SOLOMONI MUBWA AJA NA TAMASHA LA KUSAIDIA YATIMA
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya, Solomoni Mkubwa ameandaa Tamasha kubwa la injili ambalo litafanyika Agosti 19, 2012 katika Ukumbi wa Kanisa la City Christian Center (C.C.C) Upanga.
Akizungumza na TGM leo asubuhi, Solomoni alisema kuwa lengo la tamasha hilo alilolipa jina la Asante Concert ni kurudisha fadhila kwa Watanzania kwa kuipokea kazi yake vizuri na fedha itakayopatikana itatumika kujenga kituo kikubwa cha kulelea watoto yatima maeneo ya Bunju jijini Dar es Salaam.
Waimbaji watakaoimba siku hiyo ni Bony Mwaitege, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upedo Kilahiro na Jenifer Mgendi.
Post a Comment