GETRUDE RWAKATARE AKERWA NA WANENGUAJI WA KANGA MOJA
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblise of God, Mh.Getrude Rwakatare amekerwa na mchezo wa unaoendeshwa na makundi ya Kanga Moja kwa kwa kile alicho dai ni mchezo usio na maadili katika jamii.
Wanenguaji wa Kanga Moja |
Mh.Rwakatare |
Akizungumza jana Bungeni, Rwakatare ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum (CCM) alisema kuwa mbaya zaidi wanenguaji wa makundi hayo hujimwagia maji wakati wa kukata nyonga hali ambayo huwafanya wahusika kuonekana maungo yao ya ndani.
Mbali na hilo, Mbunge huyo alikerwa pia na uvaaji wa nguo fupi sehemu za heshima kama vile maofisini, hospitalini na maeneo yenye kuzingatia maadili ya Watanzania.
Rwakatare amewataka Watanzania kukemea uvaaji wa nguo hizo ikiwa pamoja na wavulana kuvaa nguo za milegezo. Aliwataka Watanzania kuendelea kudumisha maadali ya Tanzania badala ya kuiga kutoka kwa nchi zilizoendelea.
Post a Comment