Rose Muhando aikubali Eck Production
ROSE MUHANDO - PICHA KWA HISANI YA MTANDAO |
Malkia wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando amekiri ubora wa kurekodi wa Eck Production ni wa hali ya juu ndiyo maana kazi zake nyingi hurekodia hapo.
Akizungumza na TGM hivi karibuni, Rose alisema amepita katika studio nyingi za kurekodi albamu zake lakini hazijafikia ubora wa Eck Production ndiyo maana kwa sasa ameamua kwa sasa kazi zake anazifanyia hapo.
“Sisemi kwa unafiki hakika studio ya Eck Production iliyo chini ya Enock Nyongoto ni nzuri kwani tangu niitambue kazi zangu zote nimekuwa nikifanyia hapo hata nyimbo zangu ambazo zitasambazwa na kampuni ya Sony nitazirekodia kwake,” alisema Rose.
Mwimbaji huyo aliendelea kusema kuwa, kwa kulitambua hilo baadhi ya waimbaji wenzake wa muziki huo nao wameanza kurekodi katika studio hiyo iliyopo Mwembechai jijini Dar es Salaam.
Waimbaji ambao kazi zao hasa mpya wamezifanyika katika studio hiyo ni Bahati Bukuku, Upendo Nkone, Upendo Kihailo, Stella Joel, Mchungaji Jangala Soni na wengine wengi.
Post a Comment