JOSEPH MAPUNDA AFARIKI DUNIA
MAREHEMU JOSEPH MAPUNDA (KATIKATI) ENZI ZA UHAI AKIWA NA MENEJA WA WAPO RADIO FM (KULIA) BARIKIEL GADIEL |
Mtangazaji wa WAPO Radio FM, Joseph Mapunda amefariki dunia leo mchana baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kikuu na tumbo.
Habari kutoka kwa mdogo wa marehemu Ziku Mapunda alisema kuwa Joseph alilazwa juzi katika hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata matibabu.
Akizungumza na Kipindi cha Duru za Michezo ambacho hurushwa kila siku za 12:30, mdogo wa marehemu alisema baada kufikishwa katika hospitali hiyo, madaktari walimpima na kubaini anasumbuliwa na ugonjwa wa kifua kiuu na alikuwa na uvimbe tumboni ambao ulikuwa na usaa.
Ziku alisema kuwa leo asubuhi walipoenda kumuona marehemu walimkuta akiwa analalamika kuwa na maumivu makali tumboni la madaktari walikuwa wanajitahidi kuokoa maisha yake lakini ilipofika majira ya mchana leo Mungu alimpenda zaidi.
Joseph alikuwa kiongozi wa kipindi cha michezo kupitia radio hiyo hivyo kifo chake kimeacha pengo kubwa. Msiba upo Mtoni Kijichi maeneo ya Bujunga.
Bwana ametoa, na Bwana ametwaa - Jina la Bwana lihimidiwe.
Post a Comment