LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

EUGINE KUSHUHUDIA UZINDUZI WA HESABU BARAKA



Joyce Mwaikofu
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Mhe. Eugine Mwaiposya anatarajia kushuhudia uzinduzi wa albam ya pili ya mwimbaji wa nyimbo za  injili nchini, Joyce Mwaikofu itwayo Hesabu Baraka utakaofanyika Agosti 4 mwaka huu ndani ya kanisa la EAGT Kipunguni A Ukonga Banana barabara ya Kitunda ikiwa katika mfumo wa DVD.
Akizungumza na Tanzania Gospel Music jana jijini Dar es Salaam, Joyce alisema kuwa Mwaiposya ataungana na mbunge mwenzake wa Iramba Magharabi Mhe. Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mgeni rasmi katika uzinduzi huo wenye  lengo la kuchangisha  fedha za kununulia vyombo vya muziki na nyingine kumalizia ujenzi wa kanisa hilo linaloongozwa na mmewe mchungaji John Mabega.
 “Mwaiposya amekubali kuungana na Nchemba katika uzinduzi wa albam yangu ya pili na nina amini kuwa uwepo wao utawezesha kupatikana kwa fedha za kununulia vyombo vya muziki ambavyo vitatumika kanisani pamoja na kumalizia ujenzi wa jengo la kanisa hilo,” alisema Joyce.
Mwimbaji huyo ambaye kitaaluma na mwanasheria wakili alisema kuwa, uzinduzi huo utanogeshwa na wakali wa nyimbo za injili ambao atawaweka hadharani wiki hii baada ya kukamilika mazungumzo kati yake na wao na amewataka mashabiki wa muziki huo kufika kwa wingi siku tukio.
“Nimeanza kuongea na waimbaji mbalimbali ambao ni wakali wa nyimbo za injili nchini na nitawaweka hadharani mapema wiki hii hivyo nawatakama mashabiki wa muziki wa injili kufika kwa wingi katika tukio hilo ili kuwezesha kupata fedha hizo ambazo zitaendeleza kazi ya Mungu,” alisema mama mchungaji.
Joyce alisema kuwa uzinduzi huo ambao hautakuwa na kiingilio utaanza saa 7:00 mchana na kumalizika saa 12:00 jioni.

Newer Post Older Post