LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Paul Mgonza: Warembo wasitumie ulimbwende wao kuharibu Injili


PAUL Mgonza ni mtumishi wa Bwana anayemtumikia Mungu kwa kutangaza neno lake kwa njia ya uimbaji wa nyimbo za Injili. Mgonza alianza kuonyesha kipaji cha uimbaji tangu alipokuwa na umri mdogo, alianza kwa kuimba kwanya kanisani kama ilivyo kwa wengi walio katika tasnia hiyo.
Mtumishi huyu anaeleza kuwa kupitia uimbaji wa kumtukuza Bwana na kulitangaza neno lake, umemsaidia kutambua vitu vingi na kujifunza mengi, tangu alipotoa albamu yake ya kwanza ya Yesu ni Bora iliyotengenezwa nchini Uganda na Kenya mwaka 2007.
Mwimbaji huyu anaelezea muziki anaoimba kuwa licha ya kutangaza neno la Mungu, pia ni sehemu ya kujifariji bila kuzingatia dini ya mtu, jambo ambalo anakiri kuwa limekuwa chachu ya kupata mafanikio ya kuenea kwa nyimbo hizo.
Katika kuelezea kukua kwa muziki wa Injili miaka ya hivi karibuni , Mgonza anaeleza kuwa kuna vitu ambavyo vinajitokeza na visipozuiliwa mapema vinaweza kupoteza sifa ya ujumbe wa Injili.
“Huu ni muziki wa kumuimbia Mungu, waimbaji tunatakiwa kufanya vizuri na kufanya mazuri ndani ya mioyo yetu na mbele za uso wa Bwana aliyetupa uwezo huu wa kuimba, tuachane na mambo ya kidunia ambayo hutupoteza na kutuweka mbali na Mungu,” anasema Mgonza.
Hata Hivyo Mgonza anaeleza kuwa katika muziki wa Injili, baadhi ya wanamuziki wake wananakili kazi za wengine pasipo kuwa na rukhsa maalum jambo linalopelekea kufanana kwa vitu vingi jambo ambalo si zuri kwenye kazi ya Mungu.
“Badala ya kumwomba Mungu matokeo yake mtu anakuwa akimdanganya Muumba kama vile haoni kile anachokifanya, hilo ni moja lakini kuna mengi ambayo yanafanywa na waimbaji wa muziki huu kiasi kwamba unajiuliza huyu ndiye mwimbaji au la.
 “Waimbaji tunatumia sauti zetu kumtukuza Mungu, hatupaswi kuonyesha tabia ambazo zitaifanya jamii kudharau na kuishusha kazi yetu kwani kuna baadhi ya waimbaji pamoja na waandaji ambao wanasema wamempokea Bwana lakini hufanya uasherati tena bila kificho chochote,” anasema Mgonza ambaye pia ni mwalimu wa injili.
“Tatizo letu sisi waimbaji tunazuzuka na kuwa na kiburi pindi tupatapo umaarufu, kuna ambao wamekuwa wakihama makanisa lakini binafsi naamini Mungu ni mmoja popote utakapoenda ni yule yule.
Kama wanakutana na wakati mgumu ni vema wakawaona viongozi wa dini wakiwemo wachungaji na wazee wa makanisa, kwakuwa kila mtu anapitia katika wakati mgumu,” anasema Mgonza.
Pia alitoa onyo kwa wanamuziki wa injili wanaochipukia wasiangalie wale waliotangulia mbele yao, bali waangalie Mungu aliyewaita kufanya kazi hiyo kwani kwa kufanya hivyo watapotea, jambo la msingi kumuomba Bwana.
“Nawaambia wasigeuke popote kwa ajili ya kuangalia wapi watapata msaada, Mungu mwenyewe anajua ni mahali gani atakuelekeza na ndiko kwenye mafanikio kwani yeye anajua nini haja zetu, cha msingi ni kumuomba atuonyeshe njia,” anasema Mgonza.
Aidha Mgonza anatoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha sheria ya moja kwa moja itakayoweza kusaidia kulinda haki za wasanii, si wa Injili pekee ambao wamekuwa na kilio hicho kwa muda.
Mwisho anatoa ushauri kwa mabinti ambao wamekuwa wakitamani kuingia katika fani hii ya muziki wa injili, wasitumie mvuto wao katika kutenda dhambi na wasitafute jina kupitia injili kwa malengo la maslahi binafsi bali wautumie kupendezesha kazi ya Mungu.
“Mungu aliumba mvuto kwa mabinti kwa ajili ya kutafuta utukufu wake lakini dada zetu hutumia uzuri huo kwa ajili ya kumkasirisha Mungu kwa kutenda dhambi mimi ningependa wajikite zaidi katika kazi ya Mungu,” anasisitiza Mgonza  ambaye ni baba wa mtoto mmoja.

Newer Post Older Post