Christina Shusho akanyaga sikendo
Mkali wa Muziki wa Injili Bongo, Christina Shusho amepangua vikali madai yanayovumishwa kila kona ya jijini la Dar kuwa, amekuwa na kijitabia cha kutapanya fedha zake vibaya kwa kufanya matanuzi ambayo kwa hadhi yake hapaswi kuyatenda.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Shusho alisema kuwa, anashangazwa na uvumi huo ambao hauna ukweli wowote bali una lengo la kuinajisi huduma yake ili aeleweke vibaya katika jamii.
“Si kweli kwamba mimi nafanya matanuzi kwa kutumia fedha kama watu wanavyodai, bali naona watu wameamua kunichafua kwa maneno ya uzushi ili jamii inichukie ikiwa sambamba na kuinajisi huduma yangu,” alisema Shusho ambaye ni miongoni mwa waimbaji wachache wa muziki huo ambao wamekuwa wakihesabika kuwa ‘wasafi’.
Mbali na matumizi mabaya ya pesa, msanii huyo anadaiwa kulala kwenye hoteli za nyota 5 punde anaporejea jijini usiku akitoka kufanya shoo zake mikoani.
Wadaku hao walisema kuwa, Mtumishi huyo wa Mungu amekuwa akifanya hivyo kutokana na uwezo mkubwa wa kifedha alionao bila kuangalia kama kuna watu ambao wanahitaji msaada kutokana na maisha magumu wanayoishi hasa wajane na yatima.
Akipangua skendo moja baada ya nyingine, Shusho alikiri kwanza kuwa na safari za kwenda kununua nguo zake nje ya nchi akisema kwa sababu ana duka la nguo Kariakoo.
Aisha, alisema kuwa, yeye ni mwanamitindo hivyo anapokwenda Marekani, Uingereza au China hununyua vitambaa ambavyo vikishonwa na kuvaa huonekana amenunua nguo za gharama kubwa.
“Mimi ni mtu ninayetumika madhabahuni, natakiwa nionekane nadhifu muda wote, na kweli nimekuwa nikisafiri kwenda Ulaya kununua bidhaa za dukani kwangu, na nikiwa huko huwa nanunua kitambaa kimoja kimoja, nikija kushona nguo na kuvaa zinaonekana nzuri na za gharama ya juu na baadhi ya watu hutafsiri kwamba, natumia vibaya fedha zangu,” alisema Shusho.
Akifafanua kuhusu suala la kulala hoteli za gharama nchini anaporeja Dar usiku toka kwenye shoo, Shusho alisema kuwa, jambo hilo halina ukweli wowote kwa sababu ana mapenzi na familia yake hivyo hawezi kufanya kitendo kama hicho.
Mwimbaji huyo alimaliza kwa kusema kuwa, yote hayo anamwachia Mungu yeye ndiye anayejua ukweli wa maisha yake, na masuala hayo anayapeleka kiroho zaidi kuliko kimwili kwani yanaweza kuujeruhi moyo wake.
“Namwachia Mungu masuala hayo, yeye ndiye anayefahamu ukweli wa maisha yangu kwa maana Biblia inasema; Kushinda kwetu si kwa damu na nyama bali ni katika Ulimwengu wa roho, Jehova atalidhibitisha jambo hili kama lipo, na kama halipo wanaovumisha maneno hayo atawashughulikia,” alisema Shusho.
One Response to “Christina Shusho akanyaga sikendo”
You people of Dar(Tz) are strange . This lady is your sister,engaged in winning souls for our Lord Jesus Christ.Why use the media to box her?What is the gain in trampling on her ? Ikindly beg you to lift this lady up for the sake of the gospel-Boaz Nundu,Nairobi -Kenya (boaznund@yahoo.com)
Post a Comment