LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

04/18/11

Gwajima

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ametoa mpya kwa kutahadharisha kuhusu tiba ya kikombe cha Mchungaji Ambilikile Masapile wa Samunge, Loliondo kwa kusema kuwa endapo dawa hiyo anayoitoa inaponyesha watu asibughudhiwe wala asipigwe vita.

Gwajima alitoa tahadhari hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita kanisani kwake jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Tanganyika Pakers, Kawe alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa gazeti hili juu ya msimamo wake juu tiba anayoyatoa mchungaji Masapile maarufu kwa jina la Babu.
Alisema kwamba hajajua kama dawa hiyo inaponyesha watu au laa na kueleza kuwa, kama wagonjwa wanaoitumia wanapona ni jambo zuri, hivyo hakuna sababu ya kubughudhiwa bali apewe ushirikiano ili aendelee kuwasaidia wagonjwa.
“Hao watu wanaompiga vita Masapile ina maana wameshindwa kuwasaidia wagonjwa na ndiyo maana wanakimbiwa na kubakia kulalamika huku wakiponda huduma anayoitoa mchungaji huyo. Wagonjwa ni wajanja sana, wanaangalia ni wapi wanaweza kupata uponyaji,” alisema Gwajima.
Aliongeza kusema kuwa, kunywa dawa ya miti si dhambi kwani hata vidonge vinavyotumika kutibu magonjwa mbalimbali vinatokana na mimea isipokuwa huwa vinatengenezwa kiwandani, hivyo haoni tatizo kwa Masapile kutumia uponyaji wa mizizi anayodai kuoteshwa na Mungu.

MZEE WA UPAKO

Mzee wa Upako, Mchungaji Anthony Lusekelo (pichani) amemtibulia kupata wateja Mchungaji Ambilikile Masapile baada ya kuweka kambi katika Jiji la Arusha ambako aliibuka akiwa na maji na mafuta ya upako.

Kutibuliwa kwa Babu kulishuhudiwa na mtando huu hivi karibuni baada ya kushuhudia wagonjwa wengi ambao walikuwa na mpango wa kwenda kijijini Samunge kupata kikombe kukatiza safari zao na kwenda katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid au katika Jengo la Sinema la Metropole kupata upako wa Mchungaji Lusekelo.
Baadhi ya wagonjwa waliozungumza na mtandao huu akiwemo Suzan John, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, waliambiwa kwamba Mzee wa Upako yupo jijini hapo, na kwa kushawishiwa na baadhi ya wagonjwa waliokwenda kwa Babu na kutopata nafuu waende kwa Mzee wa Upako kuliko kuendelea kungoja foleni ya kwenda Samunge.
“Mimi kuna mtu aliniambia matatizo yangu yanaponywa na Mzee wa Upako, hivyo nikaamua kukatiza safari ya Samunge nikaenda Metropole Sinema na kweli nilipoombewa tatizo langu likatoweka,” alisema Suzana aliyedai kutoka Bunda.
Mwandishi wetu alishuhudia wagonjwa wengi kutoka mikoani wakiacha safari ya kwenda kwa Babu na kuhudhuria maombi ya Mzee wa Upako ambaye alitangaza wazi kuwa, kwake kuna uponyaji wa kweli wa Mungu.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu, Mchungaji Lusekelo alikiri kuwa ni kweli aliweka kambi Arusha na kuokoa watu wengi ambao walitaka kwenda kwa Babu na hata wale waliokwenda na kutoponywa.
“Kwanza siku hiyo kulikuwa na mvua nyingi sana, nikaikemea na ikaacha kunyesha, upinde wa mvua ukakunjika katikati ya uwanja, watu walishangaa sana.“Lakini pia kulikuwa na wagonjwa, kwa mfano mama mmoja alikuwa mjamzito na alikuwa hajifungui, kuna mzee mmoja alikuwa amevimba miguu na baadhi yao walipata kikombe lakini hawakupona, niliwaombea na wakapona,” alisema Mzee wa Upako.
Alipoulizwa njia anayotumia kuponya watu alisema:”Ninatoa maji ya uzima ambayo nayabariki kwa mikono yangu na yanatibu magonjwa sugu tofauti na hicho kikombe kimoja wananchi wanachokikimbilia huko Loliondo,” alisema Lusekelo.
Akaongeza kuwa, anaamini maji hayo anayotoa ni zaidi ya kikombe cha Babu wa Loliondo na amewaomba wananchi kuyanywa kwani yanaponya magonjwa sugu.
Alitamba kuwa, alilitikisa anga la Mkoa wa Arusha baada ya kupata mapokezi makubwa licha ya kuwepo kikombe cha Babu huyo.

