LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

NDOA YENYE FURAHA

Ndoa ni nini? Ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke unaokubalika kiutamaduni na kidini ambao unatarajiwa kudumu, kuwapa haki sawa za kijinsia na kutosheleza majukumu mengine ya kijamii. Katika ndoa kuna uhalali wa watoto.
Pamoja na tafasiri hiyo ya ndoa, watu wengi siku hizi wamekuwa wakiishi maisha ya ndoa kama fasheni hali ambayo imekuwa ikishusha hadhi ya ndoa. Si jambo la ajabu kusikia ndoa iliyofungwa wiki moja iliyopita imevunjika baada ya wanandani hao kutwangana makonde.
Katika ndoa kuna matabaka mawili. Tabaka la kwanza ni kwa wanandoa kufurahia ndoa yao na tabaka la pili ni la wanandoa kuijutia ndoa yao. Hakika ndoa inaraha sana na nitendo la heshima mbele za Mungu.

Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini siku ya harusi wanandoa wote huwa na furaha? Na je, furaha hiyo baadaye hupotelea wapi? Hakuna mwanandoa yeyote ambaye huwaza kama siku moja yeye na mwenzi wake wanaweza kukorofishana na kutukanana matuzi mazito ambayo hugeuka kuwa sumu ndani ya ndoa yao.

Siku ya harusi kila mmoja huisubiri kwa shauku kubwa na kuona siku kama haziendi ili wanandoa hao wawe pamoja katika jahazi la ndoa ya maisha. Lakini mambo hubadirika kwa baadhi ya wanandoa pindi wanapoanza maisha ya pamoja. Kabla sijaendelea naomba kukuuliza wewe uliyendani ya ndoa, je ulishawahi kujiuliza ni kwanini furaha mliyokuwa nayo wakati hamjaoana leo hii haipo hivyo? Kumbuka mara nyingi penzi linalotolewa wakati wa uchumba huwa lina mbinu nyingi za kusomana tabia na kila mmoja hupenda kuficha tambia yake mbaya aliyonayo. Ni suala gumu kigodo kwa wanandoa ambao kila mmoja amekulia katika malezi tofauti kukaa na kujenga tabia moja. Wakati watu wanapokuwa katika hatua ya uchumba hushindwa kusomana vizuri tabia zao kutokana na umbali walionao. Kwa sababu kila mmoja anakuwa kwao ama kwake hali ambayo hutoa muda mwingi wa kumkumbuka mpenzi wake.( Ama hakika ndoa ni furaha, Kabula akitamka maneno ya ahadi mbele ya mashahidi kanisani huku taaaratibu akimuvisha pete ya ndoa mme wake mpendwa tayari kwa kuanza safari ya maisha ya ndoa yeye raha teeeeele!)Kipindi hicho wachumba hao hutumiana jumbe fufi kupitia mitandao kama simu na email ili kila mmoja kuonyesha ni kwa jinsi gani anampenda mwanandani wake mtarajiwa. Wahusika hao hujitahidi kutumika maneno mazuri na yenye kuvutia hisia ya mahaba hali ambayo uzidi kuongeza penzi kwa pande zote mbili. Maneno hayo huongeza shauku kwa walengwa hao kuwa na shauku ya kuwa pamoja wakidhani kuwa siku zote mambo yatakuwa hivyo.
Kwa kipindi hicho wachumba hao huwa wanaelewana kwa kila jambo wanalopenda lifanyike. Utamu wa uchumba huo kama nilivyosema hapo awali hunogeshwa na umbali uliopo kati ya wahusika hao. Wakati mwingi mmoja wapo anapotakiwa na mwenzake wakutane sehumu wanayoona inafaa kwa ajili ya mazungumzo yao ya faragha hulazimika kuwadanganya wazazi wao ama ndugu zao wanaoishi nao kwamba wanaenda kwa jamaa zao na atachelewa kurudi.

