MAKUNDI HAYA YA WAIMBA INJILI YANAFAIDA GANI KATIKA MWILI WA YESU?
DAVID ROBERT |
Ni ukweli usiofichika kuwa kuna hali ya kutoelewana kwa waimbaji wa muziki wa injili. Hali hiyo inadhibitishwa na makundi yaliyopo na kila kundi kujiona lenyewe ndiyo zaidi ya lenzake.
Hali hii ndiyo iliyopelekea watu mbalimbali waione hali hii na kusema kuwa hakuna umoja kwa waimbaji wa muziki wa injili nchini.
Makundi menyewe ndiyo haya.
1. Habati Bukuku, Bony Mwaitege na Martha Mwaipaja.
2. Christina Shusho na Upendo Nkone.
3. Jenifer Mgendi, Jeni Miso na Neema Mwaipopo.
4. Ambwene Mwasongwe, David Robert na Ado November.
5. Upendo Kilahilo, Debora Saidi na Stella Joel
6. Victor Aron, Sifa John na Joshua Makondeko
7. John Lisu, Pastor Safari na Jackson Benty.
Haya ndiyo makundi makubwa ambayo hata kwenye mialiko utakuta mara nyingi hayachangamani sana. Wapo pia waimbaji wa muziki wa injili ambao pia huwa hawapendi kupanda jukwaa moja. Hawa nao siku moja TGM itawaweka wazi.
Kwa hali hii muziki wa injili tunaupeleka wapi? Yawekana kuna makundi mengine TGM haijayataka na wewe msomaji unaweza kunitajia kwa njia email lengo ni kuondoa hali hii na kuwa kitu kimoja.
One Response to “MAKUNDI HAYA YA WAIMBA INJILI YANAFAIDA GANI KATIKA MWILI WA YESU?”
fanya utafiti sio unakurupuka kuwakilisha mawazo yako kwa sababu zako za msingi. kuna sababu ya msingi ya kusema kuna makundi wakati wengine uliowaweka ktk makundi tofauti wamekua wakifanya tour/matamasha pamoja mara kadhaa.nafkiri una sababu zako,na wewe ndio unataka makundi yawepo. watu pengine wamezoeana ndo maana wanafanya kazi pamoja,au wana sali pamoja na si lazima wanamuziki wote wawe wanajuana na kuzoeana kiasi cha kufanya kazi nying pamoja.pengine sababu ya kutofanya kazi pamoja ni kwamba hawajuani,na once wakikutanishwa watafanya tu kazi pamoja.angalia kwa makini,chunguza ndo uandike si kukurupuka kisa una kjukwaa la kupotosha watu
Post a Comment