MSAMA ARUSHIWA DONGO LA UNYANYAPAA TAMASHA LA INJILI


Baadhi ya waimbaji wa Injili Bongo, wamemkosoa muandaaji wa Tamasha la Injili litakalofanyika Aprili 24 mwaka huu, Diamond Jubilee, jijini Dar, Alex Msama kurekebisha uchujaji na upangaji wa majina ya washiriki wa kuimba.
Wakizungumza na mtandao huu hivi karibuni kwa sharti la kutotajwa majina yao, waimbaji hao walisema karibu washiriki wote ni wale wale kila mwaka wakati kuna wapya wameibuka na nyimbo kali.
“Unajua nini, itafika mahali jamii itahoji kuna nini kwenye Tamasha la Injili, kila mwaka waimbaji ni wale wale tu, kwani hakuna wengine, au ana unyanyapaa?” Alihoji mwimbaji mmoja.
Mwimbaji mwingine ambaye anashika kasi katika nyimbo hizo, yeye alisema ni wakati wa Msama kuingiza sura mpya kila mwaka ili kulifanya tamasha hilo kusisimua zaidi.
Msama mwenyewe alipohojiwa na mtandao huu alisema sura mpya zipo kibao, akaongeza kuwa, hakuna mwaka aliyoingiza wasanii kwa upendeleo, anafanya nao mazungumzo kwanza, wanaokubali wanaingia mkataba, wengine huwa wanamwambia hawatakuwa na nafasi.

JANETH JONAS MREMA MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI (THE HEALING VOICE)

YAJUE MAISHA YAKE, WAPI AMETOKEA NA ANAKOENDA

Janeth ni mtoto wa kwanza wa familia ya Mzee Elly Temu na marehemu mama Veronica Bagenyi. Baba yake alizaliwa Marangu Moshi kijiji cha Komalyangoe na mama yake alizaliwa mkoani Kagera Wilaya ya Karagwe kijiji maarufu cha Kaisho. Aidha katika tumbo la mama yake wamezaliwa watoto wanne wa kike wawili (2) na wa kiume wawili (2) wengine ni Lucas, Eric na Catherine.

