LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013
WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.
JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA
KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.
ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.
IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404
REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI
Waumini Wakristo ulimwenguni kote kesho watasherehekea Sikukuu ya Pasaka ya kukumbuka ufufuko wa Bwana Yesu Kristo. Katika Sikukuu hii Wakristo na wale wasio Wakristo wanakumbuka mateso, kifo na Kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo.
Kwa baadhi ya madhebu ya Kikristo, Sikukuu ya Pasaka hutanguliwa na maandalizi makubwa ambayo huchukua muda wa majuma sita ya Kwaresma.
Katika kipindi hicho cha Kwaresma Waumini wamekuwa wakihimizwa kufanya toba kwa kusali zaidi, kuhimizwa kufanya matendo mema mbalimbali na hasa kuwasaidia maskini na wale wote wasiojiweza.
Biblia kupitia Mtume Paulo inawaambia Wakorinto kuwa "Kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu." (1Wakorinto 15:17). Au pia anasema kuwa kama Kristo hakufufuka, basi kuhubiri kwetu ni bure; na imani yenu ni bure (1Wakorinto 15:14).
Pamoja na baadhi ya Wakristo katika hali ya mfungo na kutubu dhambi zao, miongoni mwao wamejiandaa kufanya vitu vya ajabu ambavyo ukiviangalia ni sawa na kwamba ni heri wasingefunga kwa sababu hujikuta wanaibua dhambi kubwa zaida kuliko ilivyokuwa mwanzo.
Hali hii inatokana na mmomonyoko wa maadili katika jamii ambapo watu wengi wamekuwa na imani kuwa, siku hiyo ni yakufanya starehe chafu ambazo mwisho wa siku huwaacha katika majuto na simanzi kubwa.
Kwa muda wote huo baadhi yao wameshona nguo ambazo wakizivaa ni vituko katika jamii, miongoni mwao wamejiandaa kunywa kunywa pombe kupita maelezo, wengine wamepanga bajeti za kutoka out na wake za watu, wachumba kwenda kufanya tendo la ndoa kabla ya muda na vitu vingine vingi vya anasa.
Cha kusikitisha zaidi kuna maadhi ya wanakwaya tayari wameshapanga sehemu ya kwenda kutembea kesho mara baada ya ibada kwa lengo la kufanya ngono. Kana kwamba hiyo haitoshi kuna wengine tayari wameshapanga jinsi ya kuwadanyanga waume/wake zao, wazazi wao, ndugu zao kwa lengo la kwenda kufanya uchafu huo.
Nakatika siku ambazo maambukizi ya virusi vya ukimwi huongezeka kwa kasi ni katika Sikukuu kama hii. Ushauri kwa leo ni kwamba, kwa wanandoa tulieni na familia zenu, baba tulia na mkeo na wewe mama tulia na mumeo mfurahie wote kwa pamoja. Siku ya kesho si ya kunywa pombe la kulewa kwani mwisho wa siku wahusika hujikuta wako katika majuto makubwa. Kwa ndugu zangu waimbaji wa muziki wa injili nawaomba muwe na hofu ya Mungu kwa kuogopa kufanya yasiyompendeza Mungu kwa kufuata mkumbo wa wamataifa ambao wao huitumia siku kama ya kesho kufanya ufusika usiotamkika kwa baadhi yao kupelekana beach.
Kwa wakristo wote nawaomba pia nanyi muwe na hofu ya Mungu, jambo ovu ambalo umepanga kulifanya kesho kwa siri elewa Mungu anakuona kuliko huyo ambaye utamficha kwa madai ya kufanya hivyo kwa kificho. Kikubwa kila mmoja awe na hofu ya Mungu, tambua unaweza kufanya jambo hilo ambalo umekusudia kulifanya na baada ya muda Mungu akakuita, je nani utamlaumu?
Kikubwa tusifanye yasiyompendeza Mungu kwa kificho kwa madai ya watu wasikuone, bali elewa kwamba Mungu mwenyewe ambaye ndiye mtoa hukumu anakuona. Wewe uliyejiandaa kufanya maovu kwa kutegemea badaye uje utubu, nasema unajidanganya. Mungu anaweza kukuchukua wakati ukiwa katika tendo hilo unalofikiria kulifanya.
KAMA UNA HABARI NA MATUKIO MBALIMBALI POPOTE DUNIANI TUMA KWA EMAIL HII. productiongmk@gmail.com. NAMI NITAZIWEKA KWENYE BLOG HII BILA GHARAMA YOYOTE. NAKARIBISHA HABARI ZA MATAMASHA YA INJILI, MIKUTANO, RATIBA ZA MAKANISA, SEMINA, HARUSI NA MAMBO MBALIMBALI KWA AJILI YA KUWAJULISHA WANAULIMWENGU. WASILIANA NAMI KWA NAMBA ZIFUATAZO. +255 712 001 880, +255 755 240 136.
Post a Comment