Na pindi mazungumzo yao yanapoanza huku muda ukizidi kwenda wachumba hao hutamani muda urudi nyuma ili waendelee kuongea na kupeana habari za hapa na pale kuhusu maisha yao ya badae. Sasa shauku hiyo ya kuwa pamoja hupotelea wapi baada ya kuoana ambapo huwa kuna muda mrefu wa kuwa pamoja tofauti na kipindi kile walipokuwa wanaona muda unaenda na mazungumzo yao bado yanaendelea?

Nadhani utaungana na mimi kwamba kwa baadhi ya wanandoa mambo hayo hupotea pindi wanapoingia ndani ya ndoa kutokana na muda mwingi kuwa pamoja. Utakuta wanaongea masuala yao mpaka yanaisha. Na kisha wanalala. Siku zote mwanadamu hakosi kuwa na madhaifu maishani mwake. Kipindi hicho wanandoa hujikuta wapo katika wakati mugumu pindi mmoja wapo anapofanya kosa hata si kwa makusudi. Inawezekana akawa ni mama akawa mkorofi ama baba ama wote kwa pamoja. Na hiyo hutokea kila mmoja kujiona anahaki ya kufanya atakavyo na hayupo tayari kukosolewa.

Ni imani yangu kuwa kila mwanandoa siku ya kufunga ndoa huwa kunaviapo ambavyo hutamkwa na wahusika wote. Kwamba watakuwa tayari kuishi katika maisha ya raha na shida, iwe magonjwa nk. Lakini mambo huwa sivyo pindi safari ya maisha ya ndoa yanapo anza.

SUMU YA MAISHA YA NDOA

Hakuna asiyefahamu kwamba asilimia kubwa ya vitu tunavyovitumia vina sumu. Lakini hatuoni madhara ya sumu hiyo kutokana na kufuata taratibu za matumizi na vitu tunavyovitumia. Mfano mzuri ni dawa ya panado ambayo mtu anapoumwa kichwa hutumia dawa hiyo ili kuondoa maumivu hayo. Na dawa hiyo huwa haitoi madhara yoyote. Lakini dawa hiyo ukinywa kinyume na masharti yake lazima madhara uyapate kama si kufa tambua utaugua zaidi. Nimetoa mfano huo ili unielewe vizuri kwamba na katika ndoa kuna mambo ambayo yasipofanyiwa kazi huleta madhara katika ndoa.(Ndoa ni furaha mama huyu anamvisha pete ya ndoa mmewe huku akionyesha tabasamu kubwa akiashiria maisha yenye raha teeeeele)
Mambo hao kwanza kabisa ni heshima, upendo wa dhati, mawasiliano mazuri katika familia, kusaidiana na Uvumilivu. Haya ni mambo muhimu sana kwa wanandoa. Kumbuka kwamba wanandoa wanaokosa mambo hayo muhimu ndoa yao lazima iwe mashakani na ugomvi hauwezi kuisha kamwe.

Kwa wanandoa upendo unapotawala ndani ya nyumba huifanya ndoa hiyo kuchanua kila mara na hiyo huambatana na uvumilivu.

Neno jingine ambalo wengi huliona kama halina maana ni SAMAHANI pindi mmoja wenu anapokosea. Inapotokea ukamkosea mwenzako jitahidi kuomba samahani badala ya kukaa kimya na ukifanya hivyo itaonekana unadharahu. Ukiyazingatia yote hayo ni lazima ndoa yako iwe na furaha siku zote.

Kwa leo niishie hapa baada ya hapa nitakulete sababu za mwanamke kwenda nje ya ndoa, na kisha mwanaume naye kwenda nje ya ndoa. Nakaribisha maoni na ushauri juu ya yale uliyoyasoma hapo juu. Pia na wewe unaruhusiwa kutoa somo ama kufundisha jambo lolote ulilonalo kwa ajili ya faida ya sisi tusiojua.

Newer Post Older Post

One Response to “NDOA YENYE FURAHA”

Unknown said...

Bwana Yesu asifiwe,kwa hapo sina cha kuongezea kwani umeongea umemaliza yote,kazi yako nzuri Mungu akuzidishie hekima zaidi ya kuandika mada kali kama hzo.
Unaweza kupitia na blog yangu
www.gshayo.blogspot.com
uwe na wakati mzuri.