JOYCE MLABWA: TUSAMEHEANE TUNAPOKOSANA
Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili nchini, Joyce Mlabwa amewataka watu wote kupenda na kusameheana wanapokosana badala ya kujihesabia haki. Akizungumza na TGM hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Joyce alisema kuwa ni vema kila mtu kutoa kwanza kibazi kilicho ndani ya jicho lake ndipo aangalie udhaifu wa mwenzake.
''Toa kwanza Boriti kwenye jicho lako kabla hujaona kibanzi ndani ya jicho la mwenzako!...''Ukitaka kupendwa anza wewe kuwapenda wengine kwanza, ukitaka watu wakujali anza wewe kuwajali wengine kwanza, ukitaka kuheshimiwa anza wewe kuwaheshimu wengine kwanza, ukitaka kusamehewa anza wewe kusamehe wengine kwanza,...tusipende kujihesabia haki,” alisema Joyce.
Mwimbaji huyo aliyetamba na kibao cha ‘Nisalama Rohoni’ miaka ya nyumba amewataka watu wote kuwa kwenye hali ya toba wakati wote ili siku Mungu akimuita awe akakae naye kwenye ufalme wa mbiguni.
Mkurugenzi huyo wa kampuni AJM PRODUCTION ambayo ni changa lakini imeshafanya kazi na kwaya pamoja na waimbaji maarufu Tanzania alisema njia sahihi ya kumpendeza Mungu ni kusamehe kila watu wanapokoseana na kuacha kujihesaba haki.
Post a Comment