LOVE TANZANIA FESTIVAL YAKANA KUFIWA NA WAIMBA INJILI TOKA KENYA
Shirika la Love Tanzania Festival (Ipende Tanzania) la nchini Marekani upande Tanzania limekanusha uvumi ulioenea jijini Dar es Salaam kuwa wanakwaya kadha wamepoteza maisha leo asubuhi katika ajari iliyohusisha magari manne eneo la Makole mkaoni Pwani.
Habari kutoka ndani ya uongozi wa shirika hilo zinasema kuwa hakuna wanakwaya walioalikwa kutoka Kenya hivyo taarifa hizo hazina ukweli wowote.
“Waimbaji wanaoonekana kwenye matangazo yetu ndiyo hao na hatuna waimbaji kutoka Kenya. Habati hizo zimelenga kuharibu tamasha letu,” alisema mmoja wa waratibu wa shirikisho hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe mtandaoni.
Uvumi huo umeanza kuenezwa asubuhi ya leo baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari manne mabasi mawili na malori mawili na kuua watu 11 na 25 kujeruhiwa.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa watu hao waliopoteza maisha wote ni raia wa Kenya.
Post a Comment