Kwa sehemu kubwa ya maisha yake Janeth ameishi eneo la Area C Dodoma ambapo baba yake ni mwajiriwa wa Wizara ya Nishati na madini (GST) Dodoma. Janeth alihamia rasmi jijini Dar es Salaam mwezi July 2002 baada ya kuajiriwa na Kampuni ya Ujenzi kutoka Kuwait iitwayo M.A Kharafi & Sons katika idara ya uhasibu, Kampuni iliyohusika na ujenzi wa majengo makubwa duniani yakiwemo majengo maarufu ya Millenium Tower Kijitonyama na Ubungo Plaza yote ya jijini Dar es salaam. Ni katika ujenzi wa Majengo hayo Janeth alipokutana na mhandisi Jonas Mrema na hatimaye kufunga naye ndoa mwaka 2004. Aidha mwimbaji Janeth Mrema ni mama wa Kijana aitwae Ernest Mrema (Junior).
ELIMU
Janeth Mrema alihitimu elimu ya msingi katika shule ya msingi kiwanja cha Ndege Area C Dodoma mwaka 1991, alifaulu na kuchaguliwa kujiunga shule ya Sekondari ya Dodoma na kuhitimu kidato cha nne (O-Level) mwaka 1995, hapo pia alifaulu na kuchaguliwa kujiunga na shule ya wasichana Ashira iliyopo eneo la Marangu mkoani Kilimanjaro ambapo alihitimu kidato cha sita mwaka 1998. Mwaka 1999 dada Janeth alijiunga na na chuo cha Biashara kampas ya Dodoma kwa ajili ya elimu ya juu ambapo mwaka 2002 alihitimu na kutunikiwa Stashahada ya juu ya uongozi wa biashara ( Business Administration), aidha Janeth amekuwa akivutiwa na mambo ya ujasiriamali na uongozi hivyo ameendelea kuhudhuria kozi mbalimbali zinazohusu mambo hayo ili kujinoa zaidi, pamoja na huduma ya uimbaji, Janeth na mumewe Jonas wanajishughulisha na shughuli za ujasiriamali.
JANETH NA UIMBAJI
Kipaji chake cha uimbaji, walianza kukigundua walimu wake wa shule ya Jumapili (Sunday School) katika kanisa la KKKT usharika wa Arusha road Dodoma, na kati yao hakusita kuwataja mwalimu Alexander Lyaro na Mchungaji Menard Kipyali ambaye pia alihusika sana kukinoa kipaji chake baadaye alipojiunga na kwaya ya vijana.
Akiwa darasa la saba Janeth alichaguliwa na walimu wake wa shuleni kutunga wimbo ambao uliimbwa katika maadhimisho ya UMISHUMTA 1991, ambayo kitaifa yalifanyika mkoani Dodoma kwa mwaka huo.
Akiwa Sekondari alishika vyeo mbalimbali kama katibu wa Ukwata Dodoma Sekondari, Mwenyekiti msaidizi wa Ukwata akiwa Ashira High School, na katibu wa Tafes alipokuwa chuoni. Mwaka 2001 aliweza kuwa mwakilishi katika mkutano mkubwa wa vijana EZRA Conference uliofanyika Nairobi nchini Kenya, na katika mambo yote hayo msukumo mkubwa ulitokana na huduma yake ya uimbaji.
Baada ya kuolewa Janeth na familia yake ni washiriki wa kanisa la Kibaptisti Magomeni jijini Dar es Salaam, chini ya Mchungaji Anyingisye Mwasandube, ingawa huduma ya uimbaji inawapa nafasi ya kushiriki makanisa na huduma mbalimbali.
MSAMBAZAJI NA UPATIKANAJI
Watu mbalimbali walimtia moyo na kumhimiza Janeth kuingia studio, na hilo limewezekana, Janeth amefanya albam nzuri sana mwanzo mpaka mwisho yenye nyimbo maarufu kama Piga Makofi, Mbona washika tama, Sala yangu, Nakuhitaji Roho n.k ambayo sasa imeingia sokoni na inasambazwa na UMOJA AUDIO VISUAL na GMC wasanii promoters na inapatikana katika Audio tape, Audio Cd, Vcd na Dvd.


UZINDUZI
Albamu ya piga ya PIGA MAKOFI itazinduliwa rasmi siku ya Jumapili ya tarehe 29 May 2011 katika ukumbi mwanana wa Ubungo Plaza kuanzia saa 7:45 Mchana.
Uzinduzi huu utakuwa ni wa aina yake kabisa na utahudhuriwa na wageni mbalimbali mashuhuri wakiwemo, wanasiasa, wafanyabiashara, watumishi wa Mungu na wakurugenzi wa makampuni mbalimbali. Aidha dada Janeth anapenda kuwakaribisha watu wote wa dini na madhehebu yote kuhudhuria tamasha hilo kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Waimbaji mbalimbali wa ukweli watakaotinga ndani ya ubungo Plaza kumtia joto mwenzao ni pamoja na ile bendi maarufu inayoimba nyimbo za Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa n.k, ijulikanayo kama the Messengers Band, bila kuwasahau The TM Music waimbaji wa kimataifa wenye vipaji vya ajabu ambao wanaimba kwa style ya Congregational Singing (uimbaji wa watu wengi) kikundi hiki kina waimbaji wengi zaidi ya watu 200, pia kwaya mbalimbali zitakuwepo.
Waimbaji binafsi ni pamoja na Martha Mwaipaja, Stella Joel, Ningile Mwakatage, Kanuni Kayombo, Addo November, Upendo Nkone, bila kumsahau mwana mama Christina Shusho.
KIINGILIO
Kiingilio katika uzinduzi huo kimeshushwa ili kila mtu aweze kuhudhuria hivyo kitakuwa shilingi elfu tano kawaida na elfu kumi viti maalumu usingoje kusimuliwa, njoo ushuhudie mwenyewe, na Mungu akubariki, Amina.

