Thursday, October 13, 2011

Rose Muhando apata pigo







Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini Rose Muhando amepata pigo baada ya kufiwa na dada yake Salma Muhando usiku wa kuamkia leo na msiba uko nyumbani wako Tanga, Kilindi. Wadau wote wa Rose tuko naye katika hali hii ya majonzi na Mungu ailaze mahala pema pepo roho ya marehemu, kwani Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.

Tuesday, August 16, 2011

RADIO USHINDI FM


Ni radio ya watu wote katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. Inapatikana katika masafa ya 98.6. Inarusha matangazo yake kutoka jijini Mbeya. Karibu uburudike kiroho na kimwili.

SEMINA YA MWALIMU MWAKASEGE

Mwalimu Christopher Mwakasege anatarajiwa kuendesha semina ya Neno la Mungu Septemba 4, 2011 mpaka Septemba 11, 2011 kwenye Viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Semina hiyo itakuwa inaanza saa 9 alasiri mpaka saa 12 jioni kila siku. Semina hiyo imeandaliwa na Kamati ya Maandalizi ya Mwl.Christopher na Diana Mwakasege, watu wote mnakaribishwa. Picha kwa hisani ya Amani masue bloG

Saturday, July 30, 2011

J. SISTERS KUZINDUA ALBUM CHUKUA USHINDI


Kundi la Muziki wa Injili la J SISTERS linaloundwa na wanamuziki ndugu JENNFFER, JESSICAR , JAQUILLINE na JULIET linatarajiwa Kuzindua albamu yao ya tatu inayojulikana kama CHUKUA USHINDI Jumapili hii ndani ya ukumbi wa DIAMOND JUBILEE.
Mgeni rasmi katika shughuli hiyo anatajiwa kuwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete litanogeshwa na waimbaji wa muziki wa Injili nchini kama Frola Mbasha, Bonny Mwaitege, Martha Maipaja na wengine wengi. Kiingilio cha juu ni shilingi 10,000, 5,000 na 3000 kwa watoto.

Friday, July 29, 2011

HAKIGRAM IKITUMIKA IPASAVYO ITAWANUFAISHA WASANII

Endapo serikali itafanikiwa kuwabana wasambazaji wote wa kazi za wasanii nchini kwa kubandika stika ya usalama itakayojulikana kama HAKIGRAM kwa kila nakala ya kazi itakayosambazwa itadhibiti wizi wa kazi hizo na kuwanufaisha wahusika.

Naungana na serikali kupitia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, alipokuwa anajibu swali Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya (CCM) mjini Dodoma Julai 27, 2011.

Ni ukweli kwamba, utaratibu wa kila msambazaji kuingia mkataba na msanii kusambaza idadi flani ya nakala na kupewa stika za HAKIGRAM ambazo zitabandikwa kwa kila nakala kutawezesha kujua msanii kauza nakala ngapi na kwa muda upi.

Kazi nyingi za wasanii wa Tanzania zinauzwa kinyume na sheria  nchi za Congo, Burundi, Malawi, Rwanda na Zambia.

Waharamia wa kudurufu kazi za wasanii wametajirika huku wahusika wakiwa katika hali ya umasikini na wanafanya bila uoga kutokana na kosekana kwa sheria ya kuwabana moja kwa moja.

Nasema hivyo nikiwa na ushahidi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Auction Mart, Alex Msama ambaye amekuwa akipambana na maharamia hawa kila kukicha.

Hivi karibuni Msama alifanikiwa kukamata mtambo mmoja mkubwa wa kudurufu CD wenyewe uwezo wa kuzalisha CD feki 300 ndani ya dakika 20.

Na ili zoezi hili lifanikiwe inatupasa waimbaji wote wa muziki wa Injili na wadunia kuungana kwa pamoja ili kuondoa ujangili huu ambao unadidimiza maisha ya wasanii huku wasiohusika wakitajirika.
Mpaka sasa Msama amefanikiwa kuwakamata baadhi ya wanyonyaji kama Fred Jumbe, Martin Mkinga na Mstafa Rashidi.

