NJIA ZA WAIMBA INJILI WENGI HAZIKO SAWA
Baadhi yao wanaishi kama hawajaokoka
Wengi wanaongoza kwa masengenyo, uongo, uzinzi, chuki, majivuno na kujikweza.
Hakuna ubishi juu ya suala hili kwamba waimbaji wengi wa muziki wa injili hawaishi maisha yanayompendeza Mungu na kushindwa kujua kama wanamtumikia Mungu aliyehai.
Waimbaji wengi nao wanaandamwa sana na dhambi ya usengenyaji, uongo, uzinzi, chuki, majivuno na kujikweza na nyinginezo hali inayoshindwa kuwatofautisha na watu wasiookoka.
Siku moja niliwahi kumuuliza mwimbaji mkubwa hapa nchini juu ya suala hili naye akajibu kuwa, suala kufanya dhambi hizo halikwepeki kwani baadhi ya waimbaji huwa wamefungwa na roho za mababu ndiyo maana wanashindwa kujinasua na tatizo hilo.
Ukisikiliza nyimbo zao unashawishika kumurudia Mungu aliye hai. Ukifuatilia matendo yao yanaweza kukurudisha nyuma kiroho hakika suala hili linaniumiza sana.
By George Kayala
Post a Comment