LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

04/16/10

Maji ya uponyaji yazua utata nchini


Mtafaruku mkubwa umeibuka katika makanisa mbalimbali nchini kuhusu uhalali wa utumiaji wa maji ya uponyaji (Anointed Water) ambayo yamekuwa yakiingizwa kwa kasi kubwa na watumishi wa kiroho kwa ajili ya kuwahudumia kondoo wao wenye matatizo mbalimbali.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, mtafaruku wa maji hayo unatokana na baadhi ya wachungaji huwatoza fedha kidogo  kondoo wao kwa madai ya kuwa wanachangia gharama za kuyasafirisha kutoka Israel ama Nigeria.
Upekuzi huo umebaini kuwa, kwa miaka ya hivi karibuni, maji mengi yanatolewa bure na mtumishi wa Mungu, Nabii Temitope Balogun Joshua a.k.a TB. Joshua ambaye ni mwangalizi wa The Synagogue Church of All Nations (SCOAN) nchini Nigeria.
Hivi karubuni, mchungaji mmoja alitua nchini akiwa na maji hayo kutoka kwa TB Joshua na kuanza kuwauzia waumini wake kwa lugha ya kuchagia kidogo gharama za usafirishaji kutoka Nigeria hali ambayo imetafasiriwa na watu wengine kwamba si sahihi.
Mbali na kuwatoza fedha kidogo waumini wake, mchungaji huyo inasemekana ameleta maji ya Kichina (feki) kutokana na kukosa nembo  ya TB Joshua ambaye kanisa lake hujaza watu wazito kutoka nchi mbalimbali.
“Maji ya uponyaji yaliyoingizwa nchini na mchungaji (anamta jina) ni feki kwa sababu hayana hata picha za Nabii TB Joshua, na amekuwa akiwapulizia waumini wake kwa kuwatoza kiasi kidogo cha fedha kwa kutumia lugha ya kuchangia gharama aliyotumia kuyasafirishia kutoka Nigeria wakati yeye alipewa bure,” alisema mchungaji wa kanisa moja lililopo jijini Dar es Salaam.
Kama kawaida yetu baada ya kupata nyeti hizo, gazeti hili lilimsaka kwa udi na uvumba mchungaji anayetumia maji hayo kujitajirisha kiana kupitia huduma hiyo na lilipompata kisha kumuwekea tuhuma zake mezani, aliruka futi mia kwa maelezo kwamba madai hayo si ya kweli.
 “Siyo kweli kwamba maji haya ni feki kama inavyodaiwa na baadhi wa wachungaji wenzangu, wakati nayachukua kutoka kwa TB Joshua niliacha kuna mengine yanatengenezwa na yametoka hivi karibuni, kwa mantiki hiyo kusema haya ni ya Kichina wanakosea.
“Kuhusu suala ya kuwatoza fedha waumini wangu na watu ninao wahudumia hili nalo si kweli, isipokuwa huwa wanachangia kiasi kidogo cha pesa kama kurudisha gharama ya pesa nilizotumia wakati wa kuzisafirisha,” alisema mchungaji huyo mwenye mwili mnene kidogo na kijipara cha mbali.
Mchungaji huyo aliongeza kuwa ili kuthibitisha kuwa maji hayo si feki tayari ameshaongea na TB Joshua kuja nchini kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa maji hayo na kukata kilimi cha watu wanaompakazia maneno ya kizushi yenye lengo la kuua huduma yake ambayo ameihangaikia kwa muda mrefu.
Wakati mchungaji huyo akipangua tuhuma hizo, kuna baadhi ya watumishi wa Mungu ambao wamekuwa wakipinga huduma hiyo ya maji na kusema kuwa, kufanya hivyo ni sawa na kuyaabudu.
Mmoja wa watumishi hao ambaye amekuwa mstari wa mbele kupinga huduma za wenzake hasa wanaotumia maji, vitambaa, fungo za gari, sabuni na nguo kuwaombea waumini alisema kuwa, leo hii Watanzania wamekuwa kama vile wamerongwa kwani wamekuwa wanaangalia ni kanisa lipi linatenda miujiza na kukimbilia.
Mchungaji huyo mwenye sifa za kutumia muda mwingi kuhubiri habari za kuponda huduma za wenzake alisema kuwa Watanzania wasipojihadhari na mlipuko wa miujiza unaofanywa na watumishi wenzake watajikuta mwisho wa siku wanaangukia motoni.  




