REMERA WA KWAYA YA AMBASSADORS OF CHRIST KUFUNGA PINGU ZA MAISHA KESHO
Remera na mumewe mtarajiwa Ronnie wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mwimbaji huyo kufanyiwa sherehe ya kuangwa hivi karibuni - Picha kwa hisani ya KJ Marcello Velosco. |
Mwimbaji wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kanisa la Waadventista Wasabato ya nchini Rwanda, Remera Ngamije Thamar ‘Tammy’ kesho atafunga pingu za maisha na Ronnie jijini Kigali.
Remera ambaye ni kipenzi cha wadau wa muziki wa injili nchini Tanzania kutokana na kuiimba vema sauti ya kwanza na yapili muda mwingi ameonekana mwenye shauku ya kuisubiri siku hiyo na kuanza safi ya maisha ya ndoa.
Wiki iliyopia mwimbaji huyo alifanyiwa sherehe ya kuangwa rasmi na waimbaji wenzake wameandaa zawadi mbalimbali za kumpa ili akaanze maisha mapya kwa raha zote na mumewe mtarajiwa bwana Ronnie.
Ngamije Thamar kushoto akiwa na dada yake wakati wa sherehe hizo za utambulisho.
Post a Comment