata majina makubwa katika jamii inayowazunguka na kujiona wao ni bora kuliko wengine.

Wambura alisema kuwa, leo hii si jambo la ajabu kuona baadhi ya wanamuziki wa muziki huo wakipata kiburi, maringo na dharau baada ya kufanikiwa badala ya kuendelea kutoa huduma ya kiroho kwa mapana na marefu na baadhi yao hawajasimama katika huduma ya uimbaji.

Aliendelea kudai kuwa kipindi waimbaji hawa wakiwa hawajainuliwa,  hushinda kanisani wakisali na kuomba na wakati mwingine kuhitaji misaada kwa watu ili watoke katika hatua moja kwenda nyingine, lakini baada ya mafanikio huwadharau hata watu ambao waliwasaidia katika siku za awali.

Mtumishi huyo wa Mungu aliendelea kusema kuwa, baadhi ya waimbaji wamekuwa wakiimba kwa ajili ya kutafuta fedha zaidi kuliko kumtumikia Mungu wao ambaye ndiye anawawezesha kufikia mafanikio wanayoyafikia.

Mwanamuziki huyo anasema ni kweli mtu hufanya kazi ya muziki wa Injili akiwa na lengo la kufikisha ujumbe wa Mungu kwa mataifa na mwisho wa siku anahitaji kujikimu katika maisha ya kawaida. Na hayo yanaweza kutimia kama mtu akiwa na fedha.

"Pamoja na kwamba tunahitaji fedha za kujikimu si sahihi kuzitafuta kwa njia za ajabu na kusahau kuwa lengo letu ni kutoa huduma na fedha zinakuja baadaye.

"Kwa kawaida hakuna kiwango cha fedha ambacho mtu anaweza kukitaja kwa ajili ya kutoa huduma ya Mungu, lakini unapojitoa katika kazi hiyo hata Mungu anakubariki na mambo mengine yanakunyookea.

Nyimbo zinazopatikana katika hiyo mpya inayokwenda kwa jina la 'Roho wa Bwana', ambao ni 'Amtegemeae Mwanadamu', 'Usiipende Dunia', Yesu Amesikia Kilio Chako', 'Mwache Yesu Atawale', 'Upendo', 'Hakuna Kama Wewe' na 'Kuja Kwa Yesu'.

Wambura, ambaye alianza kuimba tangu akiwa mdogo katika Kanisa la TAG, Kijenge, Arusha amesema anafurahia mafanikio aliyoyapata kwani sasa anafahamika na muziki wake unakubalika kwa watu wa rika zote.

"Napenda kuona watu wa rika zote wakimtukuza Mungu, napoona kazi yangu inasonga mbele namshukuru sana Mungu wangu ambaye ndiye anayeniwezesha kupiga hatua kila kukicha."

Akielezea suala la kuzungumza kwa lafudhi kama ya watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Wambura alisema kuwa watu wengi wanafikiri anatoka katika nchi hiyo lakini yeye ni Mtanzania, bali muda mrefu ameishi na watu wa Kongo.

"Nilipata lafudhi ya Congo kutokana na kuwa karibu mno na watu wa nchi hiyo. Mwaka 1999, nikuwa Afrika Kusini, ambapo nilikuwa nikifundisha muziki katika Chuo cha Muziki cha Amakosi Theatre jijini Johannesburg, huko nilikuwa na rafiki wengi kutoka Congo . Suala la kuwa nao karibu kwa miaka mingi, limenifanya nizungumze kama wao," anasema Wambura ambaye ni mume wa Penita na baba wa mtoto mmoja aitwaye Timoth.

Upendo Nkone: Nitafanya 'sapraizi' siku ya harusi yangu

Wapendwa katika Yesu Kristo leo nimefanikiwa tena kukutana na muimbaji wa muziki wa Injili nchini anayekwenda kwa jina la Upendo Nkone ambaye nimefanya naye mazungumzo kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake ungana nami ili upate kile alichokizungumza.