Frola Mbasha: Nilianza kuona aibu kucheza ngoma za asili nilipofika darasa la saba, pia walikuwa wananiita mama Asha sababu ya kupenda midoli

Wapendwa wasomaji wa blog  nzuri ambayo imekuwa ikielezea maisha na kazi za waimbaji wa muziki wa injili nchini leo ninaye Frola Mbasha ambaye naamini kila mmoja wetu anamfahamu kutokana na makeke yake awapo jukwaani.
Frola pia amebahatika kuwa na kibali katika jamii kutokana na ujumbe wa nyimbo zake kuwa na mguso wa aina yake kwa  kila anayefanikiwa kuzisikiliza ama kuziona kwa njia ya video. (Pichani kushoto ni Flora Mbasha enzi ya utoto wake aliyeshika daftari)

TGM iliamua kuchoma mafuta mpaka anakoishi Frola na Tabata jijini Dar es Salaam na nilipofika mambo yalikuwa hivi.
TGM: Hodi hapa nyumbani.
FLORA: Karibu, nani mwenzangu.
TGM: Toka nje, wewe utanijuaje kama utakuwa ndani.
FROLA: Siunajua tena jiji hili limeshachafuka, unaweza ukatoka kichwa kichwa ukakutana na vibaka.
TGM: Hapana uwe na amani kabisa hii ni SIDE B leo imeamua kuja kukutembelea.
FLORA: Aman, karibu sana mdau.
TGM: Nashukuru. Bwana Yesu asifiwe
FLORA: Amen, za uzima.
TGM: Nzuri, Mungu ananisaidia.
FLORA: Haya nakusikiliza kwa maana nyingi mkionekana kwa mtu ni lazima kuwe na jambo. Nikijaribu kuangalia kila eneo naona niko salama sina sikendo hata kidogo na sitaki hali hiyo initokee maishani mwangu.
TGM: Wala usihofu mimi nimekuja kwa mema tu. Tatizo lenu wasanii ni hilo, mkiona waandishi tu mnafikiria masuala ya skendo.
FLORA: Nikweli, japo mimi huwa sifikirii sana ishu kama hivyo kwa sababu Mungu ananisaidia nisifanye mambo yaliyokinyume na mapenzi yake.
TGM: Ok. Twende kwenye pointi, nimekuja kwako kutaka kujua maisha yako kwa ujumla pamoja na huduma yako.(Pichani kulia Flora akiwa na watoto wenzake)
FLORA: Kwanza kabisa mimi nilizaliwa tarehe 1 Juni 1983 katika hospitali ya Hindu Mandhal mjini Mwanza. Baba yangu anaitwa Henry Joseph Mayalah ambaye kwa sasa ni marehemu. Mama yangu anaitwa Calorin Moses Kulola. Katika familia yetu tumezaliwa watoto wa 5, wa kiume ni mmoja aitwaye Benjamini na wakike tupo wa nne, mimi nikiwa wa pili kuzaliwa, akafuata Dorcus, Suzan na wa Mwisho akiwa ni Esther.
TGM: Tanzania ni nchi yenye amani. Watu huulizana makabila ili wapate kutaniana vizuri kwa lengo la kudumisha undugu. Niambie wewe ni kabila gani?
FLORA: Sisi ni Wasukuma wa Sengerema wilaya ambayo imo ndani ya mkoa wa Mwanza. Nimekulia katika maadili ya dini ya Kikristo, babu yangu akiwa ni Askofu mkuu wa kanisa la Evangelistic Assembilies of God. Babu na bibi yangu mpenzi Elizabeth ndiyo walionilea kwa pamoja wakishirikiana na mama yangu mpendwa.
TGM: Huduma ya uimbaji uliianza lini.
FLORA: Nilianza kuimba nikiwa darasa la tatu. Wakati huo nilikuwa nikienda na mama zangu wadogo kwenye kwaya hadi nilipokuwa na umri wa miaka kumi na tatu na ndipo nilipoanza rasmi kuimba kwaya ya kanisani na kuimbisha baadhi ya nyimbo.
TGM: Inamaana mumeo Emmanuel Mbasha alikuoa ukiwa mwimbaji wa kwaya ama ulikuwa unaimba peke yako?
