LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

MTUME WA UREJESHO PETER NYAGA KUENDELEZA KUNJA LAANA LEO

Mtume wa urejesho wa kanisa la RGC Miracle Center Tabata Chang’ombe  Peter Nyaga leo ataendelea na harakati za maombezi ya kuvunja laana, umasikini, ndoto mbaya kwa watu watakaofika katika kanisa hilo. Akizungumza na Tanzania Gospel Music muda mfupi uliopita  Mtume Nyaga amewataka wakazi wote wa jijini la Dar es Salaam kuwahi kufika katika ibada itakayoanza saa 2:00 asubuhi na kumalizika saa 6:00 kabla ya kuanza ibada ya jioni. Mtume huyo wa urejesho alisema kuwa katika ibada hiyo pia atauza vitabu vyake vya Nguvu ya Pesa na Utajiri.

SEMINA YASOGEZA MBELE TAMASHA LA INJILI



               Mwinjilisti Kabula George

Semina iliyoandaliwa ghafla na viongozi wa kanisa la Moravian Usharika wa Yerusalem mkoani Mbeya umesababisha kusogezwa mbele tamasha kubwa la muziki wa injili lililokuwa lifanyike Julai 21,2013 mkoani humo na sasa litafanyika  Agosti 4  kwenye ukumbi ambao utangazwa wiki ijayo. Mratibu wa tamasha hilo, George Kayala amesema leo kuwa taarifa za kutumika kwa ukumbi huo semina ya vijana alipewa juzi na kusababisha usumbufu baada ya kukosa eneo mbadala la kufanyia shughuli hiyo. “Juzi nilipigiwa simu na wenyeji wa kanisa hilo wakisema siku hiyo kutakuwa na semina ya vijana hivyo haitakuwa rahisi kufanya tamasha hapo hali ambayo imenipa hasara kubwa baada ya kukosa eneo mbada na tayari nilikuwa nimekamilisha maandalizi yote kwa aiili ya siku hiyo,” alisema Kayala. Mratibu huyo aliendelea kusema kuwa mbali na kupata hasara ya awali baada ya kulisogeza mbele tamasha hilo anaamini hatawaangusha Agosti 4 mwaka huu kwani atafanya maandalizi mazuri na yenye kufurahisha. “Pamoja na kupata hasara hiyo bado namwamini Mungu baada ya kulisogeza mbele nitafanya maandalizi mazuri zaidi ili kila mmoja apate kufurahia na ninawaomba radhi wadau ambao walikuwa wamejiandaa kwa tarehe 21 mwezi huu,” alisema Kayala. Kayala alisema kuwa bado anakaribisha wadhamini wa tamasha hilo na sasa waliojitokeza ni  Ushindi Redio FM ya Mbeya, RGC Miracle Center Tabata Chang’ombe, Shalom Production, DD Entertainment,  The Genesis Global College na Eck Production. 

Kampeni ya Komesha Uchawi na Mchawi… Mwanamke ajifungua kiloba cha shanga *Asimulia shetani alivyofunga tumbo lake

