Upendo Nkone: Nitafanya 'sapraizi' siku ya harusi yangu
Wapendwa katika Yesu Kristo leo nimefanikiwa tena kukutana na muimbaji wa muziki wa Injili nchini anayekwenda kwa jina la Upendo Nkone ambaye nimefanya naye mazungumzo kwa ajili ya maandalizi ya harusi yake ungana nami ili upate kile alichokizungumza.
TGM: Bwana Yesu asifiwe Upendo
UPENDO: Amee, kwa jina naitwa Upendo Nkone ni mwenyeji wa Kigoma, nimezaliwa katika familia ya kilokole na kulelewa katika maadili ya dini ambayo yamenifanya mpaka leo hii nionekana katika jamii nikimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
TGM: Lini hasa ulianza rasmi kujihusisha na masuala ya muziki wa injili?
UPENDO: Swali zuri, binafsi suala ya uimbaji nililianza nikiwa na miaka mitano (5) kwa sababu muda mwingi nilikuwa nasikiliza nyimbo za dini kupitia radio ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kwenda kanisani ambako nilikuwa nawaona wanakwaya wakiimba nami kuwa navutiwa nao.
TGM: Upo kwenye game ya muziki wa injili kwa muda mrefu sasa, mpaka sasa umepata mafanikio gani kutokana na huduma hii ya kumuimbia Mungu?
UPENDO: Nianze kwa kusema kuwa, mpaka sasa nimefanikiwa kutoa albamu zangu tatu. Ya kwanza ilijukina kama Mungu Baba, yapili niliita Hapa nilipo na ya tatu inakwenda kwa jina la Zipo faida. Namshukuru Mungu kupitia huduma hii nimepata mafanikio makubwa sana. Miongoni mwa hayo ni kupata marafiki wengi ndani na nje ya nchi wanaopenda huduma yangu, ninasomesha wanangu kwenye shule za kimataifa (International), ninausafiri wangu na sasa ninajenga bonge la nyumba maeneo ya Mbezi.
TGM: Hivi karibuni ilielezwa kuwa, umeshampata mwenza wako wa maisha ambaye hukupenda kumuweka wazi, je harusi itakuwa lini?
UPENDO: Na nyinyi wadaku huwa hampitwi na jambo. Ni kweli Mungu ameshajibu kiu ya kuwa na mume wa kufanana na mimi, lakini suala na lini ndoa yangu itafungwa linabaki kuwa siri ya familia yangu na upande wa mwenzangu, na nimedhamilia kufa ‘sapraizi’ siku ya harusi yangu.
TGM: Vipi kuhusu umarufu wako, unakusaidia katika maisha yako ya kila siku?
UPENDO: Kwa namna moja ama nyingine unanisaidia kufanikisha baadhi ya mambo, lakini asilimia kubwa ni mateso. Kwa mfano kwa muda wa miaka 9 ya ujane wangu nimeishi maisha ya mashaka na wasiwasi wa kufanyiwa lolote baya. Kwa sababu sina uhuru wa kutangulizana na mwanaume yeyote hasa nyakati za usiku kwa sababu watu wanaweza kufikiri kitu kibaya. Kwa kifupi umarufu ni mateso.
TGM: Mbali na uimbaji wa muziki wa injili, unafanya kazi gani.
UPENDO: Nafanya kazi ya kushona, taaluma yangu ni fundi chelehani na hivi karibuni natarajia kufungu ofisi yangu hapa mjini.
TGM: Nini malengo yako kuhusiana na huduma ya uimbaji wa muziki wa injili.
UPENDO: Nataka kumurumikia Mungu wangu kwa uimbaji kwa viwango vya juu kuliko ilivyosasa.(Picha kwa hisani ya blog ya Jiachie)
3 Responses to “Upendo Nkone: Nitafanya 'sapraizi' siku ya harusi yangu”
amina dada Mungu akubariki na mungu akutie nguvu zaidi mapka ushangae.
Nabarikiwa sana na nyimbo zako
Grace mashimba
ZANZIBAR
Mungu akutie nguvu sana kwa yeye ndio anayajua yote. atakutetea kwa kila hali.
Usiolewe muda wako umepita. Msubiri Mungu. Wanaume siku hizi si wema, wanaweza wakufanye usifanye vyema kwenye music wako.
Post a Comment