FLORA: Alinioa nikiwa naimba katika Word Alive Band na baada ya kufunga ndoa Septemba 22 2002 mwaka 2002 tulianza kuimba pamoja na mume wangu tukiwa. Mungu alitusaidia mwaka 2003 nikajifungua binti mrembo aitwae Elizabeth, jambo hili hunifanya nimshukuru Mungu kwa kutupa mtoto huyo. Mwaka wa 2004 nilifanikiwa kurekodi album yangu ya kwanza niliyoita "JIPE MOYO" ikiwa na nyimbo 10.
TGM: Nikitu gani ambacho ulikipenda sana kipindi cha utoto wako.
FLORA: Nilipenda sana kusikiliza nyimbo za dini kutokana na familia yetu kuwa katika mazingira ya kidini zaidi. Pamoja na hayo nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu sana nyimbo za Maria Kelly na Celine Dion. Vibao vya akina dada hao vilikuwa vinaukosha moyo wangu na kunifanya niwe na kazi ya kuzirekodi nyimbo zako kisha kujizimba kwa kwa sauti ya juu kama wao.
TGM: Nyimbo hizo ni za kidunia, na wewe ulikuwa katika maadili ya dini ya kikristo, hukuona kama ulikuwa unafanya makosa kufanya hivyo?(Kulia Flora akiwa na Christina Shusho jinsi alivyo sasa).
FLORA: Hapana kipindi hicho nilikuwa sielewi kama nilikuwa nafanya makosa bali nilikuwa najifunza hasa sauti zao. Kutokana na kuvutiwa na uimbaji wao nililazimika kununua daftari na kuziandika nyimbo hizo na kuzikariri mpaka nikazifahamu zote. Baada ya kuzikariri nikawa na kazi ya kuziimba hasa nyakati za usiku nilikuwa silali mapema kwa sababu ya kuimba nyimbo zao.
TGM: Ok, baada ya kuzikariri na kuziimba nyimbo hizo uliambulia nini katika maisha yako.
FLORA: Kicheko kidogo. Unajua wasanii hao naweza kusema ndiyo walimu wangu wa sauti kwa sababu kipindi hicho nilikuwa naimba wimbo kwa ‘kii’ ya juu ambayo waimbaji wengi inawashinda, na ndiyo maana mpaka leo hii nyimbo zangu huwa naziimba kwa sauti ya juu sana na kisha nashusha. Na mimi sijaenda kusomea masuala ya muziki na kupata zoezi la kuimba kwa ‘kii’ ya juu.
TGM:  Mbali na kupenda nyimbo za wasanii hao kutoka ‘mamtoni’ ni mchezo gani mwingine ambao ulikuwa unapenda kuucheza enzi za utoto wako.
FLORA: Duh! Jamani maswali hayaishi tu? Any way, hakuna mchezo ambao nilikuwa naupenda sana kama ngoma za asili hasa nilipokuwa shuleni. Kila niliposikia kuna maandalizi ya tamasha, kongamano ama umitashumita nilijawa na furaha moyoni mwangu na nilikuwa nafanya mazoezi kwa kujituma kiasi kwamba walimu na wanafunzi wenzangu walinipenda.
TGM: Mlikuwa mnacheza ngoma gani?
FLORA: Tulikuwa tunacheza ngoma za makabila mbalimbali na wakati mwingine tulikuwa tunavaa nguo fupi na baadhi ya maungo yalikuwa wazi. Lakini nilipofika darasa la saba nilianza kuona aibu kucheza nimevaa hivyo mbele za watu na ndiyo ulikuwa mwisho wangu wa kucheza ngoma za asili.
TGM: Ulijiona umekua ama?
FLORA: Ndiyo. Kicheko, si unajua tena masuala ya kiutu uzima yakianza kumuingia mtu, baadhi ya mambo aliyokuwa anayafanya bila kuona aibu anaanza kufanya hivyo.
TGM: Najua kila mtoto huwa anapitia kwenye hatua ya kuigiza kama baba na mama, wakati mwingine kujipikisha ugali, wali wa mchanga kwa imani kabisa kuwa ni chakula safi na kazi nyingine nyingi. Jew ewe unakumbuka mchezo gani ambao leo hii ukiukumbuka huwa unacheka pekeyako kutokana na ulivyokuwa unaigiza?
