CHRISTINA SHUSHO KWA NINI ANANG’ARA ZAIDI KENYA KULIKO WAIMBAJI WENGINE?
Mwimbaji wa muziki wa injili nchini Christina Shusho nyota yake inaonekana kung’ara zaidi nchini Kenya kuliko waimbaji wengine wakubwa kama Bahati Bukuku, Bony Mwaitege, Upendo Nkone, Rose Muhando na wengine wengi.
Mara kwa mara mwimbaji huyo amekuwa akitwaa tuzo ambazo huendeshwa nchini humu. Mfano mwaka huu mwanzoni aliibuka tena kidedea kwenye tuzo za groove zinazotolewa kila mwaka nchini Kenya kupitia kipengele cha mwanamuziki bora wa mwaka kutoka Tanzania tuzo ambayo alishinda mwaka jana akiwapita waimbaji wenzake waliopendekezwa kwenye kipengele hicho akiwemo Rose Muhando,Bahati Bukuku,Neema Mwaipopo pamoja na Boniface Mwaitege.
Kwa Mara Ya Pili Mfululilzo katika Category ya Wanamuziki Kutoka Tanzania, Christina Shusho ametamba tena kwa kutwaa tuzo hizo. Ikumbukwe Mwaka jana 2011 Mwanamuziki Christina Shusho alitwaa tuzo hizo hizo katika Category hiyo hiyo.
Swali, ni staili ya nyimbo anazoimba ama upako wake umekubalika zaidi pande hizo? Maoni yako yatanipa nafasi ya kumuuliza mtumishi huyo wa Mungu.
Post a Comment