George Kayala amtukuza Mugu kwa makuu aliyomtendea
Majaribu yameruhusiwa ili yatujenge kiimani. Hivi karibuni nilipatwa na jaribu zito ambalo lilinitoa katika imani moja na kunisogeza hatua nyingine. Namshukru Mungu wangu aliyekuwa upande wangu kwani binafsi nilinyamaza kimya na yeye alinipigania. Jaribu lenyewe lilikuwa la kusimamishwa kazi ghafla kwa muda wa mwezi mmoja na wiki moja baada ya kuzingiziwa jambo flani ofisini kwangu. Kabla ya kusimamishwa nilipata msukosuko mingi. Hapa namshukuru Mungu wangu kwa kunishindia suala hilo. Mtumishi wa Mungu, Askofu Nicolaus Suguye alikuwa upande wangu kwa kuniombea usiku na mchana pamoja na mchungaji Anna Suguye. Hakika Mungu ni mwana sana.

