MSAMA AKAMATA CD FEKI DODOMA NA DAR ES SALAAM
Msama akionesha kompya zinazotumiwa na maharamia wa kazi wa wasanii mkoani Dodoma jana |
Msama akionesha CD alizokama jana mjini Dodoma |
CD feki alizokamata Msama Buguruni juzi jijini Dar es Salaam |
Kopyuta za maharamia ya kazi za wasanii |
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amefanikiwa kuwakamata watu mbalimbali wakiuuza na kudurufu CD feki katika mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam.
Waliokamatwa kwa Dar es Salaam ni ni Malik Sultan, Ally Msangi, Edward Michael na Sijali Andrew ambao walikuwa na CD feki 322 za wanamuziki mbalimbali hasa wa nyimbo za injili.
Kwa Da es Salaam maeneo yanayoongoza kuuza CD feki ni Ubungo, Manzese, Mwenge na Buguruni.
Msama alisema zoezi la kukamata wezi wa kazi za wasanii linaendelea kwa kufanya uchunguzi katika maeneo sugu ambako hatua inayofuata ni kwa wale wanauza kazi hizo mikononi.
Kwa Dar es Salaam peke Msama amekamata CD feki za wasanii mbalimbali za Tanzania na nje, zenye dhamani zaidi ya Shilingi milioni 25, walizozikamata maeneo ya Buguruni jijini Dar es Salaam juzi.
Jana alendesha zoezi hilo mkoani Dodoma na kukamata Computer zenye thamani ya shilingi milioni Sitini na saba.
Hali hii inatia hasira sana kwani fedha nyingi ninaishia mikononi mwa majangili wachache na kuwaacha wahusika wanaotumia gharama nyingi kuaadaa kazi zao wakifa maskini.
Naomba sehemu wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwezekana wafilisiwe ili iwe funzo kwa watu wengine wenye tabia kama hii.
(PICHA ZOTE NA DIRA MEDIA)
Post a Comment