LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

ASKOFU SYLVESTER GAMANYWA

CHANGAMOTO ZA MIGOMO NA HATMA YA AMANI YA NCHI (3)

Askofu Sylvester Gamanywa
Katika toleo tulichambua habari kuhusu shinikizo la nje kuwa lina maslahi ya nje na tukajadili jinsi ambavyo amani ya si kipaumbele cha matajiri wa nje. Leo napenda tuingie ndai kidogo kutafakari juu ya dalili za migomo inayoshamiri kutokana na shinikizo kutoka 

Shinikizo kupitia baadhi ya mashirika ya misaada
Kwanza nianze kwa kuonesha moyo wa shukrani kwa mashirika ya misaada kutoka nje ambayo yamekuwa yakichangia bajeti za serikali, na mashirika ya ndani kwa ajili ya huduma za kijamii km afya, elimu, miundombinu, na mazingira. Mara nyingi misaada hii hupatikana kutokana na mahusiano mazuri kati ya nchi yetu na nchi wafadhili.

Baada ya kutambua na kukiri kuhusu uwezesho wa kifedha wa mashsirika ya misaada kutoka nje, napenda sasa kuweka upande wa pili wa sarafu ambao ni changamoto zitokanazo na masharti ya baadhi ya misaada hiyo. Nadhani ni wakati muafaka kujifunza kwamba, misaada ya kifedha haipatikani kwa kuombwa moja kwa moja ati kwa sababu sisi ni wahitaji.

Kila mtoa msaada anayo malengo yake katika kutoa msaada husika. Malengo hayo ya utoaji misaada huambatana na masharti maalum ambayo mtoa msaada hujiridhisha na kutoa msaada husika. Naweza kusema kwamba, hata kuomba msaada kunahitaji ujuzi na uzoefu wa kujua malengo, masharti na michakato inayotakiwa kufuatwa mpaka kupokea au kutokupokea misaada husika.

Nia na madhumuni ya baadhi ya masharti ya misaada yanalenga kuweka udhibiti wa matumizi ya misaada hiyo ipate kufikia maeneo yaliyolengwa kupokea misaada husika. Masharti hayo ni kuwezesha kupatikana taarifa za kweli za mapaot na matumizi ya misaada. Mpaka hapa masharti haya hayana utata hata kidogo.

Utata wa baadhi ya misaada unakuja pale ambapo, baadhi ya masharti yanamshinikiza mpokea msaada kufanya mambo ambayo ni maslahi na matakwa ya mtoa msaada. Halafu maslahi na matakwa hayo yanakuwa hatari kwa mpokea msaada pale yanapoingilia na kuathiri maadili ya kijamii ya muhusika!

Mfano ulio dhahiri ni mazingira ya sasa ambapo kuna shinikizo la baadhi ya watoa misaada wanapodai kwamba ili tupate misaada yao ni lazima tukubaliane na kuhalalisha kisheria ushoga na ndoa za jinsia moja! Tumesikia hivi karibuni jinsi ambavyo baadhi ya nchi za kiafrika zimekwisha kulegeza misimamo na mitazamo yake na wako tayari kuhalalisha mambo yanayoathiri maadili ya kijamii, kwa sababu ya kutaka kuendelea kupokea misaada.

 Kuna baadhi ya nchi, Tanzania ikiwemo bado tunasimama kidete kwa kusema hatuko tayari kupokea misaada inayokiuka utu wetu na maadili yetu. Bado haijulikani kama msimamo wetu huu utaendelea kwa muda mrefu kiasi gani.  Nasema hivi kwa sababu ziko changamoto katika kukataa misaada yenye masharti yenye athari za kimaadili.

Huu ni mfano mmoja tu unaoonesha baadhi ya masharti ya misaada yanavyoweza kuingilia na kusababisha athari kwa maadili ya kijamii na hata kiuchumi kwa mpokeaji.



Shinikizo la nje kupitia taasisi za utetezi na uanaharakati
Hapa nianze kwa kusema waziwazi kwamba, mashirika mengi ya utetezi (Advocacy) na uanaharakati (Activism), yametoa mchango mkubwa katika kuleta mabadiliko makubwa katika nchi mbali mbali duniani, na hata hapa nchini pia. Kuna mambo mengi ambayo si mazuri au mila potofu katika jamii ambazo zimeshughulikiwa kutokana na shinikizo la watetezi na wanaharakati wetu. Pengine nianze kwa kutoa ufafanuzi wa matumizi ya maneno haya ili tujue tofauti zake:

1.    Tofauti kati ya mtetezi (Advocate) na mwanaharakati (Activist)
Ni vigumu kutofautisha maana za maneno haya, kwa sababu matumizi yake huingiliana na kila moja kuchukua nafasi ya jingine. Pamoja na mwingiliano huu, ni muhimu kujua kwamba kimsingi bado kila moja linayo maana yake ya msingi ambayo ni muhimu kuifahamu.

