FANUEL SEDEKIA ATAKUBMBUKWA KWA TUNGO ZAKE KALI
Aliyekuwa muimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini Fanuel Sedekia alizikwa Januari 10 mkoani Arusha baada ya kufariki dunia usikua wa kuamukia Januari 5 akiwa nchini Israel alikokuwa ameenda kufanya ibaada ya kuhiji yeye pamoja na wakristo wengine wakiongozwa na Mwalimu Christopher Mwakasege.
Katika mazishi wa kumuaga marehemu karibu waimbaji wote wa muziki wa injili chini walihudhuri pamoja na waimbaji wa muziki huo kutoka nchi jirani na mwili wa wake uliagwa katika Uwanja wa mpira wa miguu wa Sheh Amri Abed kabla ya kwenda kuwekwa katika nyumba yake ya milele.
Sedekia atakumbukwa zaidi na Watanzania kutokana na tungo zake kuwa kali na zilimgusa kila aliyezisikiliza. Mwimbaji huyo enzi za uhai wake aling’ara na traki kali za muziki wa nyimbo kama vile Ametenda Maajabu, Upendo,Nani Kama Wewe na Unaweza. Hili ni pigo kubwa kwa fani ya muziki huo hapa Afrika Mashariki kwa maana bado mchango wake ulikuwa inahitajika katika fani hiyo lakini binadamu hatuwezi kuhoji zaidi kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa.
Chanzo cha kifo cha msaniii huyo kimeelezwa kuwa ni athari za ugonjwa wa kisukari, Nimonia pamoja na ubongo kutofanya kazi vizuri. Hali hiyo ilijitokeza wakati mtumishi huyo wa Mungu akiwa safarini nchini Israel katika kutekeleza ibada ya hija ambapo alikimbizwa katika hospitali ya Poriya Tiberia nchini humo na kulazwa kwa muda wa wiki tatu akiwa hajitambui.
Kwa muda wote huo marehemu alikuwa pamoja na Mhubiri wa Kimataifa Mchungaji Christopher Mwakasege ambaye kwa muda mrefu wamekuwa akifanya kazi kwa pamoja.
Hata hivyo kituo cha Radio Wapo cha jijini Dar es Salaam kilimkariri mmoja wa ndugu wa Sedekia akisema kuwa mwanamuziki huyo alifika nchini Israel kwa ajili ya shughuli za hija akiwa salama lakini baadaye aligundulika kuwa na matatizo hayo yaliyosababisha alazwe kwa muda wa wiki tatu sambamba na kupoteza fahamu hadi alipofikwa na mauti Januari nne mwaka huu.
Hata hivyo ilielezwa kuwa waganga na wauguzi wa hospitali ya Poriya Tiberia walitumia uwezo wao wote kuhakikisha wanaokoa maisha ya muimbaji huyo na kuweza kufanikiwa kuondoa tatizo la sukari mwilini ambacho kilionekana kuwa ni kiini cha tatizo ila mwili ulikosa nguvu, ubongo kutofanya kazi vizuri na kupelekea kushindwa kuamka huku akilishwa chakula kwa kutumia mipira.
Awali kulikuwepo na taarifa za kifo cha msanii huyo ambazo zilikuwa ni uvumi, ikiwa ni muda mfupi baada ya kutua nchini Israel, hata hivyo uvumi ambao ulikanushwa vikali na watu wakaribu na marehemu lakini walikiri kuwa alikuwa ni mgonjwa na alikuwa amelazwa katika hospitali ya Poriya Tiberia ya nchini humo akiwa mahututi.
Fanuel Sedekia alizaliwa mkoani Kigoma miaka kadhaa iliyopita kisha kuhamishia makazi yake mkoani Arusha alikokuwa anafanya shughuli za muziki wa Injili hadi alipofariki duniani.
Hadi sasa haijaweza kufahamika mara moja kuwa mwili wa msanii huyo utazikwa mjini Arusha alipokuwa anaishi yeye pamoja na familia yake au utazikwa mkoani Kigoma alipozaliwa.
Kifo cha mwimbaji huyo kimeacha pengo kubwa katika fani ya muziki wa Injili katika ukanda wa Afrika Mashariki kutoka na umahiri wake wa utunzi na uimbaji wa nyimbo za taratibu ambazo wengi wanaziita ni nyimbo za kuabudu.