 Nabii Suguye akifanya maombezi
Kampeni ya Komesha Uchawi na Mchawi Lete Roho kwa Yesu inayoendeshwa na Nabii Nicolaus wa huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) iliyopo Matembele ya pili Kivule imeendelea kuwa mkombozi kwa watu baada ya mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Demetria kujifungua kiloba cha shanga. Akisimulia mkasa huo ndani WRM, Demetria alisema kuwa kabla ya kufika hapo alikuwa haoni siku zake takribani miaka mitano na kuombewa na watumishi mbalimbali bila mafanikio huku tumbo lake likiwa linauma kana kwamba ana mchango.
Demetria alisema hali hiyo ilimtesa muda mrefu hali iliyosababisha akate tamaa na kwa kujua kuwa hakuna njia mbadala ya kutatua tatizo hilo lakini alipata nguvu ya kufika WRM na bahati nzuri akakutana na mkono wa Mungu kupitia Nabii Nicolaus na kupata muujiza wake.
“Jamani ninalia kwa furaha kwani Mungu wa WRM amenifungua vifungo vyangu. Nina kama miaka mitano sioni siku zangu na sikujua tatizo nikaenda kwa watumishi mbalimbali wa Mungu kwa ajili ya maombezi lakini sikupata uponyaji huku nikiteseka kwa tumbo kuuma kama nina mchango.
“Cha ajabu baada ya kusikia kampeni hii nikaamua kufika na kweli nilikutana na mkono wa Mungu kwani baada ya kufika nyumbani usiku wa manane tumbo la uchungu lilianza kuuma wakati sina mimba na nikawa katika hali ya kujifungua na kweli nikajifungua kiloba kilichojaa shanga.
“Nilishtuka sana kuona kitu hicho na baada ya kujifungua ndipo nikaanza kuziona siku zangu na kutambua kuwa kweli kampeni hii si ya kawaida. Namshukuru Mungu wa Nabii Nicolaus kwa kuniponya na tatizo hili,” alisema Demetria.
Wakati huo huo Mwamini Richard amefanikiwa kupata watoto mapacha baada ya kukaa kwenye ndoa miaka mitano bila kishika ujauzito hali iliyopelekea kuanza kuchukiwa na baadhi ya ndugu wa mwanaume.
Akisimulia muujiza huo, Mwamini alisema kuwa alifika WRM akiwa kama kujaribu bahati yake ya kunasa mimba na wakati wa maombezi jicho la Mungu kupitia Nabii Nicolaus lilimuona na kumuambia kuwa atapa mimba na atajifungua mapacha wakiume jambo ambalo kweli limetimia.
“Namshangaa Mungu wa WRM, nilifika hapa kama kujaribu bahati ya kupata mimba kwani nilitukanwa sana. Lakini wati nabii naombea watu alipofika kwangu alisimama na kuniambia Mungu amesikia kilio changu nitashika mimba na nitajifungua macha wa kiume na kweli imekuwa,” alisema Mwamini.
Kampeni hiyo inaendelea leo Nabii Nicolaus atawaombea watu wenye uhitaji wa kazi, biashara, makampuni na amewataka walengwa kufika na vyeti vya usajili wa makampuni, biashara, funguo za magari kwani Mungu kuna kitu ataenda kufanya.

MTUME WA UREJESHO PETER NYAGA KUVUNJA LAANA LEO

Mwangalizi wa kanisa la RGC Miracle Cente Tabata Chang’ombe, Mtume wa Urejesho Peter Nyaga leo ataongoza maombezi ya kuvunja laana, umasikini, ndoto mbaya ili kupokea Baraka katika kanisa hilo kuanzia saa 2:00 mpaka saa 6:00 mchana. Akizungumza na Tanzania Gospel Music jana jioni, Mtume Nyaga amewataka wakazi wote wa jijini la Dar es Salaam na vitongoji vyake kufika kwa wingi katika maombezi hayao. 

KAMPENI YA KOMESHA UCHAWI NA MCHAWI LETA ROHO KWA YESU Umati mkubwa wa watu wafunguliwa nguvu za giza *Wachawi watajana mbele ya madhabahu *Wakiri kuelemewa na nguvu ya Mungu kupitia Nabii na Askofu Suguye


Dada huyo ambaye jina lake halikujulikana mara moja akilia kwa uchungu wakati wa maombezi ya kukomesha uchawi.
Jumapili iliyopita itabaki kuwa ya historia kwa umati mkubwa wa waamini waliofika katika huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) baada ya wachawi kuanza kutajana waziwazi mbele ya madhabahu hiyo huku wengine wakikiri kuelemewa na nguvu ya Mungu kupitia Nabii na Askofu Nicolaus Suguye.
Wakizungumza na gazeti Tanzania Gospel Music jana  mara baada ya maombezi yaliyofanyika ibada ya kwanza naya pili chini ya Nabii na Askofu Suguye waamini hao walisema kuwa kampeni hiyo iwe ya kudumu kwani imeonekana kuwa mkombozi kwa watu wengi walioteswa na shetani kwa muda mrefu.
“Hii itabaki kuwa historia kwa wakazi wa Kivule hasa waaamini wa huduma hii ya WRM kuona wachawi wakitajana waziwazi mbele ya madhabahu juu ya kazi wanazozifanya nyakati za usiku na kufunga maisha ya watu mbalimbali,” alisema mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maria Mwaibale.
Naye Joseph John alisema kuwa ametembea katika huduma nyingi lakini hajawahi kukutana na nguvu ya Mungu kama aliyoiona WRM nay eye binafsi alifunguliwa nguvu za giza ambazo zimekuwa zikimtesa kwa muda mrefu.
“Muda mrefu nilikuwa namsikia Nabii Suguye kupitia vyombo vya habari juu ya nguvu ya Mungu aliyonayo juu ya watu waliofungwa na nguvu za giza. Niliposikia kampeni hii niliamua kufika kuona kama kweli naweza kufunguliwa vifungo vyangu, hakika kweli huyu ni mtumishi wa Mungu aliyeitwa kwani niko huru kabisa,” alisema John.
Tangu kampeni hiyo ianze mwezi uliopita shuhuda za watu wengi wanaofunguliwa nguvu za giza zimekuwa nyingi na Jumapili iliyopita ilikuwa na aina yake kwani wachawi wengi waliumbuka kwani walikuwa wanatajana huku wengine wakiaga na kusema kampeni hiyo imefanikiwa kuharibu kazi zao.
Kampeni hiyo inaendelea tena kesho Jumamosi chini ya Nabii Suguye na Manabii wadogo na watenda kazi wengine kuhakikisha watu wanafunguliwa nguvu za giza na kuharibu maisha yake.