SHIKA YESU BEND IKIMTUKUZA MUNGU NDANI YA BUSTANI YA EDENI JULAI 26, 2011


ELIZA AKIIMBA PAMOJA NA KABULA GEORGE WAKIIMBA JULAI 27,2011




KABULA J.GEORGE AKIIMBA NDANI YA HUDUMA YA NENO LA UPATANISHO ILIYOPO BUSTANI YA EDENI



 Waunimi wakifuatilia uimbaji wa Kabula

Thursday, July 21, 2011

VIONGOZI WA DINI NA MADAWA YA KULEVYA

Ni Mungu yupi wanayemtumikia viongozi hawa wa dini wanaojihusishwa na madawa ya kulevya?
Swali hili nimekuwa nikijiuliza kila siku kuwa, watumishi hawa wa Mungu wanaojihusisha na madawa ya kulevya huku wanapanda kwenye madhabahu kuhubiri neno lake, ni Mungu yupi wanayemhubiri?
Wanaupata wapi ujasili wa kuhubiri neno la Mungu huku nyuma ya pazia wanatambua kuwa wanafanya matendo ya kuangamiza watu kwa kuwauzia madawa ya kulevya.
Iweje watumie kivuli cha uchungaji, uaskofu, utume na unabii kwa kuwadanganya waumini kuwa, utajiri walionao wameupata kutokana na baraka za Mungu?
Wanafanya hivyo kwa faida ya nani? Leo Mungu akiwaita kwake watajitetea nini? Watumishi hawa wanalipeleka wapi kanisa la leo?
Ina maana hawana uhakika wa kutajirishwa kihalali na Mungu wanayemhubiri mpaka watumie njia za mkato?
Tunawaona wamevaa vito vya thamani mwilini mwao na magari ya kifahali wengi tukijua Mungu kawabariki kumbe shetani ndiye kawafanya wawe hivyo.
Jamani kanisa linaelekea wapi? Kuna kila sababu ya kutulia kwenye magoti na kuliombea taifa liondokane na viongozi wa namna hii.
Viongozi wa dini tunaowategemea kukemea maovu leo hii wao ndiyo watenda maovu wakubwa.
Namshukuru Mungu kwa neema tuliyonayo ndiyo maana watumishi hao leo hii ndiyo maana wanafanya maovu mengi bila kudhurika na amewapa nafasi nyingine ya kutubu kwani yeye ni mwingi wa rehema.
Naungana na viongozi hao waliokuwa wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kuiomba Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii kuficha majina yao na madhehebu kwa ajili ya usalama wao.
Ni ukweli kuwa, Kamati hiyo ikitaja majina yao ni dhahili kwamba waumini wao watarudi nyuma kiimani na kuyahama makinisa hayo ikiwa ni pamoja na kujenga chuki dhidi yao hasa kwa viongozi ambao ndiyo wasisi wa madhehebu husika.
Pamoja na hayo bado serikali inauwezo wa kufanya inaloona linafaa kuhusu viongozi hao wanaolidhalilisha jina la Yesu ambaye wanamtangaza kila siku kwa wafuasi wao.
Naleta hoja hii kwenu wasomaji wa mtandano huu, je ni vema Kamati kuendelea kuwakumbatia viongozi hawa kwa kuficha majina yao ama wayaweke hadharani?
Mchango wako ni wa muhimu sana kwa ajili ya manufaa ya Watanzania wote. Nikukumbushe kuwa, suala hili liliibuliwa na Rais Kikwete Juni 5 mwaka huu katika sherehe za kumsimika Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbinga kwa kuwataka viongozi wa dini nchini kuacha tabia ya kushiriki biashara ya madawa ya kulevya.
Hata hivyo kauli hiyo ilionekana kupingwa na baadhi ya viongozi wa dini na kusema kuwa, rais amewadhalilisha na kumtaka awatajie majina ya watuhumiwa hao.

Monday, July 18, 2011

MWINJILISTI WA KIMATAIFA KABULA GEORGE AWAPONGEZA WAKENYA

Mwinjilisti wa kimataifa Kabula J.George amewapongeza wananchi wa Kenya hasa mkoa wa Kisii kwa mapokezi yao mazuri waliyompa kwenye kanisa la Mlima wa Sayuni na kumwandalia mkutano mkubwa wa nje ulioponya watu wengi.
Kabula amewashukuru waumini wa kanisa hilo kwa ukarimu wao wote waliouonesha kwa muda wa wiki moja akiwa kanisani hapo kwa ajili ya kulihubiri neno la Mungu kwa njia ya uimbaji na kuhubiri.
Anashukuru Mungu pia kutumia wachungaji wote wa kanisa hilo pamoja na Edward Makoli. Kabula alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha waumini hao kuja Tanzania kwa ajili ya kulitangaza neno la Mungu.

Sunday, July 17, 2011

SEMINA YA MASOMO YA NDOA

Kutana na mshauri wa masuala ya mapenzi na ndoa George Kayala ambaye amefanyika msaada mkubwa katika ndoa za watu wengi kila pembe ya Tanzania.
Kayala amekuwa akizunguka katika makanisa mbalimbali kwa ajili ya kutoa somo la ndoa hasa kwa wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume. Ndoa nyingi zimekuwa zikivunjika kutokana wanaume kushindwa kuwafurahisha wanaume wawapo faragha.

Kwa mialiko ya semina za ndoa piga simu namba +255755240136 ama +255656215572.