BONY MWAITEGE AIBUKA UPYA
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kusikika katika anga ya injili, hatimaye muimbaji maarufu wa muziki huo Bony Mwaitege aliyetamba sana na wimbo kinao cha Utanitambuaje kama nimeokoka, ameibuka na albamu mpya inayokwenda kwa jina la Mama ambayo imeanza kusikika katika vituo mbalimbali vya radio hapa nchini.
Kuibuka upya kwa muimbaji huyo kunamaliza maswali yaliyokuwa yanaulizwa na watu mbalimbali juu ya ukimya wake aliokuwa nao huku wengine wakisema kuwa aliishiwa maishari. Kwa habari zaidi juu ya mwimbaji huyo endelea kufuatilia kupitia mtandao huu.
