Mjue Kabula J.George
Kuna siri kubwa katika uimbaji, ni zaidi ya kusikiliza ala za muziki na sauti nzuri ya muimbaji, Uimbaji unaomgusa Mungu lazima utawagusa na watu pia, watu wataokoka, wataponywa na watagangwa mioyo yao kupitia uimbaji.
Ni imani yangu kuwa mwimbaji bora wa nyimbo za injili ni yule kwanza awe ameokoka kweli na mwenye lengo kweli la kuwafikia watu wa Mungu au wa mataifa katika kuwapa neno la Mungu na kuwaasa waache anasa na si kwa lengo lingine lolote hapo liwe la kufanya biashara au kujulikana kwa watu.
Mwimbaji wa muziki wa injili Kabula John George ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi hiyo kupitia kipawa chake alichopewa na Mungu. Tayari amefafanikiwa kutoa albam ya nyimbo za injili inayojulikana kwa jina PESA na inasambaza na Mam Store.
Watu wengi wamezipenda nyimbo zake kutokana na ujumbe mzuri uliomo na radio mbali mbali za kidini zinacheza nyimbo hizo. Radio ambazo kwa sasa zinapinga nyimbo za dada Kabula ni Wapo Radio, Prise Power zote za
Kabula ambaye kwa wanamuita "Mama Pesa" kutokana na wimbo wake wa PESA aliouimba kwa mahadhi ya zuku anatoa huduma mbalimbali katika makanisa ya mkoa wa Dar es Salaam na yupo tayari kutoa huduma hiyo ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na nje ya nchi.
Mwimbaji huyo amekuwa akiwagusa watu wengi wanaozisikiliza nyimbo zake hizo na wamekuwa wakimwalika katika mikutano mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma hiyo ya kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya Uimbaji.
Dada Kabula anawakaribisha watumishi wote wa Mungu kumwalika katika semina, mikutano, makongamano n.k kwa ajili ya kulitangaza neno la Mungu wetu kupitia huduma hiyo ya uimbaji.
Nyimbo zilizo katika albam hiyo ni
1.Milele
2.Pesa
3.Ninamjua
4.Nkomoji (wimbo wa Kisumuma)
5.
6.Tunakulilia
7.Yatima
. Nakupa utuku na
. Niguse.
Mwimbaji huyo kwa sasa anajiandaa na kurekodi mkanda wa video wa albam hiyo ambayo inatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa.
Kwa mawasiliano zaidi mpigie simu no:- 0757- 140 336 au 0755 – 240 136
Ama kwa njia ya Email- kabulageorge@yahoo.com
Yupo tayari kufanya nawe huduma mahala popote pale kwa lengo la kumtangaza Mungu.
Post a Comment