Tukianza na neno hili mtetezi, kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu ni “mtu anayepigania haki au jambo la mtu mwingine ili asionewe; mgombezi” Kwa maelezo mengine tunaweza kusema kuwa ni mtu aliyejitoa mhanga kusema kwa niaba ya mtu mwingine au kundi la watu. Madhumuni ni kutetea haki, kuzuia uonevu dhidi ya wanyonge.

Mtetezi hata kama atajikuta ametumbukia katika mambo yenye utata, bado atazingatia lengo lake la msingi la utetezi kwa kutumia ushawishi wake katika kuwasiliana na wenye mamlaka ya kutunga sera na sheria wakubaliane na utetezi wake na wafanye mabadiliko ya kisera na kisheria.
Kwa upande wa Mwanaharakati. Nikiri kwamba neno hili halijawa rasmi katika Kamusi. Lakini ndani ya Kamusi tuna neno moja lijulikanalo kama Harakati; Tafsiri ya neno harakati ni “juhudi zinazofanywa na watu kwa ajili ya kufikia lengo fulani; mapambano”

Kutokana na matumizi ya neno hili, ndipo tunalazimika kutumia neno hili “mwana-harakati” kwa maana ya mtu mwenye kufanya tendo la makusudi la kutaka mabadiliko ama ya kisiasa au kijamii. Uanaharakati ni harakati au mapambano ya kisaikolojia katika ama kuunga au kupinga jambo fulani. Uanaharaka ni harakati au mapambano ya kisaikolojia katika ama kuunga au kupinga jambo fulani. Baadhi ya vitendo vya ki-harakati ni pamoja na maandamano, midahalo, ikiwa ni pamoja na migomo.
Sasa tukiyachunguza matumizi ya maneno haya tutagundua kuna mahali huingiliana. Kuna maeneo ambayo wanaharakati hufanya utetezi wenye ushawishi kwa mamlaka za kubadili sera na sheria; na pia watetezi kujikuta katika mazingira ya kuunga mkono au kuwahamasisha wale waliokuwa wakiwasemea nao wajitetee wenyewe kwa kufanya vitendo vya ki-harakati.



2.    Madhumuni ya awali kwa uanaharakati na utetezi
Tukifuatilia historia ya utetezi na uanaharakati, hapo mwanzoni yote yalilenga kutetea na kulinda haki za kimsingi za binadamu. Kazi na vitendo vyake vililenga kuleta mabadiliko ya kisera na kisheria katika jamii ili kupambana na kufuta ubaguzi, upendeleo, ukandamizwaji na unyanyaswaji wa binadamu uliomo katika jamii kwa misingi ya rangi, dini, jinsia, tabaka za kiuchumi na kimaeneo.
Kwa nyakati tofauti na vizazi tofauti, kila mtu kwa sehemu yake, na kiwango chake ameshiriki katika utetezi na uanaharakati uwe wa kisiasa, kijamii, kiuchumi, na hata kidini! Na walio wengi katika ushiriki wao ulitokana na uchungu na shauku ya kuona mabadiliko yanayofanyika. Mpaka hivi leo, sehemu kubwa ya madhumuni ya utetezi na uanaharakati ni kushinikiza kuwepo kwa mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

3.    Utetezi na uanaharakati unapotekwa nyara
Shughuli za utetezi na uanaharakati haziwezi kufanikiwa kama hakuna fedha za kutosha kugharimia matumizi yake. Changamoto kubwa ni vyanzo vya fedha za kuendesha shughuli hizi. Kwa bahati mbaya, baadhi ya vyanzo vya ruzuku ni mashirika au matajiri wenye ajenda za siri katika kuchangia mapato ya utetezi na u-harakati! Ajenda za siri ni masharti yenye kuambatana na michango ya fedha ambayo huitoa kwa mashirika ya ki-harakati na utetezi.

Itaendelea wiki ijayo

Newer Post Older Post