FLORA: Kicho kidogo. Unajua wakati mwingine ukiyafikiria maisha ya utoto utabaini yanaraha sana. Mimi nilipenda sana kuigiza nikiwa mzazi na nilifanikiwa kumpeda mdoli ambao niliuita Asha. Watoto wenzangu walikazoea kuniita Mama Asha. Jina hilo lilizoeleka shuleni na hata nyumbani, jina la Frola baadhi yao walilisahau.
TGM: Mbali na kupenda sana doli, ni mchezo gani mwingine ambao ulikuwa unakufahisha ulipokuwa unakutana na watoto wenzako.
FLORA: Nilipenda sana kucheza mchezo wa lede kwa sababu nilikuwa mwepesi wa kuruka.
TGM: Nasikia enzi za utoto wako wako ulikuwa mtundu sana kiasi kwamba wazazi wako wakawa wanakuchapa viboko mara kwa mara.
FLORA: Mh! Nikweli lakini haikuwa sana kama unavyofikiri, naamini suala la mtoto kuchapwa na wazazi wake hilo huwa halikwepeki. Lakini Namshukuru Mungu muda mwingi nilikuwa nafanya vitu ambavyo wazazi wangu walikuwa wanavikubali.
TGM: Nijambo gani ambalo ulilifanya utoto na kipindi hiki ukilikumbuka huwa unajishangaa kama ni wewe uliyekuwa unafanya hivyo?
FLORA: (Kicheo kidogo). Ni suala la kuitwa mama Asha, muda wote huo nilikuwa najiona kama tayari nimesha zaa. Hiyo ilitokana na kuupenda sana mdoli wangu ambao nilikuwa nalazimika kulala nao kitandani, na wazazi wangu walipokuwa wakininyanganya nilikuwa nalia kweli mpaka wananionea huruma na wananirudishia.
TGM: Nikitu gani ambacho ulikuwa unakiogopa sana utotoni mwako? Nilikuwa naogopa kuchwa fimbo na wazazi wangu, mara nyingi nilikuwa najitahidi kufanya kwa makini kila nililokuwa naaelekezwa ilimradi tu nisitandikwe bakora.
TGM: Unakumbuka kwa mara ya mwisho kuchapwa fimbo na wazazi wako ilikuwa mwaka gani.
FLORA: Mh! Kwakweli sikumbuki hata kidogo.
TGM: Nikitu gani ambacho ulikuwa unapenda kukifanya ukubwani kama ulivyo sasa?
FLORA: Nilipenda sana niwe  injinia wa kopyuta na umeme, japo ndoto hii haijatimia lakini naamini ipo siku nitapiga kitabu kwa lengo la kuyafikia malengo yangu.
TGM: Wakati tunamalizia mazungumzo yetu kuhusiana na masuala ya maisha yako ya utotoni, hebu sasa tuangalie ya sasa. Wewe ni muimbaji uliyefanikiwa kupata jina ndani na nje ya nchi. Kwa nini umeanza kupoteza mashabiki wako kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
FLORA: Siyo kweli mimi bado ninamashabiki kibao, ila kuna baadhi ya watu wamekuwa wakidai kwamba hawanielewi kutokana na nyimbo zangu za sasa.
TGM: Kivipi tena.(Kushoto Frola akiwa na kundi laki akiwa katika kumtukuza Mungu, katikati ni mumewe Emmanuel Mbasha)
FLORA: Kuna baadhi ya watu wanadai kutonielewa kwa sababu wakati mwingine nimekuwa najichanganya na wanamuziki wa kimataifa na hasa niliposhiriki tamasha la ‘Zinduka’ hivi karibuni.
TGM: Lakini si nikweli? Iweje wewe unaimbaji  muziki wa injili kisha unapanda jukwaa moja wana wasanii  wa muziki wa kidunia?
FLORA: Mimi kuwa muimbaji wa nyimbo za Injili, hakunizuii kushiriki katika matamasha yenye lengo la kulitetea taifa hasa kweny kampeni hiyo ya kupambana na ugonjwa wa malaria.
TGM: Mbali na uimbaji wa muziki wa injili, kazi gani nyingine unayofanya?
FLORA: Aslimia 90 natgemea muzuki na wala sina kazi yoyoye zaidi ya kufuga kuku wa nyama.
TGM: Nakushukuru sana kwa ushirikiano wako kwangu, nakutakia huduma njema.
FLORA:  Karibu tena siku nyingi.