Fanuel Sedekia atakumbukwa na kazi zake matata kama, Nani Kama Wewe, Jina Lake, Moyoni, na Unastahili Kuabudiwa, Ni wewe Bwana ambazo zitaendelea kuwafariji mashabiki wa muziki wa Injili sehemu mbalimbali Afrika Mashariki.
Mwaka jana fani hiyo ya muziki wa Injili katika ukanda wa Afrika Mashariki ulipata pigo kubwa baada ya wasanii wawili mahiri kufariki dunia kwa matukio mbalimbali.
Wasanii hao ni Debora Shaaban wa Tanzania aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu pamoja na Angela Chibalonza raia wa DRC Congo aliyekuwa anafanya shughuli zake nchini Kenya, alifariki kwa ajali ya gari iliyotokea nchini Kenya.
Mpaka mauti yanamkuta, Fanuel Sedekia alikuwa na albamu saba ambazo zitaendelea kuwa chachu ya mahubiri kwa njia ya uimbaji na zimekuwa gumzo katika vituo vya radio za Kikristo.
Albamu hizo ni Yupo Mfariji, Umaweza tena, Ametenda maajabu, Uwepo wako, Kwa sababu ya pendo, na Katika Ibada.
6 Responses to “FANUEL SEDEKIA ATAKUBMBUKWA KWA TUNGO ZAKE KALI”
JAMANI KWA KWELI INASIKITISHA NA KUSHTUA SANA KWA HABARI KAMA HIZI. HIVI WAPENDWA TUJIULIZE KAMA MUNGU ANACHUKUA WATU WANAOMWIMBIA KILA SIKU NA KUMTUKUZA YEYE, SISI WENYE DHAMBI AMBAO MIDOMO YETU KILA MARA HUTUKANIA MATUSI, KUSEMA UONGO, KUTONGOZEA KINA DADA TUNABAKI HIVI INAKUWAJE? INABIDI TUJIRUDI SASA. SI KWAMBA SISI NI WEMA MBELE ZA BWANA KULIKO SEDEKIA!!! MUNGU ATUSAIDIE. NITAMKUMBUKA KWA WIMBO WAKE MZURI WA "NI WEWE" AMBAO KILA NIUSIKIAPO HUJISIKIA VEMA. KWA UJUMLA NI ALBUM NZIMA YA "KATIKA IBADA". TUTUBU DHAMBI ZETU. BY ALEXANDER GEOFREY MUGANYIZI. 0784 736616 SUMBAWANGA TANZANIA
NIMESITIKA SANA BAADA YA KUPATA TAARIFA ZA KIFO CHA SEDEKIA, NAAMINI MUNGU ATAMLIPA KWA KAZI YAKE YA KULIINUA JINA LAKE KUU LIPITALO YOTE ULIMWENGUNI.
NITA MKUMBUKA KWA ALBUM ZAKE ZOTE.
BY BHOKE LAMECK.MASASI-MTWARA
I am shocked!During Kenyan post election violence I happened to come across Sedekia's music on youtube.Being away from home it became our comforter.
Since then I have been a great admirer of his.
May God rest his soul and comfort his family.
Nami nazipokea habari za Tanzia ya Muimbaji maarufu Fanuel Sedekia kwa mshtuko mkubwa. Ni ombi langu kuwa familia yake pamoja na waimbaji wake kama Neema Alfayo, John Paul, Godwin Ombeni na wengineo watafarijika.
Oh No,..Fanuel Zedekiah…! Dead…!!?
He was a great man of God.I adored him for the very precious gift God gave Him.
When I ran into the news about His unexpected departure,I couldn’t stop my tears from rolling ,struggling to believe the unbelievable.
Zedekiah was honestly an exceptional gospel ambassador,an ordained gospel-pop-star, not only in His mother-state TZ, but in Africa.
I loved his gospel masterpiece very dearly.They happened to be my favorite collection.His nourishing gospel melodies always touched my heart,bringing me so intimate to God,and making me feel God never forgets about his sons.
May God lay His precious soul in eternal peace.
We loved you Fanuel,but God loved you the most.We gona miss big.
Its my sincere condolence to the family, relatives, funs and friends.
Tumeskitishwa sana na KIfo cha Mch. Feanuel Sedekia. Lakini amempenda kuzidi sisi. Mungu atunze Roho yake.
Post a Comment