KAMPENI YA KOMESHA UCHAWI NA MCHAWI LETE ROHO KWA YESU WACHAWI WAZIDI KUUMBULIWA WRM *Mtoto aliyechukuliwa sehemu zake za siri k wa njia ya kichawi aombewa na kurejeshewa *Mama yake mzazi asimulia jinsi alivyotabika baada ya mkasa huo

Waamini wa WRM wakisikiliza ushuhuda wa mama (pichani hayupo) ambaye mwanaye sehemu zake za siri zilichukuliwa kichawi

Kampeni ya Komesha Uchawi na Mchawi Lete Roho kwa Yesu inayoendelea katika Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) nchini ya Askofu na Nabii Nicolaus Sugure imezidi kuwauumbua wachawi baada ya awamu hii kurejesha sehemu za siri za mtoto anayekadiliwa kuwa na mwaka mmoja kupotea kimiujiza.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music hivi karibuni ndani ya WRM Jumapili iliyopita, Koreta Soso ambaye ndiye mama mzazi wa mtoto Siloam Steven Soso alisema kuwa mwanaye alimzaa akiwa kawaida na wiki mbili zilizopita ndipo alipata kituko hicho ambacho kiliwashangaza watu wengi.
“Mwanangu nilimzaa kawaida lakini wakati kampeni hii inaendelea katika huduma ya WRM ndipo kilitokea kituko hiki cha mwanangu kupoteza sehemu za siri za kutolea haja ndogo na kuonekana kana kwamba alizaliwa hivyo.
“Tukio hilo lilinikosesha raha nikaamua kwenda hospitali ya Kivule nao wakasema mtoto huyo anatakiwa kufanyiwa upasuaji na kutakiwa kwenda Amana. Kabla ya kwenda Amana nikakumbuka kuwa kuna kampeni ya kukomesha uchawi na mchawi WRM ndipo nikaamua kumpeleka,” alisema Koreta.
Koreta aliendelea kusema kuwa baada ya kufika WRM aliwakuta watenda kazi na kuwasimulia tukio hilo nao wakamwangalia na kushtushwa na tukio hilo kwani mtoto huo hakuwa hivyo siku za nyuma.
Mama Siloam alifika kwa Askofu na Nabii Suguye na kufanyiwa maombi kisha akaambiwa kuwa aende Amana na akifika huko asikubali kufanyiwa chochote kwani tayari Bwana ameshafanya.
Mama huyo aliendelea kusema kuwa alipofika Amana madakitari walipomuangalia wakasema anatakiwa kufanyiwa upasuaji haraka na kuitwa daktari wa upasuaji lakini katika hali ya kumtukuza Mungu wa WRM wakati daktari anafanya ukaguzi sehemu hiyo ya siri ikaonekana.
Huyo ndiye Mungu wa WRM ambaye anafanya miujiza ya ajabu kwa kuwaumbua wachawi jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo iliendelea Alhamis na jana Jumamosi na leo inaendelea kwa lengo la kuwakomboa watu wanaoteswa na nguvu za giza.