Frank John Litambo ‘Mungu akikuinua hakuna wa kukushusha’


Muziki wa Injili unaendelea kujipatia mashabiki wengi hapa Tanzania kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika kwa mfano, Afrika Kusini, Nigeria, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambazo miaka ya hivi karibuni zimekuwa ni mifano bora kwenye maendeleo ya muziki huo.

Kwa sasa waimbaji wengi wa Kitanzania wameendelea kufuata za nyayo za wakali wengine wakubwa dunia kama Marymary, Makoma, Midnight Crew ambao kwa kiwango kikubwa wamekuwa ni mifano kwa waimbaji wa maeneo mengine duniani.

Mwinjilisti Frank John Litambo ambaye ni mmoja wa waimbaji wa muziki wa Injili hapa Tanzania kwa kuda mrefu sasa ameendelea kufanya harakati kwenye muziki huo kwa kushirikiana na waimbaji wengine wa ndani na nje ya taifa hili.

Akizungumzia harakati zake ndefu na mafanikio ambayo ameyafikia, Litambo  anasema kuwa kuna mengi amepitia lakini anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa mafanikio licha ya vikwazo mbalimbali alivyokutana navyo.

“Nina kila sababu ya kushukuru kwa maana hatua hii niliyofikia si jambo rahisi naamini kuwa Mungu akiamua kukupandisha hakuna  anayeweza kukushusha.

“Kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa kuingia kwangu kwenye muziki wa Injili halikuwa ni jambo la kutaka ila ulikuwa ni wito kutoka kwa Mungu, ndiyo sababu nimeendelea kuwepo hadi sasa,” ameongeza muimbaji huyo ambaye yupo ndani ya fani hiyo kwa miaka sita sasa.

Baada ya kufanya utumishi huo kwa muda mrefu hivi sasa Muinjilisti Litambo ametoka tena na kazi mpya ikiwa ni ya pili  ambayo tofauti na kazi nyingine ameamua kufanya uzinduzi kwa njia ya hisani kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu wa masikio (viziwi) utakaofanyika Mei 9 mwaka huu.

“Katika albam yangu hii uzinduzi wake utakuwa ni tofauti kwa kuwa nimelenga kupeleka fedha kwa watu wenye matatizo katika jamii, miongoni mwao ni watoto wasiokuwa na uwezo wa kusikia.

“Kwenye jambo hili  nimeshirikiana na viongozi wa dini na wanasiasa ili kulifanikisha naamini huu ni mchango wao mkubwa katika jamii inayowazunguka,” amefafanua muimbaji huyo.

Ndani ya hafla hiyo atasindikizwa na waimbaji mbalimbali wa Injili kutoka Tanzania ambao ni Ambwene Mwasongwe, Sifa John, Victor Aron, Catherine Ntepa, KKKT Unjilisti Kijitonyama na The Messengers Band.

Katika albam hiyo ya pili kwa Muinjuilisti huyo imebeba jumla ya nyimbo nane ndani yake ambazo baadhi yake ni Mama, Atatufuta Machozi, Yatima, Ndoa na nyingine nyingi.

Newer Posts Older Posts