JANE MISSO AKUMBWA NA SKENDO

MUIMBAJI maarufu wa nyimbo za injili nchini Jane Miso hivi karibuni alikumbwa na skendo baada ya kudaiwa kukunja kitita kirefu cha fedha na kuingia nazo mitini.

Mtandao huu kwa masikitiko yaliyoambatana na maswali ya siamini jamaa mmoja anajihusisha na biashara za kuuza spea za magari aliyejitambulisha kwa jina la Benson Mafuwe alisema kuwa mwanzoni mwa mwezi wa tisa mwaka 2007 alikutana na muimbaji huyo na kumuomba amsaidie kukamilisha albam yake iliyotambulika kwa jina la ‘0M0Y0’ ambapo bila ya kuweka kinyongo na mimi mwenyewe ni mmoja wa watu waliokoka nikakubali kumsaidia lakini kilichokuja kutokea siamini mpaka hivi sasa naongea na wewe.
‘Unajua nasema siamini kwasababu gani sikutegemea mtu kama Jane angekuwa tapeli kiasi hiki’ alidai Benson
Akiendelea kusimulia Benson alisema kuwa baada ya makubaliano yao kufikia hatua nzuri waliongoza hadi kwa Mwanasheria wake aliyemtaja kwa jina moja Rwiza wa kampuni ya Azania Law Chambers na kuandikishiana mkataba na kumkabidhi fedha taslimu shilingi milioni kumi ‘10,000,000’ zitakazotumika kutengeneza Audio na Video Cd za albam hiyo maandalizi ya uzinduzi pamoja kuwalipa vikundi mbalimbali vitavyoalikwa siku ya uzinduzi na kukubaliana chochote kitakachopatikana kwenye albam hiyo ya ‘OMOYO’ basi  wagawane pasu kwa pasu, mkataba ambao uliingiwa September 17, 2007 na Ijumaa kubahatika kupata nakala ya mkataba huo.
‘Kiukweli tangu niingie naye mkataba hakuweza kunishilikisha kwa chochote kile hadi siku alipozindua albam yake na kushuhudia akipata fedha taslimu milioni nane kwani mgeni rasmi alitoa milioni tano na watu wengine walichanga kiasi cha milioni tatu kwa ajili ya harambee iliyopitishwa ukumbini hapo naye hakuweza kunipa taarifa zozote zile baada ya muda nikimpigia simu anakuwa hapokei nikibadili namba akipokea ananiambia yuko Nairobi nimsubiri harudi aje aniludishie fedha zangu kitu ambacho ajatekeleza hadi leo hii’ alidai Benson.
Katika kuendelezea kusimulia Benson hakuishia hapo alisema kuwa amefanya jitihada nyingi sana za kutaka angalau aludishiwe kiasi cha fedha zake alizozitoa lakini imeshindikana kilichobaki suala hili kulifikisha Mahakamani.
‘Mi naona Mahakama ndio itakayoamua hatima ya suala langu kwani nimevumilia zaidi ya miaka mitano bali ya kupata ufumbuzi wowote’
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo gazeti hili liliwasiliana na Jane Miso ambapo baada ya muandishi kujitambulisha na kisha kumsomea mashtaka yake alidai kuwa yuko kwenye basi akielekea Kahama kwa hiyo si vizuri kuzungumzia suala hilo akiwa safarini.
‘Ngoja nifike nitakupigia tuongee vizuri’ alisema Jane.
Baada ya kama dakika tano Jane alipiga simu na kuuliza huyo mdai wake yupo hapo ofisi za mtandao huu, lakini  alitakiwa ajibu tu madai yanayomkabili siyo kujua huyo mtu yupo au la matokeo yake Jane hakuwa muwazi kwani hakuweza kukubali wala kukataa.
Mtandao huu unakuhaidi kufuatilia kwa undani suala hili na kisha kukuletea taarifa kamili juu ya sakata hili.

Newer Posts Older Posts