MWAKALUKWA AWAKUNA WAKAZI WA KYELA
Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Amon Mwakalukwa mwishoni mwa wiki iliyopita aliwakuna wakazi wa Kyela baada ya kuimba vibao vya albamu yake mpya ya Matatizo Hayana Mwenye anayotarajia kuizindua hivi karibuni.
Umati mkubwa wa watu waliomiminika katika ukumbi wa Unenamwa Inn uliopo Kyela ulianza kuulizana juu ya ujio wa mwimbaji huyo mwenye maskani yake Mbagala jijini Dar es Salaam kama kweli ataimba na mara baada ya kumuona walisimama na kuanza kumshangilia.
“Tunapenda uimbaji wa Mwakalukwa kwani nyimbo zake ni nzuri na kila ninapozisikia huwa nabubujikwa machozi ya furaha ninapokumbuka mapito ninayopitia hivyo wimbo wake huo umefanyika faraja kwangu,” alisema mmoja wa shabiki wa mwimbaji huyo.
Mwimbaji huyo alikuwa wilayani Kyela kwa mwaliko maalum wa kwenda kuimba katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji mwenzake Saimon Mwakalukwa.
Post a Comment