FURAHA ISSAYA KUJA KIVINGINE


Furaha Issaya akiwa studio
Baada ya kukaa kimpya kwa muda wa miaka sita, mwimbaji wa nyimbo za ainjili nchini, Furaha Issaya aliyevuma na kibao cha Nina Jua Neno Moja ndani ya albamu ya kwanza iliyojulikana kama Usiogope amereje tena studio kurekodi albamu ya pili.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music leo jijini Dar es Salaam, Furaha alisema kuwa albamu hiyo ataipa jina la Sema Nami na kazi hiyo anaifanyika katika studio ya Eck Production na amewataka wadau wa muziki huo kuwa tayari kuipokea.
“Nimeamua kuja kivingine baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu nikisubiri maelekezo ya Mungu kwamba nitokeje. Nawaomba mashabiki wangu kukaa mkao wa kuipokea albamu yangu mpya ambayo naamini itakuwa kali kuliko ya kwanza,” amesema Furaha.

MWIGULU NCHEMBA MGENI UZINDUZI WA HESABU BARAKA

Mwigulu Nchemba

Mbunge wa Iramba Magharibi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albam ya pili ya mwimbaji wa nyimbo za  injili nchini, Joyce Mwaikofu itwayo Hesabu Baraka utakaofanyika Agosti 4 mwaka huu ndani ya kanisa la EAGT Kipunguni A Ukonga Banana barabara ya Kitunda ikiwa katika mfumo wa DVD.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music jana jijini Dar es Salaam, Joyce ambaye ni mwanasheria wakili alisema kuwa, Nchemba amekubali kuizinduzi albam hiyo iliyokuwa izinduliwe Julai 28 mwaka na lengo nikupata  fedha za kununulia vyombo vya muziki na nyingine kumalizia ujenzi wa kanisa hilo linaloongozwa na mmewe mchungaji John Mabega.
 “Nchemba amekubali kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa albam yangu ya pili na nina amini kuwa uwepo wake utawezesha kupatikana kwa fedha ambazo zitanisaidia kununulia vyombo vya muziki vitakavyotumika kanisani pamoja na kumalizia ujenzi wa jengo la kanisa hilo ambao umesimama kwa sasa,” alisema Joyce.
Akizungumzia mabadiliko ya tarehe ya uzinduzi huo kutoka Julai 28 mpaka Agosti 4 mwaka huu mama mchungaji huyo alisema kuwa imetokana na Nchemba kupata dharura na kuomba usogezwe mbele naye hakuna na kipingamizi na kuwaomba radhi mashabiki wake kwa sumbufu utakaojitokeza.
 Joyce alisema kuwa uzinduzi huo ambao hautakuwa na kiingilio utasindikizwa na wakali wa nyimbo za injili ambao atawataja wiki ijayo kutokana na sasa kuwa katika mazungumzo ya mwisho na wameonyesha hali nzuri ya ushirikiano wa kufika katika shughuli hiyo itakayoanza saa 7:00 mchana.

MWINJILISTI KABULA: NITAING’ARISHA MBEYA JULAI 21


               
MWIMBAJI wa nyimbo za injili nchini Mwinjilisti Kabula George amesema kuwa atainga’ara Mbeya  siku ya tamasha la kuitambulisha albamu yake ya Nitang’ara litakalofanyika katika kanisa la Moravian Usharika wa Yerusalem Airport.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music leo muda mfupi uliopita, Mwinjilisti Kabula amesema kuwa hii ni mara ya kwanza kutoa huduma katika mkoa wa Mbeya hivyo atahakikisha anaweka historia katika fani ya muziki huo.
“Nitaing’arisha Mbeya Julai 21 mwaka huu katika tamasha la kuitambulisha DVD yangu ya Nitang’ara Tu. Nipo katika mazoezi makali kwa ajili ya kuwafurahisha Wanambeya watakaofika katika shughuli hiyo.
Tamasha hilo litanogeshwa na wakali wa muziki huo kutoka mikoa mitatu ya Tanzania Bara wakiongozwa na  Ambele Chapanyota,Christina Shusho, Enock Jackson na wengine wengi.
Mratibu tamasha hilo George Kayala  alisema kuwa kiingilio katika tamasha hilo kitakuwa elfu 1000 kwa wakubwa na 500 kwa watoto ili kuwawezesha watu wengi kufika kushuhudia tamasha hilo.
“Tumeamua kuweka kiingilio kidogo ambacho kitamuwezesha kila mmoja kuingia kushuhudia tamasha hilo ambalo tunaamini litaweka historia mkoani hapo, kwani pia ni mara ya kwanza kwa mwinjilisti Kabula kutoa huduma mkoani hapo,” alisema Kayala.
Tamasha hilo linadhaminiwa na , Ushindi Redio ya Mbeya, GMK Production, RGC Miracle Center Tabata Chang’ombe, Shalom Production, Mbeya Yetu blog, Tanzania Gospel Music blog na The Genesis Global College. 