TGM: Bwana Yesu asifiwe Upendo
UPENDO: Amee, kwa jina naitwa Upendo Nkone ni mwenyeji wa Kigoma, nimezaliwa katika familia ya kilokole na kulelewa katika maadili ya dini ambayo yamenifanya mpaka leo hii nionekana katika jamii nikimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
TGM: Lini hasa ulianza rasmi kujihusisha na masuala ya muziki wa injili?
UPENDO: Swali zuri, binafsi suala ya uimbaji nililianza nikiwa na miaka mitano (5) kwa sababu muda mwingi nilikuwa nasikiliza nyimbo za dini kupitia radio ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kwenda kanisani ambako nilikuwa nawaona wanakwaya wakiimba nami kuwa navutiwa nao.
TGM: Upo kwenye game ya muziki wa injili kwa muda mrefu sasa, mpaka sasa umepata mafanikio gani kutokana na huduma hii ya kumuimbia Mungu?
UPENDO: Nianze kwa kusema kuwa, mpaka sasa nimefanikiwa kutoa albamu zangu tatu. Ya kwanza ilijukina kama Mungu Baba, yapili niliita Hapa nilipo na ya tatu inakwenda kwa jina la Zipo faida. Namshukuru Mungu kupitia huduma hii nimepata mafanikio makubwa sana. Miongoni mwa hayo ni kupata marafiki wengi ndani na nje ya nchi wanaopenda huduma yangu, ninasomesha wanangu kwenye shule za kimataifa (International), ninausafiri wangu na sasa ninajenga bonge la nyumba maeneo ya Mbezi.
TGM: Hivi karibuni ilielezwa kuwa, umeshampata mwenza wako wa maisha ambaye hukupenda kumuweka wazi, je harusi itakuwa lini?
UPENDO: Na nyinyi wadaku huwa hampitwi na jambo. Ni kweli Mungu ameshajibu kiu ya kuwa na mume wa kufanana na mimi, lakini suala na lini ndoa yangu itafungwa linabaki kuwa siri ya familia yangu na upande wa mwenzangu, na nimedhamilia kufa ‘sapraizi’ siku ya harusi yangu.
TGM: Vipi kuhusu umarufu wako, unakusaidia katika maisha yako ya kila siku?
UPENDO: Kwa namna moja ama nyingine unanisaidia kufanikisha baadhi ya mambo, lakini asilimia kubwa ni mateso. Kwa mfano kwa muda wa miaka 9 ya ujane wangu nimeishi maisha ya mashaka na wasiwasi wa kufanyiwa lolote baya. Kwa sababu sina uhuru wa kutangulizana na mwanaume yeyote hasa nyakati za usiku kwa sababu watu wanaweza kufikiri kitu kibaya. Kwa kifupi umarufu ni mateso.
TGM: Mbali na uimbaji wa muziki wa injili, unafanya kazi gani.
UPENDO: Nafanya kazi ya kushona, taaluma yangu ni fundi chelehani na hivi karibuni natarajia kufungu ofisi yangu hapa mjini.
TGM: Nini malengo yako kuhusiana na huduma ya uimbaji wa muziki wa injili.
UPENDO: Nataka kumurumikia Mungu wangu kwa uimbaji kwa viwango vya juu kuliko ilivyosasa.(Picha kwa hisani ya blog ya Jiachie)

SOLOMON MUKUBWA KUFUNGA PIGU ZA MAISHA KESHO


Mwimba wa muziki wa Injili nchini Kenya, Solomon Mukubwa kesho (Jumamosi) anatarajia kufunga ndoa na katika kanisa moja la Kiroho maarufu nchini humo.
Habari za uhakika ambazo TGM hii imezinyaka zinasema kuwa, Solomon amelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kupata umaarufu kupitia albamu yake ya Mfalme wa Amani ambayo imewakamata watu wa dini mbalimbali na kujikuta akipata msururu wa mademu waliokuwa wanajigongesha kwake.
“Jamaa Jumamosi (kesho) anaoa lengo ikiwa ni kujizuia na majaribu ya kuanguka kwenye uasherati, kwani baada ya kupata umaarufu kupitia albamu yake ya Mfalme wa Amani mademu kibao wamekuwa wakipanga mstari kutaka kampani yake,” kilisema chanzo cha udaku huu. (Picha kwa hisani ya blogo ya Jiachie)

WACHUNGAJI NAO WANA A.K.A!!


Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Assemblies of God, Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo naye ana jina ambalo si la asili, ‘Mzee wa Upako.’
Majina ya aina hii hujulikana zaidi kama ‘a.k.a’ ambapo mastaa wengi duniani ndiyo wenye matumizi hayo. Mfano, Joseph Mbilinyi ‘Mr II’, Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Joseph Haule ‘Profesa J’ na wengine wengi.

WACHUNGAJI NAO WANA A.K.A!!


Mchungaji wa Kanisa la Kiroho la Assemblies of God, Ubungo Kibangu, Anthony Lusekelo naye ana jina ambalo si la asili, ‘Mzee wa Upako.’
Majina ya aina hii hujulikana zaidi kama ‘a.k.a’ ambapo mastaa wengi duniani ndiyo wenye matumizi hayo. Mfano, Joseph Mbilinyi ‘Mr II’, Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Joseph Haule ‘Profesa J’ na wengine wengi.

BEATRICE MUHONE KAANGUKA?

Mwimbaji wa Injili aliyejizolea umaarufu kwenye albamu ya Ingoje Ahadi, Beatrice Muhone amezua viulizo vingi baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu sasa huku wengine wakiamini ameanguka kisanii.
Lakini ukweli ni kwamba, ameshatoa albamu nyingine mbili ila zimeshindwa kuipiku ile ya kwanza kwa sababu hazikuwa na sauti ya Upendo Kilahiro ambaye inasemekana alikuwa msaada mkubwa katika albamu ya kwanza.(Picha kwa hisani ya mtandao)

Newer Posts Older Posts