TAMASHA LA IPENDE TANZANIA KUITEKA DAR ES SALAAM LEO
Christina Shusho ataimba katika tamasha hilo |
Tamasha Ipende Tanzania lililokuwa linasubiliwa kwa shauku kubwa leo linatarajia kuiteka Dar es Salaam baada ya kuonekana kupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wakazi wa jiji hilo.
Tamasha hilo linalotarajiwa kuanza majira ya saa 7:00 mchana katika viwanja vya Jangwani chini ya muhubiri wa kimataifa Andrew Palau na timu yake na waimbaji maarufu wa muziki duniani ambao watakwenda sambamba na waimbaji wenyeji katika kumsifu Mungu huwenda likaweka historia ya kipekee katika matamasha ya injili nchini.
Kutakuwa na michezo mbalimbali kabla ya kuanza mahubiri majira ya saa 10:00 jioni na linatarajiwa kumalizika kesho.
Kutakuwa na michezo mbalimbali kabla ya kuanza mahubiri majira ya saa 10:00 jioni na linatarajiwa kumalizika kesho.
Post a Comment