STELLA JOEL KUFANYA KWELI DAGI, ARUSHA

Stella akifanya zoezi kabla ya kuelekea Arusha

Stella Joel ameahidi kuimba vibao vyake vyote vikali katika mkutano wa injili unaotarajiwa kufanyika Julai 13,2013 katika kanisa la Deliverance Assemblis of God International (DAGI) TZ lililo chini ya Mtume na Nabii Zephania J Mollel lililopo mkoani Arusha.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music leo asubuhi, Stella amesema kuwa kwa sasa yupo katika mazoezi makali ikiwa ni maandalizi ya kuweka sauti yake vizuri kabla ya kuanza safari.
“Nipo kwenye mazoezi makali nikijiandaa na mkutano wa siku saba ambao umeandaliwa na mtumishi wa Mungu aliyejawa na miujiza ya Yesu,  Mtume na Nabii Zephania J Mollel na nitaimba vibao vyangu vyote vikali,” amesema Stella. 

MATENDO AKAMILISHA ALBAM YAKE YA KWANZA

Matendo Andrew Mgeni  wakati anarekodi albam yake

Mwimbaji chipukizi wa nyimbo za injili nchini, Matendo Andrew Mgeni amekamilisha albam yake ya kwanza ambayo bado hajaipa jina ikiwa na vibao vinane.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music leo asubuhi, Matendo alisema kuwa nyimbo zote ni nzuri hivyo bado anaangali ni wimbo gani ndiyo ubebe albam.
“Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha kukamilisha albamu yangu ya kwanza katika studio ya Eck Production iliyopo Mwembechai jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa sijapata jina la albam hiyo kutokana na kila wimbo naona unafaa kubeba albamu,” amesema Matendo.

TAMASHA KUBWA LA INJILI KUFANYIKA RGC

Mtume wa urejesho Peter Nyaga


Tamasha kubwa la uimbaji wa muziki wa injili linatarajiwa kufanyika kesho katika kanisa la RGC Tabata Chang'ombe kwa kuwakutanisha waimbaji 250.
Mtume wa urejesho Peter Nyaga alisema kuwa tamasha hilo litaenda sambamba na maombezi ya kuombea amani Tanzania.

KONDA DALADALA ATEKWA NA WAARABU TANDIKA

Gari la konda aliyetekwa

Kondakta wa daladala inayofanya safari kati ya Kariakoo na Tandika ametekwa na watu watu wasiojulikana wenye asiri ya kiarabu maeneo ya Sudani na kutokomea naye na kwenda kumtupa maeneo ya Zakiem Mbagala.
Tukio hilo lilitokea jana baada ya watekaji kuligonga kwa mbele gari hili kasha konda akashuka na kuwauliza sababu za kutenda kosa hilo lakini watu hao walimweleza dereva wa daladala hiyo aitwaye Petro Mwaja na kuwapeleka abiria kituoni kasha arudi wakalinyoshe gari na alipoondoka walimchukua konda na kumwigiza kwenye gari lao dogo na kukimbia naye.
Akisimlia mkasa huo Petro alisema kuwa konda huyo baada ya kuchukuliwa akapigwa na kuumizwa kichwani kisha wakamtupa huko Zakiem na kumuacha akiwa anaugulia. Baada ya kutupwa konda huyo alijikokota na kukodi pikipiki kwa lengo la kuifukuzia gari hilo lakini hakufanikiwa kuikama wala namba zake hakuziona vizuri.
Konda alipelekwa katika hospitali ya Temeke kwa ajili ya kupatiwa matibabu na habari za tukio hilo kuziripoti katikaa kituo cha Polisi Mtongani na Jeshi la Polisi limeahidi kuwasaka watuhumiwa hao.

