JOSEPH MAPUNDA KUZIKWA LEO
Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Duru za Michezo kupitia Wapo Radio FM, Joseph Mapunda anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Chang’ombe Maduka Mawili Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Habari kutoka kwa mdogo wa marehemu, Ziko Mapunda zilisema kuwa, mwili wa marehemu utachukuliwa katika hospitali ya Temeke saa 5 asubuhi kisha kupelekwa nyumbani kwake Mtoni Kijichi.
Ziko alisema, ibada ya kumuombea marehemu itaanza saa 7:00 mchana kabla ya kuagwa na kwenda kuzikwa katika makaburi hayo. Joseph Mapunda alifariki dunia Jumamosi iliyopita baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu na uvimbe tumboni uliokuwa unatoa usaa.
Post a Comment