PETER BANZI MWIMBA INJILI ANAYEKUJA NA STAILI YA HIP HOP GOSPEL
![]() |
Muonekano wa kava |
Ninja wa Yesu |
Ameanzaa muziki tangu mwaka 1994 akiwa shuleni ya msingi akiimba katika kwaya ya watoto wa kanisa Katoliki usharika wa Iwambi mkoani Mbeya.
Amefanikiwa kukamilisha albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la ‘Sunday’ yenye nyimbo 13 zenye radha tofauti kama Hip Hop Gospo,Dansor,
na aina tofautii ya ladha ya mzingi ambayo ni ngeni masikioni mwa watu wengi.
Ukifanikiwa kuipata albamu hiyo naamini hutachola kuisikiliza kwani ujumbe wa nyimbo hizo ni mzito na unamguso wa hali ya juu.
Wimbo wake wa kwanza kuachia ulikuwa Mfaliji wa Moyo ikiwa na miondoko ya hip hop na ilifanya vizuri sana na kushika katika vituo mbalimbali vya redio za dini.
Wimbo wake mwingine ulikuwa unaitwa Bwana Usiniache ambao nao uliwagusa sana wadau wa muziki wa injili na mpaka sasa unafanya vizuri.
Mwimbaji huyo ametoa wito kwa vijana wenzake kujituma katika kumtumikia Mungu kwani hakuna maisha tamu kama ya kumpa Mungu utukufu kwa kumtegemea yeye kwa kila jambo. Ninjaa wa Yesu ni kijana mtanashati na swaga kibaoo za kumtukuza Mungu anayempigania kila iitwapo leo. Amewataka vijana wenzake wenye swagga kama yeye kuzielekeza kwa Yesu.
Hivi karibuni atatoa video yake iitwayo ‘Umenitowa Chini Umeniweka Juu’.
Post a Comment