TAMASHA KUBWA LA INJILI LAANDALIWA MBEYA



Tamasha kubwa la muziki wa  injili limeandaliwa na mwimbaji  wa nyimbo za injili nchini Mwinjilisti Kabula George  na litafanyika katika kanisa la Moravian Usharika wa Yerusalem Air Poirt Mbeya mjini Julai 21 mwaka huu na litaenda sambamba na kuizindua kwa mara nyingi DVD yake ya albamu ya Nitang’ara Tu.
 Akizungumza na Tanzania Gospel Music leo jijini Dar es Salaam, Mwinjisti Kabula alisema kuwa ameamua kuaandaa tamasha hilo kutokana  na wakazi wa jiji hilo kuomba aandae tamasha hilo kutokana na kuzipenda nyimbo zake ambazo zimekuwa zikiwagusa kila wanapozisikiliza redioni.
“Nimeandaa tamasha hilo mkoani  Mbeya baada ya kupokea maombi ya wakazi  wengi  wa Nyanda za Juu Kusini nami nimeona nikubali ombi lao na taratibu zote kwa ajili ya tamasha hilo yanaendelea hivyo naamini wakazi wa mkoa huo watapata kile wanachokitaka,” alisema Mwinjilisti Kabula.
Mwimbaji huyo alisema kuwa tamasha hilo litakuwa na waimbaji wengi kutoka mikoa mbalimbali kama Njombe, Dar es Salaam na wenyeji Mbeya na kuahidi kuacha histoaria nyanda hizo.
“Litakuwa tamasha la kipekee kufanyika katika mkoa huo kwani litawakutanisha waimbaji nyota kutoka katika mikoa mitatu ambayo ni Njombe, Dar es Salaam na wenyeji Mbeya hivyo si siku ya kukosa,” alisema Mwinjilisti Kabula.
Mwinjilisti Kabula alisema pia kuwa siku hiyo kwa mara ya kwanza ndipo ataziuza DVD zake kwa mashabiki wote watakaofika katika uzinduzi huo na anaamini kila mmoja ataondoka na nakala yake halisi.

MCHUNGAJI MWASUBI AMPA MIMBA MWANAFUNZI, ATUPWA JELA MIAKA 35


Mahakama ya rufaa Tanzania
Mahakama mkoani Mbeya imemhukumu kwenda  jela miaka 35 mchungaji  Daniel Mwasubi wa kanisa la EAGT baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Isenga mkoani hapo.
Mahakama hiyo pia imeamru kuchapwa fimbo 12 na kumlipa mwanafunzi huyo bilioni 20 kutokana na kosa la kumharibia masomo msichana huyo. Mchungaji huyo anadaiwa kupanga uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi huyo Desemba mwaka 2008 na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili.
Baada ya kutolewa hukumu hiyo mwanafunzi huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 19 aliangua kilio kwa madai kuwa huyo ni mume wake na alikuwa anamtegemea katika suala la kuwalea wanaye na mahakama hiyo imempa siku 30 mchungaji kukata rufaa kama ataona hajalidhika na hukumu hiyo.

MCHUNGAJI MWASUBI AMPA MIMBA MWANAFUNZI, ATUPWA JELA MIAKA 35


Mahakama ya rufaa Tanzania
Mahakama mkoani Mbeya imemhukumu kwenda  jela miaka 35 mchungaji  Daniel Mwasubi wa kanisa la EAGT baada ya kupatikana na hatia ya kumpa mimba mwanafunzi wa shule ya sekondari Isenga mkoani hapo.
Mahakama hiyo pia imeamru kuchapwa fimbo 12 na kumlipa mwanafunzi huyo bilioni 20 kutokana na kosa la kumharibia masomo msichana huyo. Mchungaji huyo anadaiwa kupanga uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi huyo Desemba mwaka 2008 na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili.
Baada ya kutolewa hukumu hiyo mwanafunzi huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 19 aliangua kilio kwa madai kuwa huyo ni mume wake na alikuwa anamtegemea katika suala la kuwalea wanaye na mahakama hiyo imempa siku 30 mchungaji kukata rufaa kama ataona hajalidhika na hukumu hiyo.

Newer Posts Older Posts