LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013
WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.
JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA
KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.
ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.
IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404
REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI
03/30/11
SOLOMONI MUKUBWA: MKONO MMOJA LAKINI NITAFANYA KWELI TAMASHA LA INJILI
Gospel Music Center 0
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Kenya, Solomoni Mukubwa amesema kuwa, licha ya kuwa na mkono mmoja lakini atafanya kweli katika tamasha la muziki huo linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar.
Akipiga stori na waandishi wa habari juzikati nchini Kenya, Mukubwa alisema kitendo cha kuwa na mkono mmoja haina maana hawezi kucheza kama wengine na siku hiyo atafanya vitu adimu ambayo hajawahi kuvifanya tangu aanze kuimba muziki huo.
“Kitendo cha kuwa na mkono mmoja hakunifanyi nishindwe kuimba na kucheza kama wafanyavyo wengine, siku ya tamasha la muziki wa Injili nchini Tanzania nitafanya vitu adimu ambavyo sijawahi kuvifanya tangu nianze fani hii,” alisema Mukubwa ambaye ni raia wa Kongo.(Picha kwa hisani ya francisgodwin).
TAMASHA LA PASAKA KUVUNJA REKODI MWAKA HUU
Gospel Music Center 0
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa tamasha la Pasaka la mwaka huu linalotarajiwa kufanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, litavunja rekodi ya matamasha yote aliyowahi kuandaa.
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, litavunja rekodi ya matamasha yote aliyowahi kuandaa.
Akizungumza na mtandao huu ndani ya ofisi zake jijini Dar es Salaam, Msama alisema kuwa kuvunja rekodi kwa tamasha hilo kunatokana na waimbaji waliodhibitisha kushiriki kuwa katika maandalizi mazuri na kila mmoja amekuwa na mda mzuri wa maombi kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa Rais, Jakaya Kikwete. Tamasha hilo litapambwa na waimbaji nguli wa nyimbo za kumsifu Mungu wakiongozwa na Rose Muhando.
Anawataja wasanii wengine wa nyimbo za Injili watakaopamba tamasha hilo ni Upendo Nkone, Bony Mwaitege, wanamuziki kutoka Kenya, Anastazia Mukabwa na Pamela Wanderwa na Mzambia, Ephraim Sekeleti aliothibitisha kushiriki.
Tamasha hilo lina malengo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima, kuwasaidia
mitaji ya biashara wajane wasiojiweza na waathirika wa mabomu yaliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto, Dar es Salaam, Februari 16 mwaka huu. Msama anasema kwa Dar es Salaam kiingilio kitakuwa Sh 4,000 kwa viti vya kawaida, viti vya maalumu (B) Sh 10,000 na viti maalumu (A) Sh 20,000. Tiketi za kategoria hiyo hazitauzwa mlangoni.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya mbili kutoka katika nchi hizo.
Msama anasema msanii Sekeleti naye amekubali kushiriki na atatua nchini akiwa na albamu mpya iitwayo Mungu Mwenyewe. Anazitaja baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo kuwa ni Uniongoze na Kidonge cha Yesu.
Anasema Sekeleti atakuja nchini pamoja na waimbaji wake 10 na ataimba live siku hiyo.
Msama amesema kwamba tamasha la mwaka huu limekuwa na maboresha makubwa mno kwa ajili ya kukidhi matakwa ya wapendwa wengi.
“Kwanza kabisa tofauti na matamasha yaliyopita mwaka huu tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa muziki wa Injili kutoka nchi za nje,” anasema. “Waimbaji wote maarufu wa muziki wa Injili
watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakikisha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali.
WALIOTEMBELEA BLOG HII
TUMA HABARI NA MATUKIO
KAMA UNA HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI POPOTE DUNIANI TUMA KWA EMAIL HII. productiongmk@gmail.com. NAMI NITAZIWEKA KWENYE BLOG HII BILA GHARAMA YOYOTE. NAKARIBISHA HABARI ZA MATAMASHA YA INJILI, MIKUTANO, RATIBA ZA MAKANISA, SEMINA, HARUSI NA MAMBO MBALIMBALI KWA AJILI YA KUWAJULISHA WANAULIMWENGU. WASILIANA NAMI KWA NAMBA ZIFUATAZO.
+255 712 001 880,
+255 755 240 136.
HABARI MUHIMU
-
Wapendwa katika Yesu Kristo leo nimefanikiwa tena kukutana na muimbaji wa muziki wa Injili nchini anayekwenda kwa jina la Upendo Nkone ambay...
-
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Efatha Ministries anayetikisa jijini la Dar es salaam na amejikusanyi waumini wengi kiasi kwamba huduma...
-
Aliyekuwa muimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini Fanuel Sedekia alizikwa Januari 10 mkoani Arusha baada ya kufariki dunia usikua wa kua...
-
Nivigumu kuamini lakini ukweli ni huo kwamba, mtoto mmoja wa miaka 10, Anna Msingwa aliyezaliwa akiwa kipofu ameanza kuona huku Iringa, kwa...
-
Hakuna asiyeelewa kwamba mkoa wa Mbeya ni mkoa ambao umekuwa ukitoa waimbaji mahiri wa muziki wa injili wenye tungo ambazo msikilizaji wa ny...
-
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Kenya , Solomon Mukubwa leo (Jumamosi) anafunga pingu za maisha na Bi. Betyy katika kanisa moja la Kir...
-
Ndoa ni nini? Ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke unaokubalika kiutamaduni na kidini ambao unatarajiwa kudumu, kuwapa haki sawa za kiji...
-
Kwa wapenzi wa muziki wa injili nchini, jina la Shusho si jina geni masikioni mwao kutokana na umahiri wa kutumia kipawa cha uimbaji cha mwa...
-
Baraka akiwa na mwanaye Deliver akiwa nyumbani kwake mkoani Mbeya Deliver Baraka akiwa katika pozi safi Deliver Baraka ...
-
Baada ya kukaa kimpya kwa muda mrefu bila kutoa albam mpya na kupelekea baadhi ya wadau wa muziki wa Injili kuhoji uwepo wa Bony Mwaitege ka...
Categories
- George Kayala (23)
- George Kayala. (6)
- Kabula John George (1)


